Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole
Sendeka kuwachukulia hatua watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa
waliohusika na upotevu wa fedha za maendeleo zaidi ya sh. milioni 700
zilizopelekwa katika halmashauri hiyo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya
maendeleo zikiwemo sh. milioni 300 za ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri
hiyo.
Majaliwa
ametoa kauli hiyo Januari 26, 2017 wakati akizungumza na wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri
alipokuwa katika ziara yake katika Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.
“Mkuu
wa Mkoa watu wote waliohusika na upotevu huu watafutwe popote walipo na
kuchukuliwa hatua na kisha nipewe taarifa ya hatua ulizochukua.
Hatuwezi kuwavumilia watu hao ambao wanachora ramani kwa sh milioni 200
na sh. milioni 100 zingine hazijulkikani zilipo,“ – Majaliwa.
Aidha,
Majaliwa amemuagiza Mkuu huyo wa Mkoa kufuatilia kiasi kingine cha sh
milioni 400 zilizopelekwa wilayani hapo kwa ajili ya maendeleo ambazo
nazo hazijulikani zilipo.
“Tafuta waliohusika popote walipo hata kama ni nje ya Njombe waje kutueleza ziliko fedha zetu,” amesema
Majaliwa
pia ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini
(TAKUKURU) kuhakikisha inashirikiana nayo inafanya uchunguzi ili kubaini
watu waliohusika na upotevu huo.
Mbali
na hayo, Majaliwa asema Serikali haitowavumilia watumishi wote
wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma, hivyo
amewataka watumishi wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na maadili.
Amewataka
watumishi wa umma nchini kuacha tabia ya kudokoa fedha za maendeleo
zinazopelekwa katika Halmashauri zao kwa sababu Serikali iko macho na
itawashughulikia wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Pia,
Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wametakiwa kusimamia vizuri
fedha za maendeleo zinazopelekwa kwenye maeneo yao na kuhakikisha
zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Kabla,
Waziri Mkuu alipokuwa njiani kuelekea Ludewa Mjini akitokea katika kata
ya Mundindi Waziri Mkuu alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha
Mlangali ambao waliiomba Serikali iwasaidie kuzipatia ufumbuzi
changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho, Michael Lameck alisema alimueleza Waziri Mkuu kwamba
awali walikuwa wanapata maji ila kwa sasa hayatoki kutokana na uchakavu
wa miundombinu hali iliyowafanya kuchangishana na kupata sh. milioni 95
kati ya 200 zinazohitajika.
Mara
baada ya maelezo hayo, Majaliwa amemuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya
hiyo, Nasib Mlenge kwenda kijijini hapo leo Januari 27 kukutana na Bw.
Lameck ili kushirikiana naye na kuangalia alipofikia na kuendeleza
uboreshaji wa miundombinu hiyo ili wananchi hao wapate maji.
“Mwenyekiti
amechangisha sh. milioni 95 na kununua baadhi ya vifaa nyinyi
mnashindwa nini. Lazima muwe makini na matatizo ya wananchi na Serikali
haitaki masuala ya urasimu. Watu wana shida ya maji na mnajua tatizo
mmekaa tu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment