Thursday, August 31, 2017

MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI BESENI 100 KWA KINAMAMA WAJAWAZITO NA WALIOJIFUNGUA KATIKA HOSPITAL YA MJI WA MAFINGA

 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwapa akina mama waliojifungua mabeseni kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa kinamama wa jimbo la mufindi na wananchi wote wanotumie hospitali ya mafinga mjini lakini mabeseni hayo yametolewa kwa msaada wa ubalozi wa kuwait hapa nchini Tanzania.
 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na mmoja wa kinamama alifanikiwa kupewa msaada wa beseni


Na Fredy Mgunda,Mafinga.

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mabeseni mia moja kwa akina mama waliopata watoto kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya Mafinga.

Mabeseni hayo yalikabidhiwa kwa kina mama waliojifungua na ambao wanatarajia kujifungua hivi karibuni hospitalini hapo.

Msaada huo wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni nne, umetolewa na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini mapema wiki iliyopita.

`ndugu zangu zawadi hii tumepewa na Balozi wa Kuwait hapa Nchini kwa ajili yenu kina mama kama sehemu ya mwanzo wa ushirikiano kati ya Mafinga na Ubalozi wa Kuwait' alisema Chumi.

Akifafanua, alisema kuwa msaada huo ni uthibitisho wa upendo alionao Balozi wa Kuwait hapa nchini kwa watu wa Mafinga.

`Mheshimiwa Balozi Jasem Al- Najem hajawai kufika Mafinga lakini kwa upendo mkubwa akasema, naomba hiki kidogo uwafikushie kina mama wa Mafinga' alisema Chumi na kuongeza kuwa ushirikiano kwenye jambo dogo ndio mwanzo wa ushirikiano wa mambo mengine makubwa.

Akishukuru wakati wa kukabidhi msaada huo wa mabeseni, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga alipongeza ushirikiano wa Mbunge na wadau mbali mbali na kuwasihi watendaji kuendelea kufanya kazi kwa kujituma.

`sisi halmashauri tuko bega kwa bega na mbunge, na ninyi watumishi kwa pamoja tuendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa kujituma' alisisitiza Makoga.

Wakati akikabidhi msaada huo wiki moja iliyopita kwenye ofisi za Ubalozi wa Kuwait Masaki Jijini Dar es Salaam, Balozi Jasem Al-Najem alisema kuwa lengo la Ubalozi ni kugawa jumla ya mabeseni elfu moja kwa ajili ya mama na mtoto.

`katika awamu ya kwanza ya kutoa msaada huu wa mabeseni haya ya mama mtoto kits, tumeona tuwakumbuke na kina mama wa Mafinga japo kwa mabeseni mia moja'

Ubalozi wa Kuwait umekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii na kibinadamu ambapo mpaka sasa wameshachimba visima arobaini kwenye shule mbali mbali za Mkoa wa Dar na Pwani.

Aidha Ubalozi umeshatoa msaada wa vifaa vya theatre katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na pia kuendesha zoezi la kuchangia damu miezi sita iliyopita.

ASKARI WANAWAKE WA JKT MGULANI WAFANYA USAFI WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE.

 Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama baada ya kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo kuhusu shughuli ya usafi  waliofanya katika Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini.

SABABU YA EID-AL-ADHA KUITWA 'SIKUKUU YA KUCHINJA'

Na Jumia Travel Tanzania

Eid al-Adha ni miongoni mwa sikukuu kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu ukiachana na Eid- al-Fitr inayosherehekewa kila mwaka duniani kote. Kwa mwaka huu sikukuu hii inatarajiwa kusherehekewa siku ya Ijumaa ya Septemba mosi ambapo kwa waumini wa dini hiyo ni kipindi cha kujitolea, kuonyesha ukarimu kwa marafiki, familia na watu wenye uhitaji.

Kama zilivyo sikukuu nyingine kuna baadhi ya watu huwa hawajui ni kwa nini huwa zinaseherehekewa namna zinavyosherehekewa. Jumia Travel kupitia makala haya imekukusanyia mambo ya msingi kuhusu maana ya sikukuu hii na namna ya kusherehekea.

MAMIA WAMIMINIKA KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA (WCF) IKIWA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI JENISTA MHAGAMA

Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na kulipa michango leo Agosti 31, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.
Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.
“Kwakweli tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema Bw. Luvena
K-VIS Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza leo Agosti 31, 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF  kujisajili na kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.
 Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF, leo Agosti 31, 2017.

 Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe, (kulia), akimkabidhi cheti cha usajili Bw.Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refregerator ya jijini Dar es Salaam.
 Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kushoto), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
 Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, akimsikiliza Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, (kushoto), akimuhudumia Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe,(kushoto), akimuhudumia Bw. Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refrigeration, ya jijini Dar es Salaam.
 Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwasikiliza waajiri waliofika leo Agosti 31, 2017 ili kupatiwa huduma ya usajili na uwasilishaji michango katika Mfuko huo.
 Maafisa wa WCF (kulia), wakimsikiliza Mama huyu mwajiri aliyefika kupatiwa huduma.



JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI

 Mkuu wa   Kikosi  cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey Kitani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu askari wa kikosi hicho kujitolea damu na kufanya usafi  katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote. 

MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 30 YA DROO YA JUMAPILI YA JACKPOT YA TATU MZUKA AKABIDHIWA FEDHA ZAKE

 Balozi wa Mchezo wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kushoto), akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 30 mshindi wa droo ya Jumapili ya Jackpot ya Tatu Mzuka, Tausi Mashombo jijini Dar es Salaam jana, aliyojishindia kutoka katika mchezo wa Tatu Mzuka ambao umejizolea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea Jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.

Monday, August 28, 2017

YALIYOJIRI KWENYE UZINDUZI WA MFUKO WA ELIMU WILAYANI IKUNGI

BMG Habari, Pamoja Daima!
Jumamosi iliyopita, Agost 19,2017 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ilizindua rasmi “Mfuko wa Elimu Ikungi” ulioanzishwa wilayani humo kwa lengo la kusaidia utatuzi wa kero za elimu ikiwemo uhaba wa maabara, madarasa, vyoo pamoja na nyumba za waalimu.

Katika uzinduzi huo, pia zilifanyika shughuli kadhaa ikiwemo uzinduzi wa ligi ya soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” yenye lengo la kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuchangia Mfuko wa Elimu Ikungi, uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imeazimia kufyatua matofali elfu kumi.

Karibu kwa dakika chache kutazama yaliyojiri kwenye uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala mkoani humo Dkt.Angeline Lutambi huku mwenyeji wake akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na mlezi wa Mfuko wa Elimu Ikungi, Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu. Tazama video hapo chini.

HIZI NDIO MECHI KUBWA ZA WATANI WA JADI BARANI AFRIKA

Na Jumia Travel Tanzania

Miongoni mwa matukio yanayosisimua zaidi kwenye mchezo wa soka ni mipambano ya watani wa jadi. Katika nchi nyingi barani Afrika ukiwauliza kwa harakaharaka mashabiki wengi wa soka ni mechi zipi huwa wanazisubiria sana utawasikia wanakutajia michezo kama vile Real Madrid na Barcelona, Manchester United na Manchester City, Inter Milan na AC Milan, Liverpool na Manchester United, Chelsea na Arsenal au Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Kutokana na umaarufu wa soka la nchi za Ulaya imekuwa ni rahisi kwa mechi zao kufuatiliwa kwa urahisi ukilinganisha na huku Afrika. Lakini hiyo haimaanishi kwamba bara la Afrika nalo halina michezo ya namna hiyo ambayo ikiwa inakaribia homa miongoni mwa mashabiki huwa juu kuliko kawaida.

Ukweli ni kwamba mechi za namna ya mifano iliyotajwa hapo juu zipo na zimekuwa zikichezwa kwa miaka mingi tu.kw au pengine inawezekana ukawa unazisikia tu lakini haujui umuhimu uliopo pindi zinapokutana. Jumia Travel imekukusanyia orodha ya mechi kali za mpira wa miguu ambazo timu zikikutana kunakuwa ni patashika, presha na vimbwanga vya kila aina.  
Orlando Pirates dhidi ya Kaizer Chiefs (Afrika ya Kusini) -  Soweto derby. Kama yalivyo mapambano mengine ya watani wa jadi, mchezo huu ni zaidi ya mpira wa miguu kwani ni uhasama hasa. Mchezo ambao umpewa jina la ‘Soweto derby’ huzikutanisha timu za Orlando Pirates na Kaizer Chiefs mara kadhaa ndani ya mwaka katika jiji la Johannesburg. Uhasama wa timu hizi mbili unakuja kutokana na kuwa zote zinatokea sehemu moja. Kaizer Chiefs ilianzishwa na aliyekuwa mmojawapo wa wachezaji wa Orlando Pirates, Kaizer Motaung.
   
Wydad Casablanca dhidi ya Raja Casablanca (Morocco) - Casablanca derby. Hakuna ubishi kwamba nchi za Afrika ya Kaskazini zimebarikiwa kuwa na vipaji lukuki vya mpira wa miguu ambapo mpaka hivi sasa vinaliwakilisha vema bara hili sehemu mbalimbali duniani. Katika mji wa Casablanca kwenye nyakati tofauti za mwaka kunakuwa na mchezo mkali ambao huzikutanisha timu za Wydad Casablanca na Raja Casablanca ambao pia hujulikana kama ‘Casablanca derby’. Mchezo wa watani wa jadi hawa mara nyingi hupigwa katika uwanja wa Mohammed V Stadium ambapo licha ya kuonyesha nani ni fundi wa kusakata kandanda lakini pia ni juu ya nani ni bora katika anga za kuliwakilisha jiji na nchi kwa ujumla.  
Al Ahly dhidi ya Zamalek (Misri) - Cairo derby. Linapokuja suala la mchezo wa soka basi mashabiki wa timu za Al Ahly dhidi ya Zamalek ni nambari moja kwa kuzishangilia timu zao. Mojawapo ya mitanange mikali kabisa ya soka ambayo hutawaliwa na presha na msisimko mkubwa ni pindi timu hizi zinapokutana ambao pia umepewa jina la ‘Cairo derby.’ Inapofikia siku ya mechi hii hali ya hewa ya jiji zima la Cairo hubadilika kutokana na homa ya mchezo huo. Mbali na kuwa ushindani huwa ni wa kisoka lakini kwa upande mwingine ni wa kisiasa zaidi.
    
Club Africain dhidi ya Espérance Sportive de Tunis (Tunisia) - Tunis derby. Katika jiji la Tunis kwenye ratiba tofauti za mchezo wa soka huzikutanisha timu mbili zinazowakilisha jiji hilo za Club Africain na Espérance Sportive de Tunis. Ushindani mkubwa katika mchezo huu umekuwa na historia tofauti ambapo hapo awali ulihusishwa na matabaka kama vile ilisemekana timu ya Espérance ilikuwa ikimilikiwa na serikali na tabaka la juu la watu wa mji wa Tunisia huku Club Africain ikimilikiwa na watu maarufu wa matabaka tofauti. Lakini hiyo imebadilika na ikawezekana kutokuwa na ukweli ndani yake kwani unaweza kukuta watu wa familia moja wanashabikia hizo kwa wakati mmoja.
  
Simba S.C. dhidi ya Young Africans S.C. (Tanzania) - Dar es Salaam au Kariakoo derby. Tukiachana na umaarufu wa mchezo wa mpira wa miguu katika nchi za Afrika ya Kuskazini pia katika kalenda za soka barani Afrika huwa inapigwa mechi kali sana kwenye ukanda wa Afrika ya Mashariki baina ya timu za Simba na Young Africans au Yanga ambazo zote hutokea jiji la Dar es Salaam. Mbali na timu hizo kukutana katika michezo kadhaa ya ligi kuu pia kuna michezo mingine ni pamoja na ngao ya jamii, kombe la shirikisho la mpira wa miguu, kombe la mapinduzi ne mingineyo. 
Kama ni mgeni kwenye jiji la Dar es Salaam basi ikifika siku ya mchezo huo utajua homa ya watani wa jadi wa timu hizo mtaani kwani utawatambua mashabiki wa timu hizo kwa mbwembwe, tambo na shamrashamra kwa kuvalia jezi za rangi nyekundu na nyeupe (Simba) huku Yanga ni (kijani na njano). 

Uhasama wa timu hizo ambazo zinatokea katika eneo moja la Kariakoo si tu kuhusu mpira bali ni heshima juu ya nani ni mfalme na bingwa wa kusakata kandanda nchini Tanzania na kuliwakilisha taifa kwenye anga za kimataifa. Mchezo baina ya timu hizi mbili huwa unapigwa kwenye uwanja wa taifa ambao unao uwezo wa kukusanya mashabiki takribani 60,000.
USM Alger dhidi ya MC Alger (Aljeria). Mchezo huu wa watani wa jadi kama ilivyo mingine huzitenganisha familia na majirani na wakati mwingine huisha kwa ugomvi na vurugu baina ya mashabiki wa pande mbili. Uhasama baina timu ya hizi mbili unahusishwa kwa kiasi kikubwa na historia ya nchi hiyo wakati wa harakati za kudai uhuru. Katika sehemu mbalimbali za nchi ya Aljeria mchezo baina ya timu hizi mbili hubakia kuwa ni tukio la kitaifa kutokana na kuzungumziwa na kupewa nafasi kubwa kwenye vyomo tofauti vya habari.

TP Mazembe dhidi ya FC Lupopo (R.D Congo). Jina la TP Mazembe sio geni miongoni mwa mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania kutokana na wachezaji wa hapa nyumbani Mbwana Samata ambaye alifanikiwa kujitwalia taji la mchezo bora wa ndani wa Afrika na Thomas Ulimwengu kuchezea pale. Katika jiji la Lubumbushi kila mwaka kunakuwa na tukio kubwa la mchezo wa soka ambalo huwakutanisha watani wa jadi kati ya TP Mazembe na FC Lupopo.

Gor Mahia dhidi ya AFC Leopards (Kenya) - Nairobi au Mashemeji derby. Shamrashamra na tambo za mashabiki wa mchezo wa mpira miguu katika mitaa mbalimbali ya jiji la Nairobi huonekana wazi pindi timu za Gor Mahia na AFC Leopards zinapokutana. Mchezo huu ambao una historia ya muda mrefu kwenye soka nchini Kenya huchukuliwa kama ni siku kubwa ambapo mashabiki licha ya kuonyesha uhasama mkubwa lakini ni sherehe, likizo na huchukuliwa kama siku maalum.
Asec Mimosas dhidi ya Africa Sport Abidjan (Ivory Coast) - Abidjan derby. Miongoni mwa tukio baya kutokea pindi timu hizi mahasimu zinazotokea katika jiji la Abidjan nchini Ivory Coast ni mwaka 2001 ambapo vurugu zilitokea ambapo mtu mmoja alifariki huku 30 wakijeruhiwa. Timu ya Asec Mimosas inajivunia kwa kutoa vipaji vikubwa kabisa vya soka nchini humo na duniani wakiwemo Kolo Toure, Didier Drogba na Gervinho.

Al-Merreikh dhidi ya Al-Hilal (Sudani). Uhasama wa timu hizi mbili zinazotokea kwenye jiji la Omdurman nchini Sudan ambapo mnamo mwaka 1934 timu ya Al-Merreikh iliifunga Al-Hilal kwa mabao 2 bila ya majibu ambapo kulikuwa hakuna uwanja enzi hizo. Uhasama baina ya timu hizo mbili pia huchochewa kwa kiasi kikubwa na idadi ya wachezaji kila timu iliyo nayo kwenye kikosi cha timu ya taifa.      
Ipo michezo mingine mingi tu ya watani wa jadi kwenye soka lakini hiyo ndiyo mikubwa ambayo inasubiriwa na kuangaliwa zaidi. Jumia Travel inaamini kwamba sasa utakuwa umeijua na utaanza kuifuatilia kwani kuna burudani nyingi ulikuwa ukiikosa kwa kutoifuatilia. Mechi hizo kutokupewa nafasi kubwa na vyombo vya habari tofauti barani Afrika kama ilivyo kwa ile ya Ulaya haimaanishi kwamba haina ushindani mkubwa.

WATAALAMU WAAINISHA UMUHIMU WA KUIPITIA UPYA SERA YA MAENDELEO YA VIWANDA ENDELEVU (SIDP 1996-2020) IENDANE NA WAKATI

WATAALAMU na wanazuoni wamekubaliana haja ya kupitia mpango wa maendeleo endelevu wa viwanda, SIDP (1996-2020), ili kwenda na wakati kwa kubadili kilimo na kuiweka nchi katika njia bora ya kufikia uchumi wa viwanda. Kauli hiyo imetamkwa kwa namna tofauti na wataalamu hao ambao wamekutana jijini hapa kuangalia uhusiano uliopo kati ya viwanda, mabadiliko ya tabia nchi na kilimo; na ni namna gani sera ya viwanda inaweza kupitiwa upya kuakisi mahusiano haya. Warsha hiyo iliyoandaliwa na ESRF na CUTS International imelenga katika kuelezea umuhimu wa kuangalia mahusiano ya sera ya maendeleo ya viwanda na mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara. Wakijadili mada mbalimbali zilizowasilishwa katika semina hiyo iliyofanyika ESRF, wataalam hao walitambua umuhimu wa pekee wa kupitia upya sera hiyo ili iweze kuonesha muunganiko fasaha uliopo kati ya viwanda, kilimo na biashara; na hatua/mikakati ipi iwepo kukinga adhma hii ya viwanda dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi. Wamesema kwamba kwa kuunganisha sera ya maendeleo endelevu ya viwanda na uchakataji wa bidhaa za kilimo na kilimo chenyewe kunaleta mwanya wa kuweka msingi imara katika mchakato wa maendeleo na hasa viwanda. Pia, kwa kuwa na sera madhubuti, nchi itaweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika sekta ya Viwanda, hususani viwanda vinavyotegemea maligafi za sekta ya kilimo. Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption] Katika mkutano huo ilikubalika haja ya kuwa na mikakati ya utetezi kwa kuangalia tafiti zitakazofanywa juu ya kinachojiri katika maendeleo kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara. Zaidi ya yote, pia wadau waliona kuna haja kubwa ya kuwa na tafiti itayoweza kuonesha ni kwa kiasi gani sera ya SIDP (1996-2020) imeweza kuchangia katika ukuaji wa viwanda Tanzania, na changamato zipi imekumbana nazo ambazo zinapaswa kutatuliwa na kuanishwa wakati wa mapitio ya sera hii. Akiwasilisha hoja yake ndugu Solomon Baregu, Mtafiti wa ESRF na Meneja wa Mradi wa PACT EAC 2, amesema kwa kuangalia hali halisi ya sasa ipo haja kwa wataalamu kutambua changamoto zinazojitokeza katika maendeleo endelevu ya viwanda na kukiangalia kilimo kama msingi wa uimarishaji wa viwanda. Aidha alisema kwamba kwa kuangalia hali ya sasa ipo haja kubwa ya kubadili kilimo cha Tanzania ili kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha viwanda kwa kuvipatia mali ghafi ya kutosha na yenye ubora. Alisema ni vyema kuelewa uhusiano uliopo katika sera za maendeleo ya viwanda na kilimo ili kuwa na mpango mahsusi wa utetezi kwa lengo la kuimarisha viwanda. Katika mkutano huo washiriki pia walipitia mambo mbalimbali na hatua zinazochukuliwa kupitia sera ya mpango wa maendeleo wa viwanda unaomalizika 2020. Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Ushirikishaji Kikanda kutioka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bi. Sekela Mwaisela akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption] Miongoni mwa mambo yaliyojitokeza kwenye mazungumzo ya tafiti ni umuhimu wa kuoanisha sera mbalimbali katika kilimo na viwanda kuzihuisha na kuzipa mwelekeo wenye maana kama chachu katika kuimarisha uchumi wa viwanda. Walisema ipo haja ya kuangalia sera hizo ili ziwe msaada katika kuimarisha kilimo na kutoa ushindani kwa viwanda vinavyotegemea bidhaa za kilimo ili kujiimarisha. Aidha katika mazungumzo kwenye mkutano huo imeelezwa kuwa ingawa serikali kupitia wizara zake mbalimbali na Ofisi ya Makamu wa Rais wamechukua hatua kadhaa kuwa na matokeo bora katika utetezi wa bidhaa za viwanda zinazotokana na kilimo, kukosekana kwa uangalizi na utekelezaji wa pamoja kumeleta shida kwa wananchi. Sera ya sasa ya maendeleo endelevu ya viwanda (SIDP) imetengenezwa mwaka 1996 na itaisha 2020 lakini bado ipo haja ya kuweka mahusiano katika utekelezaji wa mpango huo wa maendeleo, kwani kwa mazingira ya sasa hakuna mahusiano na kuna vikumbo katika sera mbalimbali. Wamesema kwamba sera hiyo haitoi mwanya wala mahusiano kati ya viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula. Mtafiti wa ESRF na Meneja wa Mradi wa PACT EAC 2, Solomon Baregu akiwasilisha namna bora ya kufanya utafiti wenye lengo la kuoanisha mpango wa maendeleo endelevu ya viwanda na mabadiliko ya tabia nchi na kilimo wakati wa mkutano huo wa kuzungumzia mradi wa PACT-EAC2 uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption] Aidha walisema kwamba mpango wa pili wa maendeleo (2016/17-2020/21) unaonesha haja ya kuweka Tanzania katika njia ya viwanda kwa kuijengea nchi uwezo wa kuzalisha katika kilimo na pia katika ufugaji. Haja ya kubadilisha Kilimo inatokana na ukweli kuwa ni moja ya sekta zinazoingiza kipato cha kigeni kwani inachangia asilimia 29.1 ya pato la taifa, huku ikichangia asilimia 30 ya fedha za kigeni. Aidha ndio chanzo pekee cha uhakika cha biashara ikitoa asilimia 65 ya mahitaji ya viwanda (ghafi) na asilimia 90 ya chakula cha taifa huku ikiajiri asilimia 66.9 ya nguvu kazi ya Taifa. Ndugu Peter Lanya, aliekua Makamu Mwenyekiti wa TCCIA, akitoa ufafanuzi zaidi alisema kwamba kunatakiwa mabadiliko katika sera hiyo ili kuupa usasa kwa kuwekeza kwenye mahusiano ya kilimo, mali ghafi kama taifa likitaka kuendelea kuelekea uchumi wa viwanda. Naye ndugu, Joseph Kihaule, Afisa Mkuu wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi, alisema kwamba kuna haja ya kubadilika katika kilimo ili kuweza kufanya vyema huku akisema mazungumzo ya kimataifa ya kupata muafaka, hususani yahusuyo mabadiliko ya tabia nchi, ni muhimu yakaunganishwa na sera mbalimbali ili kuimarisha kilimo na upatikanaji wa chakula. Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa TCCIA, Peter Lanya akizungumzia SIDP 1996-2020 wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Ushirikishaji Kikanda kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bi. Sekela Mwaisela.[/caption] Awali akifungua semina hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji (viwanda) Adelhelm Meru alishukuru taasisi za ERSF na CUTS International kwa kuona umuhimu wa kuwa na mkutano huo wanne wa kitaifa kuzungumzia mradi wa PACT-EAC. Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Viwanda Ushirikishaji Kikanda, Bi. Sekela Mwaisela alisema kwamba wizara inatambua haja ya kuweka pamoja viwanda na uchakataji wa mazao ya kilimo kwa kuwa inasaidia kuweka sawa maendeleo ya viwanda. Alisema kwamba kazi iliyofanywa na ESRF inaiweka wizara hiyo katika nafasi bora zaidi ya kufanya mabadiliko ya muhimu kufikia mwaka 2020. Alisema sera hiyo iliyoanza 1996-2020 imepita katika maeneo matatu ambayo yalilenga kuimarisha uwezo wa viwanda (1996-2000), matumizi ya teknolojia (2000-2010) na uimarishaji wa viwanda 2010-2020. Alisema SIDP imesaidia kuimarisha viwanda na sasa lazima kuwepo na uangalizi ili kuwepo na mahusiano mazuri kati ya sera zote zinazotegemewa kuwezesha maendeleo endelevu ya viwanda. Afisa Mkuu wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Joseph Kihaule akichangia maoni katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption] Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida katika hotuba yake iliyosomwa na Prof. Fortunata Makene amesema ipo haja kubwa ya kuwepo kwa mabadiliko katika SIDP kutokana na mahusiano yake na sekta nyingine hasa yenye uhusiano na kilimo. Katika mkutano huo wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), Dk Kida alisema kwamba taasisi yake imefurahi kutoa mchango kwa ajili ya kusaidia kuimarisha viwanda nchini. Alisema mkutano huo unaoangalia namna ya kuboresha sera ya viwanda, SIDP (1996-2020), kabla ya utafiti utakaoanza baadae ni muhimu katika kuona kwamba kilimo kinaboreshwa sanjari na SIDP kwa kuweka mahusiano ambayo awali yalikosekana katika sera ya SIDP. Pichani juu na chini sehemu ya washiriki wakichangia maoni wakati wa mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption] Alisema kwa taifa la Tanzania ili lisonge mbele ni vyema masuala muhimu katika SIDP yakaangaliwa ili kutekeleza mipango ya maendeleo ya viwanda kwa kuhusisha na uchakataji wa mazao ya kilimo. Aidha alisema katika utafiti utakaosaidia kuboresha SIDP majukumu ya biashara ya kimataifa katika maendeleo ya viwanda na tabia nchi haviwezi kudharaulika. Alisema utafiti utakaofanywa utasaidia kuongeza ‘nyama’ zaidi katika mikakati ya maendeleo kwa kufanya utetezi kwenye mabadiliko ya tabia nchi, biashara na usalama wa chakula kwa kufanya mabadiliko makubwa katika uchakataji bidhaa za kilimo kwa kutambua pia makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania ni mshiriki, hususani UNFCCC na WTO. Picha juu na chini washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi walioshiriki kwenye mkutano huo. Picha ya pamoja ya washiriki.

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA NDG: RODRICK MPOGORO AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA MAKATIBU WA UVCCM MIKOA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI

Naibu katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi ndg; Rodrick mpogoro akifungua Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam.
 Mwenyekiti wa umoja wa Vijana na mjumbe wa kamati kuu  ya Chama Cha Mapinduzi Ndg:Sadifa Juma khamisi akizungumza katika Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam
 Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam


washiriki wa mafunzo elekezi wakifuatilia mafunzo
mshiriki Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa kirimanjaro ndg; abdulrahim hamid akiuliza swali wakati wa Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaa.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More