Msemaji wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania, Sheikh Khamis Said Mataka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kwa niaba ya Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ali, kuhusu waislamu kote nchini kuiombea nchi ipate mvua na iondokane na ukame na baa la njaa. Kulia ni Katibu Mkuu wa Bakwata aliyemaliza muda wake, Suleiman Lolila na kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Ali.
Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Ali (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Bakwata aliyemaliza muda wake, Suleiman Lolila (kushoto), akitangaza rasmi kustaafu wadhifa huo.
Mkurugenzi wa Daa'wa na Tabligh Bakwata Makao Makuu Sheikh Hassan Said Chizenga (wa pili kushoto), akiongoza dua maalumu katika mkutano huo.
Dua likifanyika.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kazini.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WAISLAM nchini wametakiwa kuomba nchi ipate mvua ili kuondokana na ukame na kuepusha baa la njaa.
Mwito huo umetolewa na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ali wakati ukitolewa kwa niaba yake na Msemaji wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania, Sheikh Khamis Said Mataka wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo.
"Taarifa mbalimbali zinaashiria nchi kukabiliwa na ukame kwa kukosa mvua za msimu zilizotarajiwa kutokana na hali hiyo Mufti anawaomba Masheikh, Maimamu na Waislamu wote kwa ujumla kuleta toba,kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu ili
aijaalie nchi yetu na nchi jirani zetu kupata mvua za kheri zitakazotusaidia kutuepushia ukame na madhara yake ikiwemo baa la njaa" alisema Sheikh Mataka.
Katika hatua nyingine Mufti wa Tanzania amewateua Mwenyekiti wa Halmshauri Kuu Bakwata Taifa, Sheikh Khamis Said Mataka na Mkurugenzi wa Daa'wa na Tabligh Bakwata Makao Makuu Sheikh Hassan Said Chizenga kuwa wasemaji rasmi wa Baraza
Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) uteuzi ambao umeaanza mara moja.
Akizungumzia matumizi ya wadhifa wa Sheikh Mkuu alisema kumekuwa na matumizi yasiyosahihi kwa baadhi ya masheikh wa mikoa na wilaya kujiita masheikh wakuu wa maeneo hayo.
Alisema wadhifa wa Sheikh Mkuu ni Mufti pekee na si vinginevyo na akasisitiza kuwa masheikh wa mikoa na wilaya na mitaa wanakumbushwa kutumia nyadhifa zao kama ilivyoainishwa katika katika ya Bakwata.
Katika mkutano huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi kustaafu kutokana na kutumikia nafasi hiyo kwa muda mrefu na kuwa na umri mkubwa.
Nafasi hiyo hivi sasa itashikiliwa kwa muda na Ustadhi Salm Ahmed.
0 comments:
Post a Comment