Tuesday, July 26, 2016

KAMPUNI YA MGODI WA GEITA GOLD MINING (GGM) YAFANIKISHA ZOEZI LA KUKUSANYA PESA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

 
Mkuu wa wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiongozana na kundi la wapanda mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining (GGM) waliopanda kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.

 
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM)  ,Simon Shayo akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya kundi la wapanda mlima wakiwemo wafanyakazi wa mgodi huo waliopanda kwa leongo la kuchangisha fedha  za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.
   
Kiongozi wa kundi la wafanyakazi wa kampuuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining ,Kelvin Yasiwa akizungumza kwa niaba ya wenzake mara baada ya kuwasili wakitokea katika kilele cha Uhuru ,Mlima  Kilimanjaro.
 
Balozi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto akizungumza mara baada ya kurejea salama kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
 
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Lucy Mashauri(15)baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
  
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba akikabidhi cheti kwa mtoto Jacob Musa (16) baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
 
Balozi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Msanii Mrisho Mpoto akifurahia baada ya kukabidhiwa cheti kwa kufanikiwa kufika katika moja ya vilele vya Mlima Kilimanjaro,kilele cha Stela .
 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba akikabidhi vyeti kwa washiriki wengine wa changamoto hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ukimwi.
 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba aliyekua mgeni rasmi katika hafla hiyo Kipi Warioba akizungumza mara baada ya kuwapokea wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining.
 
Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia taasisi mbalimbali zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa hafla ya mapokezi yao,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kipi Warioba.
 
Watoto Yatima ambao ndio pekee walioshiriki katika changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kufika Kileleni wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba pamoja na viongozi wengine akiwemo Makamu wa Raisi wa kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mining,(GGM).
 
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mining (GGM) Simon Shayo akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mapokezi ya washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More