Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha
kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu
Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe akiwa na wakuu wa wilaya wapya wa mkoa huu baada ya kuapishwa.
na matias cana,singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu ala kiapo cha
kuitumikia Wilaya hiyo kwa uadilifu, ubunifu na utu kwa kila mwananchi, Kiapo
hicho kimejidhihirisha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe.
Muda mchache baada ya kiapo hicho mkuu huyo ameshiriki hafla fupi ya
kukaribishwa na Chama Cha Mapinduzi katika ofisi za Chama hicho katikati ya mji
wa Singida.
Mtaturu amesema kuwa ana dhamira ya dhati kuhakikisha wananchi
wanapata maendelea shirikishwa hususani katika kuimarisha sekta ya elimu, afya,
miundombinu na kukemea Rushwa ambayo inarudisha nyuma Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Mtaturu
amesema kuwa ushirikiano baina ya serikali na wananchi wa Ikungi itakuwa turufu
kubwa katika kuhakikisha wilaya inakomaa zaidi kimaendeleo.
"Naenda kusaidiana nao ili kuhakikisha wilaya ina komaa zaidi
kimaendeleo na watu wake kuondokana na uduni wa kipato walionao wananchi,
wananchi wana uwezo wa kufuga na kulima vizuri jambo ambalo linaashiria
kuwaondoa wananchi kwenye wimbi la umasikini".
Amesema Mtaturu Kuhusu wananchi wa Ikungi kukataa kuchangia
shughuli za maendeleo kufuatia pingamizi lilichagizwa na mbunge wa jimbo hilo
Mtaturu amesema kuwa Utaratibu wa kuchangia maendeleo upo katika dunia nzima
nchi mbalimbali za ulaya na kwingineko zimekuwa zikichangia shughuli za
maendeleo nchini Tanzania kwa ajili ya wananchi masikini lakini wananchi
tunaosaididiwa kuondokana na wimbi hilo tunapaswa pia kuchangia shughuli za
maendeleo.
Amesema wananchi wa Ikungi hawapaswi kutumika kisiasa huu ni muda
wa kufanya kazi ili tusikubali maendeleo yetu kurudishwa nyuma na wanasiasa au
watu wachache wenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko maendeleo.
"Huko nyuma kulikuwa na watu wanajitolea kufanya shughuli za
mikono kwa kuchangia mawe, tofali au mchanga hivyo mchango huo ulikuwa muhimu
zaidi japo asilimia kubwa ya watanzania wanadhani mchango ni pesa pekee"
Ameongeza Mtaturu Katika halfa hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng
Methew Mtigumwe amemuapisha mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bw Jackson Jonas Masaka,
Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw Elius Chollo John Tarimo, na Mkuu wa Wilaya ya
Iramba Bw Emmanuely Jumanne Luhahula.
Aidha mkuu wa Wilaya ya Manyoni hakuapishwa kutokana na kuwa nje ya
nchi kikazi tangu alipoteuliwa. Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Singida
amewataka wakuu wote wa Wilaya walioapishwa kuhakikisha wanasimamia vizuri
katiba na sheriaza nchi sawia na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka
2015-2020.
"Nawaomba mkasimamie uadiligu, uaminifu, kufanya kazi kwa
weledi na kuhakikisha wanapinga rushwa kwa nguvu zote, lakini nataka
niwakumbushe hadi kufikia jana tarehe 30 Hakuna Halmasahauri ambayo imefanikiwa
kukusanya mapato na kufikia asilimia 80 hivyo nendeni mkahakikishe watu
wanalipa kodi stahiki ili kukuza pato la kila wilaya na kunusuru Halmashauri
zetu kufutwa"
Amesema Mtigumwe Mkuu huyo Amewapongeza wadau mbalimbali katika
Wilaya hiyo kwa kujitolea kuchangia madawati elfu arobaini mpaka sasa na
kuubakisha mkoa huo ukiwa na upungufu wa madawati kati ya 1500 katika mkoa huo.
Imetolewa na Ofisi ya muda ya Mkuu wa Wilaya (Ikungi) Julai 1, 2016
0 comments:
Post a Comment