WAKATI wananchi wanajiandaa kushiriki
Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, Mahakama ya
Hakimu Mkazi Iringa imewahukumu Majuto Kisumbe (22)na Zawadi Mdegela
(33) kulipa faini ya laki moja au kwenda jela mwaka mmoja baada ya
kukiri kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la Kudumu
la Mpiga Kura .
Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi
Andrew Peter Scout alisema Kisumbe na Mdegela wamehukumiwa kulipa faini
au kenda jela mwaka moja kwa kosa la kujiandisha mara mbili kwenye
Daftari la Kudumu la Mpiga Kura (BVR) kinyume na Sheria ya Uchaguzi ya
mwaka 2010.
Alisema kuwa katika nyakati tofauti
Kisumbe, mkazi wa Mahenga wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa na Zawadi
Mdegela wa Ifunda wilayani Iringa walijiandikisha mara mbili katika BVR
katika vituo viwili tofauti.
Hakimu Mkazi Andrew Peter Scout alisema
Kisumbe alitenda kosa hilo tarehe 04 Aprili mwaka huu katika Kijiji cha
Mahenge, Wilaya ya Kilolo.
Alisema kuwa mtuhumiwa Kisumbe alikutwa
na kadi mbili za kupigia kura zenye namba T-1000-7557-236-8 na T-
1000-1387-385-4 alizojiandikisha katika sehemu tofauti eneo la Mahenge.
Naye Mdegela alikutwa na kadi mbili zenye namba T-1001-3631-728-2 na T-1001-2848-874-4.
Hata hivyo hakimu mkazi huyo alisema
kuwa Majuto Kisumbe na zawadi Mdegela wamepoteza sifa ya kupiga kura
katika uchaguzi mkuu mwaka huu kutokana kujiandikisha mara mbili kwenye
daftari
Kesi hizo ziliendeshwa katika mahakama
isiyo wazi na washitakiwa waliomba wapunguziwe adhabu na hakimu
alizingatia hilo kwa vile washitakiwa walitenda kosa hilo kwa kutojua na
ni mara yake ya kwanza alisema kuwa walipa faini y laki mmoja au jela
mwaka moja.
Wananchi wengi waliofikisha miaka kumi na nane (18) na kuendelea tayari wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni hitaji la Kikatiba.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa
jukumu la kisheria la kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura pamoja na kuliboresha kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais,
wabunge na madiwani.
Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mkoa wa Iringa aliongeza kuwa mfumo mpya wa BVR utasaidia kupunguza au
kuondoa matatizo yaliyomo kwenye daftari lililopo ikiwamo kuzuia mtu
kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) ilibaini kuwa jumla ya wananchi 231,955 nchini walijiandikisha
zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Baada ya kuchakata daftari, mchakato wa
mwisho wa kuhakiki daftari, hatimaye idadi halisi ya wapiga kura ni
23,154,485 ambapo 22,651,292 waliandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) na 503,193 waliandikishwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
0 comments:
Post a Comment