mbunge wa jimbo la kiloloVenance Mwamoto akikabidhi mabati 57 yenye zaidi ya Mil.moja kwa uongozi wa kata ya nyanzwa
Na fredy mgunda,Kilolo
WANANCHI
wa kata ya Nyanzwa iliyopo katika kijiji
cha Nyanzwa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa wamemuomba mbunge wa Jimbo hilo
Venance Mwamoto kuwasaidia kumalizia ujenzi wa Nyumba za walimu zilizopo kwenye
kata hiyo ili kuondokana na changamoto ya walimu kuishi mbali na eneo la shule.
Kilio
hicho kimetolewa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya kata hiyo
ambapo wananchi hao waliamua kujitolea nguvu kazi zao wenyewe kufyatua tofali na
kuanza kujenga nyumba za walimu lakini walikwama kumalizia ujenzi huo kutokana na kukosekana
kwa rasiilimali fedha ambazo wangezitumia kununulia mabati.
Akizungumza
mkazi wa kijiji hicho John Mwandi alisema kuwa pamoja na jitihada za wananchi
za kufyatua tofali lengo lao ni kuhakikisha walimu wanaishi karibu za shule zao
ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wanafunzi.
“Walimu
wa shule nyingi za kata hii wanaishi nje ya eneo la shule hivyo kwa kuliona
hilo wananchi wameamua kujitolea nguvu kazi zao kwa ajili ya kujenga nyumba za
walimu ili waweze kutoa huduma ili bora kwa wanafunzi.”alisema Mwandi
Naye
Kauli Msisi alisema walimu wakiishi
jirani na eneo la shule litawasaidia kutoa elimu hiyo kwa ufanisi na wanafunzi
wataweza kupata huduma iliyo bora na baadaye kuongeza ufaulu wao.
“Walimu wa eneo hili walikuwa wakiishi mbali
sana na shule zetu,sasa tunaona kukamilika kwa ujenzi huu walimu watakuwa
hawatoki mbali,wanafunzi watapata huduma iliyobora,kiwango cha ufaulu
kitaongezeka na hatimaye tutapata wataalamu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kizazi
cha baadaye.”alisema Msisi
Hata
hivyo baada ya kuona changamoto hiyo mbunge wa jimbo hilo Venance Mwamoto
alikabidhi mabati 57 yenye zaidi ya Mil.moja kwa uongozi wa kata ili waweze
kumalizia ujenzi kwa haraka.
“Nimetoa
mabati 40 kwa ajili ya kuezeka nyumba za walimu wa kijiji cha nyanzwa,17 kwa
ajili ya kijiji cha Igunda na nimeona ni vyema nikaunga mkono kwa sababu
wananchi wameshajitolea na kawaida ni kwamba serikali ndiyo inatakiwa iunge
mkono kwa maana ya halmashauri
wanapofikia ngazi ya kuezeka serikali ndiyo inatakiwa kumalizia lakini mimi
nimeona wanachelewa kupeleka hizo bati na hivyo kuwakatisha tama.”alisema
Mwamoto
Kwa
upande wake ofisa mtendaji wa kata hiyo Kimwaga Edcoss alimshukuru mbunge huyo
na kuongeza kuwa mbunge alijitokeza kwenye mkutano na ndipo wananchi waliomba
kusaidiwa na haikuwa ahadi yake.
0 comments:
Post a Comment