Tanzania imeandika historia mpya, ambapo jana imempata Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli, ambaye alikuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu uliohitimishwa Jumapili ya Oktoba 25, mwaka huu.
Dk
Magufuli ambaye katika kampeni ya kuwania urais alikuwa na kauli mbiu
ya Hapa Kazi Tu, si mgeni katika safu za uongozi wa Tanzania kwa kuwa
amekuwa serikalini kwa miaka 20, akishika majukumu mbalimbali ambayo
yalitumiwa na Watanzania kumpima.
Moja
ya sifa yake kubwa tangu alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia
chama hicho mwishoni mwa Mei mwaka huu, ni uadilifu katika utendaji kazi
wake katika majukumu tofauti aliyokabidhiwa Rais huyo mteule wa Awamu
ya Tano, anatajwa kuwa katika majukumu yote ya kitaifa aliyowahi
kukabidhiwa, alionesha sifa ya juu ya uaminifu na uadilifu, ambao
umeelezwa kwa namna mbili tofauti.
Ujenzi barabara
Kwanza ni uongozi wake wa miradi mikubwa ya fedha nyingi, ambayo kwa muda wote wa uongozi wake hakuwahi kukumbwa na kashfa. Kwa mfano mwaka huu tu, alikuwa akiongoza Wizara ya Ujenzi, iliyokuwa na bajeti ya Sh trilioni 1.2 na Mfuko wa Barabara uliokabidhiwa zaidi ya Sh bilioni 866.

Katika
miaka 15 aliyoongoza Wizara hiyo ya Ujenzi, katika ngazi hiyo
alisimamia miradi ya zaidi ya Sh trilioni 9.5, lakini hakula hata senti
tano, badala yake alijenga mtandao mrefu wa barabara za lami nchi nzima.
Usimamizi
Namna ya pili ya kuzungumzia uadilifu wake ni usimamizi wake wa watendaji na wadau wa sekta ya ujenzi, ambao amekuwa akiwapa kazi za mabilioni ya shilingi na kuisimamia kwa karibu katika kuwatumikia Watanzania.

Magufuli amekuwa akisimamia makandarasi zaidi ya 8,500, wahandisi zaidi
ya 15,000 na wakadiriaji majengo zaidi ya 1,300, ambao wamekuwa
wakinufaika na kazi za Serikali za mabilioni ya shilingi.
Kama
angetumia vibaya nafasi hiyo na angetaka kumuomba au kushinikiza kila
mmoja wao ampe Sh milioni moja tu kwa mwaka, angeweza kujikusanyia pato
binafsi lisilo halali la zaidi ya Sh bilioni 100 kila mwaka. Pamoja na
kuwa karibu na kishawishi hicho, lakini Dk Magufuli hakushiriki kuhujumu
hata senti moja na hana historia wala hakuwahi kutajwa popote kutumia
vibaya nafasi yake hiyo katika sekta yenye maslahi makubwa ya kifedha.
Ukali kwa wazembe
Badala ya kuomba michango ya kujinufaisha kutoka kwa wadau hao wa ujenzi, Dk Magufuli alijikuta akifukuza kazi makandarasi zaidi ya 3,000 wa ndani na nje ya nchi, bila kujali utajiri wao, pale makandarasi hao walipozembea kazi au kufanya kazi chini ya kiwango.

Namna
ya tatu inayotumika kuelezea uadilifu wa Dk Magufuli, imeelezwa mara
kadhaa na Jaji Joseph Warioba, ambapo alisema mwaka 1996 alipoteuliwa na
Rais Benjamin Mkapa kuongoza Tume ya Kero za Rushwa, alikuta sekta ya
ujenzi ikinuka rushwa kubwa. Lakini, anafafanua kuwa baada ya Dk
Magufuli kuanza kufanya kazi katika sekta hiyo, kelele ya rushwa katika
sekta hiyo imetoweka. Uchapakazi Mbali na uadilifu, Dk Magufuli pia
anatajwa kuwa mchapakazi.
Hata
Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi mara kadhaa amempa jina la
‘simba wa kazi’, huku Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake, akimpa
jina la ‘tingatinga’ ambalo huwa halishindwi kazi katika mazingira
yoyote ya ujenzi, huku wananchi wengine wakimuita ‘jembe’. Matokeo ya
uchapakazi wake, yanaonekana katika sekta ya ujenzi, alikofanya kazi kwa
miaka 15 tu, ambapo amefanikiwa kusimamia ujenzi wa barabara za lami
zenye urefu wa zaidi ya kilometa 17,700.
Kazi
hiyo imeweka historia ambayo hata wakoloni, Wajerumani na Waingereza,
waliotawala Tanganyika wakati huo tangu mwaka 1884/1885 mpaka wakati wa
Uhuru mwaka 1961, zaidi ya miaka 75 walijenga mtandao wa barabara za
lami wenye urefu wa kilometa 1,360 tu.
Wasifu wake
Dk Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 Chato (sasa Mkoa wa Geita), hivyo jana alipotangazwa kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ambapo alitimiza miaka 56.

Magufuli ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 1991 – 1994 alisoma Shahada ya Uzamili
(Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha
Salford nchini Uingereza. Mwaka 1985 – 1988 alisoma Shahada ya Kwanza ya
Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na
Hisabati. Mwaka 1981 – 1982 alisoma Diploma katika Chuo cha Mkwawa
akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Kati
ya mwaka 1979 – 1981 alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya
Juu ya Sekondari Mkwawa, Iringa. Mwaka 1977 – 1978 alisoma elimu ya
sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza. Mwaka 1975 – 1977
alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera. Mwaka 1967 –
1974 alisoma Shule ya Msingi, Chato. Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria
mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha. Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.
Uzoefu wa kazi
Kuanzia mwaka 2010 alikuwa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato. Mwaka 2008 – 2010 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato). Mwaka 2005 – 2008 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).

Mwaka
2000 – 2005 Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka
1995 – 2000 Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995 Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Co-operative
Union (Ltd) Mwanza. Mwaka 1982 – 1983 Mwalimu Shule ya Sekondari
Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati). Amepata tuzo
mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki
na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa. Ameandika vitabu na
majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.
Mchakato wa urais
Dk Magufuli alitangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa Mei mwaka huu, baada ya CCM kutangaza rasmi ratiba ya mchakato wa urais kwa wanachama wake. Aliingia kwenye harakati za kuwania nafasi ya urais kimya kimya, tofauti na makada wengine wa CCM ambao walihutubia Taifa.

Lakini,
kimya chake kiliufanya mchuano wa uchaguzi wa nafasi hiyo ndani ya CCM,
uliokuwa na wagombea 42 kuwa mkali zaidi. Baada ya hapo, waliorejesha
fomu walikuwa wagombea 38 na kati ya hao baada ya kujadiliwa na vikao
vya juu vya Chama, ikiwemo Kamati Kuu, wagombea watano - Dk Magufuli,
Bernard Membe, Dk Asha Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ally na January
Makamba, ndio waliofanikiwa kupelekwa katika kikao cha Halmashauri Kuu
ya Taifa (NEC) ya CCM.
Baada
ya Nec, ambako wagombea hao walijadiliwa na kupigiwa kura, Dk Magufuli,
Balozi Amina na Dk Migiro ndio waliofanikiwa kuingia tatu bora, ambapo
walifikishwa katika Mkutano Mkuu na kuomba kura na baada ya kupigiwa
kura na wajumbe wa mkutano huo, akapatikana Dk Magufuli kupeperusha
bendera ya CCM.
Ahadi zake Dk
Magufuli katika mikutano yake ya kampeni, alikuwa akiahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi aliosema atapigania kila mmoja awe na kazi ya kumpa kipato, wajenge nyumba bora.

kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk
Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, Serikali yake itatoa Sh
milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake
na vijana. Mbali na kutoa mikopo hiyo izunguke katika ngazi ya kijiji na
mtaa, Dk Magufuli pia alisema Serikali yake itazuia kila aina ya
usumbufu, unaofanywa kwa wafanyabiashara hao, ikiwemo kukamatwa kwa
bodaboda na mama ntilie.
Kwa
wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na
mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao kwa
kuwa atahakikisha mbali na wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao,
watakapoiuzia Serikali itakuwa bidhaa kwa fedha taslimu.
Aidha, aliahidi kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara wadogo na wakulima, ili wafanye biashara kwa uhuru wajipatie kipato halali.
Aidha, aliahidi kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara wadogo na wakulima, ili wafanye biashara kwa uhuru wajipatie kipato halali.
Dk
Magufuli pia alisema baada ya kusambaza umeme, atahakikisha viwanda
vidogo, vya kati na vikubwa vinajengwa vijijini ili kusindika mazao ya
kilimo shambani ili kutoka shambani bidhaa za mazao hayo ziuzwe katika
masoko ya ndani na nje ya nchi.
Kuhusu migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, Dk Magufuli aliahidi kukabiliana na migogoro hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa ardhi zaidi kwaajili ya wakulima na wafugaji, ili kuondoa uhaba wa ardhi uliosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia mifugo na kulima.

Lakini
pia aliahidi kunyang’anya mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila
kutumiwa, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya
kilimo.
Katika elimu, alikuwa akiahidi kuhakikisha kuanzia mwakani, wanafunzi kutoka darasa la awali mpaka kidato cha nne, wanasoma bila kulipa ada, ili kuondolea wazazi usumbufu wa watoto wao kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada.

wanafunzi wa elimu ya juu, aliwahakikishia kuwa hakutakuwa na usumbufu
wa kupata mikopo na kuwataka wanahusika na kazi hiyo, kuwa tayari kwa
kuwa atataka kila mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu, apate mkopo.
Katika sekta ya afya, aliahidi kujenga zahanati kwa kila kijiji na mtaa, kituo cha afya kwa kila kata na hospitali ya rufaa katika kila mkoa, na ameahidi kukomesha kero ya kukosekana dawa katika hospitali za Serikali.

kero ya maji, alikuwa akisema kama amefanikiwa kujenga zaidi ya
kilometa 17,700 za barabara ya lami, hatashindwa kujenga mabwawa na
mtandao wa mabomba kwenda kwa wananchi ili kukomesha kero hiyo.
Pia
aliahidi kujenga barabara mbalimbali za lami za kuunganisha wilaya na
za mijini, huku akiahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi, ifanane na
ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), taasisi aliyoianzisha na
kuitetea, ambayo leo watu wengi wanatamani kuitumikia kutokana na
maslahi mazuri na mafanikio yake.
0 comments:
Post a Comment