Tuesday, January 17, 2017

WANAFUNZI 17,549 KUJIUNGA NA ELIMU YA SEKONDARI MKOANI IRINGA

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu (kushoto) ambaye pia ni Katibu wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa (RCC) akisoma taarifa katika kikao hicho huku Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza ambaye pia mwenyekiti wa kikao hicho akifuatilia kwa makini leo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Suzana Mgonukulima (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, Menrad Kigola (CCM) wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa wa Iringa (RCC kilichofanyika leo


IRINGA: Jumla la wanafunzi 17,549 mkoani Iringa (wavulana 7,988 na wasichana 9,561) sawa na mkiondo 439 watajiunga kidato cha kwanza mwaka 2017, imeelezwa.

Hayo yalisemwa na Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Iringa Richard Mfugale (pichani) wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa (RCC) kilichofanyika leo mjini Iringa.

Kaimu afisa elimu huyo alisema kuwa wanafunzi wote waliofauli wamechaguliwa kujiunga elimu ya sekondari mkoani iringa, ambapo aliongeza kuwa halmashauri zote zinaendelea na maandalizi ya kupokea wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Mfugale alisema kuwa ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne kimkoa umepanda kutoka asilimia 65.25 mwaka 2013 hadi asilimia 72.34 mwaka 2015, hali kadhalika kwa halmashauri ya manispaa ya iringa na halmashauri ya wilaya ya iringa ufaulu umekuwq ukiongezeka. 

Kwa upande wa mtihani wa kidato cha sita, Mfugale alifafanua kuwa kati ya wanafunzi 4,142 waliohitmu kidato hicho, wanafunzi 4,055 sawa na asilimia 97.88 ya walifauli kwa kiwango cha daraja la kwanza hadi la nne.

Alifafanua kuwa kati yao hao waliofauli asilimia 95.6 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu wamechaguliwa kujiunga na vyuo vikuu na vyuo vingine nchini.

Wakati huohuo, mjumbe wa kikao hicho, Mendrad Kigola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini alisema kuwa ili kuwepo boreshaji elimu, halmashauri za wilaya hazinabudi ya kutenga kiasa cha pesa kutoka katika kwenye bajeti zao kwa ajili ya maendeleo ya elimu.

Alisema kuwa ili kuunga juhudi za serikali katika sera yake ya elimu bure ni lazima halmashauri zitoe mchango wake.

Aidha, mjumbe huyo alishauri pia kuwa kuwepo na jitihadi za makusudi mazima za kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuhusu elime bure ili kupunguza malalamiko na mkanganyiko uliopo wa suala la sera ya elimu bure.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More