Mkuu
wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za mkoa huo na hii ni picha ya pamoja mara baada ya kiapo
hapa wakuu wa wilaya wakiendelea kula kiapo
Na Mathias Canal, Lindi
Mkuu
wa mkoa wa Lindi Mh Godfrey Zambi amewaapisha wakuu wa wilaya tano za mkoa huo
huku kila mmoja akiahidi utendaji uliotukuka katika kukabiliana na changamoto
zinazowakabili wananchi husika.
Hafla hiyo imefanyika katika
ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo mkuu huyo amewasisitiza viongozi hao
kuhakikisha suala la upatikanaji wa madawati linazaa taswira chanya kwa kuhakikisha
madawati yanatimia kama ambavyo agizo la rais lilitolewa hivi karibuni la
kuhakikisha wanafunzi wanaketi katika madawati pasipo kuwa na mbanano.
Zambi amewataka wakuu hao wa
wilaya kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ccm ili
kukamilisha ahadi zilizoahidiwa na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt
John Pombe Magufuli wakati wa kampeni zilizoanza Agosti na kumalizika Octoba
mawaka jana.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea
Rukia Akhibu Muwango amesema atasimamia na kudhibiti suala la watumishi hewa na
kulifanya kuwa zoezi endelevu ili wilaya hiyo iweze kusonga mbele kwa muktadha
wa mafanikio ya ajira kwa vijana na watu wenye elimu lakini nafasi zao
zilishikiliwa na watu wasiokuwa halali (watumishi hewa).
Mkuu huyo ameahidi kukutana na
makundi mbalimbali Wilayani humo ili kupata picha halisi ya namna hatua
zimefikiwa za kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa ufanisi mkubwa namafanikio
zaidi kwa maana ya kufauli na kufikia mpaka chuo kikuu.
Muwango amesema amekuwa
mtumishi erikali kwa muda mrefu hivyo kwa kiasi kikubwa anazifahamu changamoto
za wananchi hususani matatiuzo ya upatikanaji wa maji, afya, elimu na
miundombinu.
Wilaya ya lindi ni moja kati
ya wilaya zilizopo mkoani lindi zinazojihusisha zaidi na kilimo kuliko masomo
Muwango amesema kuwa atahakikisha anaanzisha kamati ya maendeleo ya Elimu ya
wilaya ambapo Kamati hiyo itakuwa na wataalam na watu maarufu wa Wilaya ya
Nachingwea na kamati hiyo itajiwekea mikakati ya uboreshaji Elimu, hivyo mkuu
wa Wilaya atatashirikiana na wataalamu wa Halmashauri kuona mikakati hiyo
inafanikiwa.
Pamoja na hayo mkuu huyo pia
amesema kuwa anataraji kuanzishaTuzo ya Mkuu wa wilaya kwa wanafunzi
watakaofanya vizuri kila kata ambapo Vigezo watakubaliana na kamati hiyo.
Wakuu wa Wilaya wengine
walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph
Joseph Mkirikiti, Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Vicent Chiwamba, Mkuu wa
Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Emil
Ngumbiagai
0 comments:
Post a Comment