Aliekuwa Mhariri wa miaka mingi wa Barmedas Tv ya Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, enzi za uhai wake. Marehemu Sokoro alifariki dunia jumamosi julai 16,2016 majira ya saa mbili usiku katika hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Kifo chake kimesababisha majonzi makubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo waandishi wa habari Jijini Mwanza ambao baadhi yao walipitia mikono ya Sokoro aliefahamika kwa jina maarufu la Mwalimu kutokana na ujuzi wake katika kufundisha nyimbo za Injili na ubobeaji wake katika taaluma ya habari.
Enzi za uhai wake alikuwa Mwalimu wa kwanza wa Kwaya ya AICT Makongoro waliowahi kutamba na wimbo wa Kekundu huku pia akiwa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza katika kituo cha luninga cha Barmedas Tv Cable ambayo awali ilikuwa ikipatikana kwa njia ya cable tu kabla ya hivi karibuni kupatikana katika ving'amuzi mbalimbali.
Mwalimu
Charles Sokoro alizaliwa mwaka 1965 na mauti yamemfika mwaka huu 2016 akiwa na miaka 51. Ratiba ya
Mazishi ni kama ifuatavyo;
1.Siku ya
Jumatatu (18/7/2016 ) saa 10:00 jioni, Mwili wa Marehemu kuwasili kutoka hospitalini
Bugando kuelekea Kanisa La AICT Makongoro
2.Siku ya
Jumanne (19/7/2016) Kanisa La
AICT Makongororo
~Saa 6:00 mchana IBADA ya Kumuaga Mareemu
~Saa 7:30
mchana Safari ya kuelekea Malaloni (Makaburini Kitangiri )
~Saa 8:30
Chakula na baadaye kuhitimisho.
Wanahabari Jijini Mwanza wakieleza namna walivyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake
Wanahabari Mwanza wakieleza namna wavyomfahamu Mwalimu Sokoro enzi za uhai wake.
Ni juzi tu
Tasnia ya Habari ilipata pigo kwa kumpoteza Mwandishi mbobezi kwenye dimba la
michenzo Dada yetu mpendwa Elizabert, na leo tasnia hiyo hiyo imekubwa na msiba
mwingine wa kaka yetu sokoro. HAKIKA msiba wa ndugu yetu Sokoro umetuacha
midomo wazi tunahisi km ni ndoto ya usiku lakini ndio ukweli.
Nani asiye
mjua sokoro kwa ukarimu wake kwa kila mtu ? Kiukweli alikuwa mcheshi asiye na makuu.
Aliipenda
taaluma yake kwa dhati na kila penye kusanyiko la wanahabari naye alimuwepo.
Hakuonyesha
umahiri pekee kwenye tasnia ya habari bali hata kwenye mambo mengine. Nani
asiyejua uwezo wake.kwenye kupiga kinanda?.
Nani
asiyejua umahiri wake kwenye kuenzi utamaduni wa kiafrika?
Kipindi
chake cha ngoma asilia pale Barmedas kilileta uhalisia wa utamaduni wetu. Sokoro
waandishi wenzako tunakulilia umetuacha kwenye wakati mgumu.
Tutakukumbuka
daima tulikuoenda lakini Mungu kakupenda zaidi na alikuita na umeitika leo
haupo nasi. Huu ni
wakati mgumu sana kwa tasnia ya habari. Mungu tupe nguvu tumpumzishe mwenzetu
kwa mikono yetu miwili.
AMINA!
NAEDWIN SOKO;
MRATIBU, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MWANZA (MPC).
0 comments:
Post a Comment