Rais wa klub za wandishi wa habari nchini DEOGRATIUS NSOKOLO akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kulewa kwa hukumu ya kesi ya mwanahabari daudi mwangosi
Mke wa marehemu Daudi Mwangosi, Bi Itika akizungumza na waandishi wa habari
Mahakama kuu kanda ya iringa
leo imemuhukumu kwenda jela Miaka 15 askari polisi PASIFICUS SIMONI aliyehusika
na kifo cha mwanahabari wa chanel ten Daudi Mwangosi.
hukumu hiyo imetolewa leo katika mahakama mkuu kanda ya iringa
hata hivyo Mke wa marehemu Daudi Mwangosi, Bi Itika
amesema kuwa anawashukuru waandishi wa habari kwa umoja waliouonesha katika
kipindi chote cha kesi.
Naye Rais wa klabu za wandishi wa habari nchini DEOGRATIUS
NSOKOLO amesema kuwa amefurahishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama.
Awali wakili ambaye alikuwa
anamtetea mtuhumiwa RWEZAULA KAIJAGE
amebainisha kuwa ataangalia kasoro zilizotokea wakati wa hukumu ili akate rufaa
ya hukumu hiyo.
Mwandishi
wa Habari, Daudi Mwangosi wa kituo cha Channel Ten aliuawa Septemba 2, 2012 katika Kijiji
cha Nyololo Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa
Iringa alipokuwa katika majukumu ya
kikazi baada ya kutokea ghasia zilizozuka kati ya wafuasi wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na polisi katika mkutano wa chama hicho.
0 comments:
Post a Comment