Polisi
mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na raia wema imewatia mbaroni watu
watatu wanaodaiwa kujifanya ni askari wa jeshi hilo na kuwaibia wananchi
fedha na mali.
Habari
zilizopatikana jana zilisema kuwa katika upekuzi uliofanywa kwenye moja
ya nyumba anayoishi mmoja wa watuhumiwa hao, kulikutwa kitambulisho cha
mwalimu aliyewahi kuibiwa mamilioni ya fedha akitokea benki.
Kwa
mujibu wa habari hizo, kundi la watu hao limekuwa likiendesha vitendo
vyake katika maeneo ya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi na mitaa
mbalimbali, hususan karibu na duka la Nakumatt.
Vyanzo
mbalimbali vimedokeza watuhumiwa hao huwakamata watu na kuwapekua kisha
kuwatuhumu kuwa fedha walizonazo au simu vimeibwa sehemu na wao ni
washukiwa wanaotafutwa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa jana alithibitisha
kukamatwa kwa watuhumiwa hao juzi saa nane mchana katika eneo la Njoro
Relini
0 comments:
Post a Comment