Kijiji cha Magigiwe kilichopo kata ya Miombweni wilayani Mbarali hakijawahi kuwa na shule wala zahanati tangu kianzishwe,hali ambayo inasababisha watoto wanaoishi kijijini hapo kusafiri umbali wa zaidi ya kilometa saba kwenda katika shule ya jirani ya Mapogoro kupata elimu.
Kijiji hicho cha Magigiwe chenye wakazi zaidi ya 900,wengi wao
wakiwa ni jamii ya wafugaji,hakijawahi kuwa na shule ya msingi wala
zahanati,changamoto ambayo imeibuliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii wa
TASAF awamu ya tatu ambao umeamua kuwapelekea mradi wa ujenzi wa vyumba
vitatu vya madarasa,mradi ambao umepokewa kwa furaha na wananchi hao
ambao nao wameamua kujitolea nguvu zao ili kufanikisha ujenzi huo.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mbarali,Venant Komba
amewapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa kujitolea kushiriki katika
ujenzi wa shule hiyo, huku mratibu wa TASAF wilaya ya Mbarali,Amos
Chiwaya akisema kuwa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya
TASAF awamu ya tatu yenye maeneo manne ya utekelezaji.
Mkuu wa wilaya ya mbarali,Gulam Hussein kifu ametembelea kijiji
hicho na kushiriki katika shughuli za ujenzi wa shule hiyo,huku
akiwataka wananchi hao kuongeza bidii ili mradi huo ukamilike kwa wakati
na hatimaye waweze kuletewa mradi mwingine wa zahanati.
0 comments:
Post a Comment