Katazo hilo limetolewa leo (Ijumaa, Julai 8, 2016) ambapo Majaliwa amefafanua kwamba usitishaji huo unalenga kutathmini taratibu, kanuni na vigezo sahihi vinavyotakiwa kutumika katika kugawa malighafi kutoka kwenye mashamba hayo.
Ameongeza kuwa wadau wote wa viwanda vinavyojikita katika malighafi ya misitu na hususani wamiliki wa viwanda vya kupasua mbao wanashauriwa kuwa watulivu wakati utaratibu huu ukifanyiwa mapitio na umma utatangaziwa rasmi pindi uboreshaji huo utakapokamilika.
Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inamiliki mashamba ya miti ya kupandwa 18.
Kati ya hayo uvunaji umekuwa ukifanyika katika mashamba nane ambayo ni kama ifuatavyo,
1.Sao Hill (Mufindi),
2.Buhindi (Sengerema),
3.Meru/Usa (Arumeru),
4.West Kilimanjaro (Hai),
5.Shume (Lushoto),
6.North Kilimanjaro (Rombo),
7.Kiwira (Rungwe) na
8.Kawetire (Mbeya Vijijini)
0 comments:
Post a Comment