Saturday, July 16, 2016

DC MTATURU AKABIDHI OFISI YA CCM MKOA WA MWANZA

Dc Mtaturu (kushoto) akikabidhi nyaraka za ofisi ya ccm mkoa wa mwanza kwa katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda

Dc Mtaturu akizungumza na baadhi ya watendaji wa ofisi ya ccm ya mkoa wa mwanza muda mchache mara baada ya kukabidhi ofisi hiyo



Na Mathias Canal, Mwanza

Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza ambaye sasa ni mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Miraji Jumanne Mtaturu amekabidhi rasmi ofisi ya CCM Mkoani Mwanza.

Dc Mtaturu amemkabidhi ofisi hiyo kwa Katibu wa Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda ambaye sasa anakaimu nafasi ya ukatibu wa Mkoa huo.

Dc Mtaturu amehudumu katika Mkoa huo kwa kipindi cha miezi 16 (mwaka mmoja na miezi minne) tangu alipowasili Mkoani hapo akitokea Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

DC MTATURU NA UTENDAJI

Katika kipindi hicho Mtaturu ameonyesha siasa ya kisayansi baada ya kutumia miezi saba (7) kuhakikisha majimbo mawili yaliyokuwa chini ya CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanarejea Chama Cha Mapinduzi.

Majimbo hayo ni pamoja na Jimbo la Nyamagana ambalo kwa kipindi cha miaka mitano limeongozwa na Ezekiel Wenje (CHADEMA) na sasa linaongozwa na Stanslaus Mabula kupitia CCM.

Pia Jimbo la Ilemela lililokuwa linaongozwa na Highness Kiwia chini ya CHADEMA sasa linaongozwa na Anjelina Mabula Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi.

Lakini pia Dc Mtaturu amechangia kurejesha Halmashauri tatu zilizokuwa chini ya CHADEMA ambazo ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Nyamagana, na Ukerewe hivyo kufanya Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza kuwa chini ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Kabla ya kuwasili Mkoani Mwanza Mtaturu alitokea Katika Wilaya ya Mufindi ambapo tarehe 14 Disemba 2014 alikipaisha chama hicho Kitaifa baada ya ushindi wa asilimia 99.5% kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa.

DC MTATURU BAADA YA KUAPISHWA

Baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa  Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Mkoa huo, Mtaturu alianza utendaji kwa kuitembelea ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida kwa ajili ya kuwasalimu na kuzungumza na watendaji wa Chama Hicho.

Baadaye alikabidhiwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Gishuri Charles ambaye sasa amestafu.

Hivyo alimshukuru Rais kwa kumpa majukumu mapya pasina kujali ni mahali gani anapelekwa.

Miraji Mtaturu ni Katibu pekee wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya dhahiri jambo hili  limeinyesha ufanisi wake katika utendaji.

Mtaturu alisema Wilaya ya Ikungi inaingia katika muktadha wa kufahamika kupitia utendaji na uwajibikaji kwa kila Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More