Wednesday, October 21, 2015

WARIDHISHWA NA HUDUMA ZA KITUO CHA AFYA KIVUNGE, UNGUJA

IMG_20151016_175545

Pichani juu na chini ni muonekano wa Jengo la kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini "A" visiwani Unguja kilichojengwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi wetu
BAADHI ya Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wameelezea kuridhishwa kwao na huduma za afya zinazotolewa katika kituo kipya cha afya cha Kivunge.
Kituo hicho kimejengwa chini ya mradi wa Umoja wa Mataifa(UN) wa kuviwezesha vituo vya afya mbali mbali nchi ambapo kituo hicho kinatoa huduma mbali mbali za akina mama na watoto pamoja na masuala ya kutibu vidonda na majeraha mbali mbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkazi wa kijiji hicho, Kassim Haji Simai alisema kituo hicho kimekuwa mkombozi wa wananchi kwani pindi panapotokea mgonjwa wa ghafla ufika katika kituo hicho na kupewa matibabu ya haraka.
Alizitaja changamoto kubwa iliyopo kituoni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa madakta na wauguzi jambo ambalo baadhi ya wananchi ukaa muda mrefu wakisubiri huduma kwani wagonjwa wanakuwa wengi kuliko watoa huduma.
IMG_9525
“Tunawashukru sana wafadhili waliojenga kituo hiki na serikali kwa ujumla kwani wametusaidia sana huduma hizi tulikuwa tunazifuata mbali sana”, alisema Haji.
Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alifika katika kituo hicho na kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo hicho na kuona ni jinsi gani kinatoa huduma kwa wananchi.
Alisema kuwa ufanisi wa mradi huo unaongeza ushawishi kwa Umoja wa Mataifa kuongeza zaidi msaada hasa vifaa vya kisasa vya huduma za afya pamoja na wataalamu wa afya ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za afya kwa ufanisi zaidi.
“ Kituo hiki kinatoa huduma kwa wananchi wengi hivyo nitapeleka salamu makao makuu ili tujadiliane na kuona ni jinsi gani tunaendelea kusaidia kituo hiki hasa katika suala la vifaa vya kisasa na madaktari.”, alifafanua Bw.Rodriguez.
IMG_9533
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitazama jengo la kituo cha afya Kivunge alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuaznishwa. Kulia ni Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt.
Naye Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James alisema kituo hicho kinatoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji kwa wananchi ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 100 hadi 200 hali ambayo kitathimini ni kubwa kutokana na uwezo wa kituo hicho kimatibabu.
Alisema kuwa bado wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuongeza vifaa na madaktari ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora ili kufikia dhana ya umoja wa mataifa katika masuala ya afya ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya na endelevu.
IMG_9557
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho huku akiwa ameambatana na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (nyuma ya Alvaro) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu. Kulia ni Daktari wa kujitolea anayehudumia wangonjwa katika kituo hicho Alexander Vogt.
IMG_9564
Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt akimwonyesha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez baadhi ya ripoti za magonjwa yanayowasumbua watoto chini ya umri wa miaka 5 wanaopatiwa matibabu katika kituo hicho.
IMG_9574
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na Dr. Mohamed Abdallah (kulia) aliyekuwa akitoa huduma kwa mtoto Salma Shamis mwenye siku 10 ambaye anasumbuliwa na masikio wakati Bw. Rodriguez alipofanya ziara fupi ya kukagua kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” visiwani Unguja kilichojengwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
IMG_9591
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye vyumba vya madaktari kama walivyokutwa na kamera yetu.
IMG_20151016_175753 IMG_9612
Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James akizungumza na waandishi wa habari waliombatana kwenye ziara hiyo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
IMG_9621
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto Shekha Khamis (3) mkazi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” aliyefika kituoni hapo kupatiwa matibabu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More