Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuna baadhi ya watu wamejipenyeza na
kutaka kuiibia Serikali kupitia suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi
wanaopisha miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.
Amesema
kuwa Serikali haiko tayari kuona wananchi hao wakitumika kama madaraja
ya wizi kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wanaojipenyeza ili
kuiibia Serikali kwa njia hiyo.
Majaliwa
amesema hayo leo Januari 26, 2017 katika ziara ya kikazi mkoani Njombe,
ambapo amesema kuwa watu hao ambao hawahusiki na eneo hilo la mradi
wamesababisha gharama za fidia kuwa kubwa, hivyo wataalam wanatathmini
ili kubaini wahusika kabla ya kulipa.
“Tunataka
wananchi wenyewe waliokuwa hapa ndiyo tuwalipe fidia yao kwa mujibu wa
tathmini husika. Fidia yenu mtalipwa baada ya kuwaondoa wezi wote
waliojipenyeza.
“Kuna
watu wanataka kuiibia Serikali kwa mgongo wenu, hili hatutakubaliana
nalo. Tupo makini vumilieni inalifanyia kazi suala letu. Hakuna haki ya
mtu itakayopotea,” amesema.
0 comments:
Post a Comment