Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anayetaraji kuwasili Mkoani humo tarehe 29 mwezi huu.
Na
Mathias Canal, Singida
Kutochangia
maendeleo yatajwa kuwa Njia mojawapo ya kukiuka haki za binadamu, kwani
wananchi wasipopata huduma bora za kijamii wanailaumu serikali.
Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Miraji Jumanne Mtaturu ameyasema hayo wakati
akitoa taarifa ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli anayetaraji kuwasili Mkoani humo tarehe 29 mwezi huu.
Rais
Magufuli atafanya ziara ya katika Wilaya hiyo Mkoani humo ambapo kabla ya
kuwasili Wilayani Ikungi atazuru Wilayani Manyoni akitokea Mkoani Dodoma.
Rais
Magufuli yupo katika Chereko ya kumbukumbu nzuri ya ushindi wa Asilimia mia
moja aliyoipata mwishoni mwa Juma wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa na wajumbe wote wa chama hicho.
Hii ni
ziara yake ya awali kuzuru Mkoani Singida tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa
Awamu ya tano Octoba mwaka Jana na tangu awe Kiongozi mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi
0 comments:
Post a Comment