KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Mufindi Gimson Mhagama amewataka vijana
kuwaepuka na kuwakwepa wanasiasa uchwara wanaotaka kuwatumia kama madaraja ya
kupitia ili kutimiza malengo yao kwa kwa
kuwahamasisha kufanya vurugu kwenye vituo vya kupiga kura siku ya uchaguzi kwani watu hao hawana nia njema na taifa hili
bali wanatakakuvuruga amani ya nchii hii
Alisema kuwa amani ambayo tunajivunia ipo siku
itatoweka na iwapo vyama vya siasa vitaacha kufanya kazi yake ya kisiasa kwa
kunadi sera za vyama vyao na kueneza chuki dhidi ya serikali kama ilivyo hivi
sasa kwa baadhi ya vyama kuendesha siasa za chuki na kuwatumia vijana kuvuruga
amani yetu.
Akizungumza katika kampeni za kuwanadi mgombea udiwani na mbunge katika
kata ya mbagala wilayani Mufindi mkoani Iringa Mhagama ilisema kuwa kumekuwa na
wasasiasa wasio na nia njema na vijana na kuamua kuwalisha viroba na bangi na
kuwamuru kwenda kufanya fujo katika
mikutano ya ccm jambo ambalo ni kuvuruga amani ili
yopo kwani wanamufindi walizoeya kufanya kampeni za kistarabu lakini sasa
inaonekana kama vita kutokana na watu wachache
wanaotaka madaraka kwa
mabavu badala ya sera za chama chake
“Ndugu zangu
na vijana wenzangu sisi bado umri wetu unadai tusikubali kushawishiwa na
watu wachache eti kwa kuwa alikupa elifu kumi na viroba uende kufanya fujo
kwenye kampeni za ccm au kwenda kufanya vurugvu kwenye vituo vya kupigia kura
nawambia anawapotosha na matokeo yake
utakubwa na matatizo na kuanza kulaumu serekali ,hawa
watu wasitufanye hatuna akili wewe piga kura rudui
zako nyumbani kwa ustarabu hakuna atayekugusa
kama kulinda mwambie alinde yeye “
Alisema katika jimbo lake la mafinga mjini kuna
vijana wengi wameingia kwa makundi makundi
kwa awamu tofauti kutoka katika mikoa ya Arusha ,Mbeya na Morogoro na lengo la vijana hao wanaosemekana kudhaminiwa
na mgombea ubunge wa jimbo la Mafinga mjini Wille Mungai ni kwa ajili
ya kufanya vurugu siku ya uchaguzi na wengine
wamekuwa wakisambazwa
katika mikutano ya ccm na kufanya vurugu za kupiga
watu na kufunga barabara ili wanaccm
wasipite kwenda kufanya kampeni
Aliwaeleza kuwa nchi hii inaongozwa kwa misingi ya
sheria za nchi hivyo kila mmoja anapaswa kuziheshimu na kuzifuata kwa kuwa wako
watu wanaojifanya wako juu ya sheria na kuwataka watu wote kujitokeza kwenda
kupiga kura kwa kuwa jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda raia na mali zaa
hivyo kila mmoja anapaswa kwenda kutimiza haki yake ya msingi ya kupiga kura
“Kuna watu humu jimboni mwetu wamezoeya jela na
wengine walikuwa wanakesi lakini walitoka kiujanja unjanja na ndio anaotusumbua kwa kupiga wanachama wetu sasa
tusubiri tu Mh John Magufuli aingie
madarakani baada ya ninyi wanachi kumpa ridha kuna
watu wataona hii nchi chungu kwa maaovu waliofanya ndio mana wanamuogopa na
mimi ninaamni huu ndio mwaka wa mabadiliko na tutashinda kwa kishindio ndio
na wale waliotoka kiujanja ujanta wataisoma nambaa
Kwa upande wake Gift Mwachanga aliyekuwa kada
maarufu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na hatimaye kujiunga na
chama cha mapinduzi ccm alisema sio
jambo la busara wanasiasa kutumia
majukwaa
yao ya siasa vibaya kwa kuwatuma watu kufanya vurugu
katika mikutano ya kampeni na wengine kuwahadaa kuwa wakalinde kura katika
vituo ila hali wao na watoto wao watakuwa majumbani kwao
mamepumzika huku wakila bata
Mwachanga alisema jambo kubwa liliomfanya kuondoka
ndani ya chama hicho ni kukiukwa kwa misingi ya demokraisa ndani ya chama hicho
kwani watu wachache ndio wenye sauti ndani ya chama huku wengine wakiwa ni
bendera fuata upepo hivyo akamua kujiengua ili
kusiadia kuleta maendeleo katika jimbo hilo kupitia ccm tofauti naapo
awalia ambapo
alikuwa akipinga kila kitu hata kama ni kizuri ili
mradi tu kimesemwa na mtu kutoka chama cha mapinduzi( CCM)
0 comments:
Post a Comment