mgombea Ubunge Jimbo la Kilolo Venance Mwamoto (CCM)
Mchungaji Peter Msigwa anaegombea ubunge kupitia (CHADEMA) Jimbo la Iringa Mjini
Na.Thobias Myovela, Iringa.
ZIKIWA zimebakia takribani siku 3 ili zoezi la upigaji
kura wa kuchagua madiwani, wabunge na Raisi baadhi ya wagombea ubunge kupitia
chama Cha Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kilolo na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Iringa Mjini na Kilolo, wameahidi kuboresha afya ya mama na mtoto mchanga iwapo
watachaguliwa kuwa wawakilishi wa majimbo hayo.
Wakiongea na blog hii nyakati tofauti wagombea
hao wamesemakuwa suala la afya ya mama na mtoto ni la muhimu na linatakiwa
kupewa kipaumbele na iwapo watapata ridhaa hiyo watahakikisha bajeti ya afya
inaongezwa ili kukidhi hitaji hilo.
Mchungaji Peter Msigwa anaegombea ubunge kupitia (CHADEMA)
Jimbo la Iringa Mjini amsema kuwa iwapo atachaguliwa tena kuliongoza jimbo hilo
atahakikisha usalama wa mama na mtoto unapewa kipaumbele.
Amesema kuwa ni
aibu kwa serikali nchi ya Tanzania kuwa nafasi ya 7 duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya
vifo vya akina mama ambavyo vinatokana na uzazi, na kama atafanikiwa kurudi
tena bungeni atahakikisha anasimamia ongezeko la bajeti la wizara ya afya.
Mchungaji
Msigwa ambaye ameliongoza jimbo hilo la Iringa kwa kipindi cha miaka mitano
iliyopita mesema kwamba, asilimia 40.4% ya watoto wanaozaliwa wamedumaa hali inayosababishwa na mama kutopata lishe ya
kutosha na akasema kwamba hii ni hatari ya kwa nchi kwani kila kwenye kundi la
watoto 10 basi wanne wamedumaa.
“”Kama nitaenda bungeni nitahakikisha serikali itoe
bajeti ya kutosha kwenye sekta ya afya nah ii itapunguza vifo au matatizo
yatokanayo na uzazi,lakini pia nitaanda makongamano, mikutano jimboni kwangu
ili kuhaklikisha kuwa watu wanajua uzazi salama” amesema.
Akizungumzia kuhusu umri wa miaka 19 ya wasichana ambao wanapata ujauzito wakiwa bado
wadogo, Mhesh. Msigwa amesema kwamba pamoja na kwamba anagombea kiti cha ubunge
katika jimbo la Iringa Mjini lakini yeye ni mchungaji wa kanisa la VINEYARD
lililopo maeneo ya Iringa Mjini, kwa mujibu wake amesema kwamba huwa anawahusia vijana kuwa na maadili mema na
kumpendeza Mungu.
Amesema kwamba anapenda kuona vijana wanafunga ndoa na
kupata watoto ndani ya ndoa na wala sio kuzaa bila mpango na kusababisha kuwa
na watoto wanaozurura barabarani bila mpango wowote ule.
Kwa upande wake mgombea Ubunge Jimbo la Kilolo Venance
Mwamoto (CCM) amesema kwamba iwapo atachaguliwa kuwa mbunge atahakikisha kwamba
anaisimamia ilani ya chama chake ya mwaka 2015-2015 ambayo inasema kila kijiji
kuhakikisha inakuwa na zahanati ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Amesema kwamba vifo vingi vinatokea hasa kijijini
sababu baadhi wao wapo mbali na huduma za afya na siku zao za kujifungua
zinapokaribia huchelewa kufika katika vituo vya afya nah ii inatokana na umbali
wa huduma hizo
“ Nikichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kilolo
nitahakikisha vituo hivyo vinajengwa kama ilani yetu ya Uchaguzi kupitia
chamamchangu inavyoelekeza,lakini pia nitahakikisha usafiri kwa madaktari
kuwafikia walengwa” amesema Mwamoto na
kuendelea kusema kuwa “ uwazi pia
unahitajika katika vituo vya afya ijulikane bajeti iliyotengwa kwa ajili ya
madawa nah ii itasaidia kupunguza kukosekana kwa madawa katika vituo hivyo”.
Akizungumzia suala la wasichana kupata mimba katika umri
mdogo Bw. Mwamoto amesema kwamba linatokana na baadhi yao kutokuwa na kipato na
hivyo hujikuta wakijiingiza katika mahusiano yanayowapelekea kupata mimba
katika umri mdogo
“Katika hili nitahakikisha mikopo inayotolewa na
serikali iwafikie walengwa mapema kwa uwazi, fedha nyingi haziwafikii wahusika,
lakini pia nitaanzisha klabs za vijana katika mashule ambao watatoa elimu ya
uzazi mashuleni kama zilivyo klabs za kupinga rushwa na hata wale waliopata
mimba wakiwa na umri mdogo watashiriki ili kuwasisitizia wasichana wenzao
wasome na sio kufanya mambo mengine tofauti na elimu”
Brayan Kikoti anaegombea ubunge kupitia (CHADEMA)
Jimbo la Kilolo nae amesisitiza suala la elimu linahitajika kama vile ilani yao
inavyosema kipaumbele cha kwanza hadi cha tatu ni elimu.
Amesema kuwa suala la afya ya mama na mtoto elimu
ambayo imekuwa ikitolewa na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali lakini
hayajapewa kipaumbele nahii inatokana na wanaopelekewa huduma hiyo kutoona
umuhimu wa suala hilo.
Amesema ni lazima wakazi wake wa eneo husika wapewa
elimu husika kuhusiana na afya ya mama na mtoto ili kuhakikisha vifo vinapungua
au kwisha kabisa.
Amesema kuwa serikali ijenge zahanati karibu na maeneo
ya wananchi na siyo mijini peke yake kwani asilimia kubwa ya wananchi wanaishi
vijijini.
Akizungumzia vifo vya watoto wachanga, Kikoti amesema
pia inasabishwa na na baadhi ya akina mama kutokuwa na elimu ya kutopsha pindi
wanapopata ujauzito hasa wa vijijini kwani kuna hatua za ukuaji wa mtoto ambako
maelezo yote wanayapata wanapoenda kliniki na baadhi ytao hawapati huduma hizo
za klinini.
“Huko vijijini wengi hawana elimu jinsi ya kulea
ujauzito wao, wengine wanakunywa pombe sana, hawazingatii mlo unaohitajika nah
ii yote kwa sababu hawana elimu ya kutosha sasa hawa wakielimishwa vya kutosha
vifo vinaweza kupungua,, wataweza kuhudhuria kliniki na kama watagundulika wana
matatizo ni rahisi kuwasaidia mapema, lakini uwepo vifaa vya kujifungulia kwa
mama ni muhimu na dawa zipatikane kwa urahisi na siyo kupewa maelekezao na
daktari maduka ya kununua dawa sasa hapo
unajiuliza huyu daktari kajuaje kama kuna dawa kwenye maduka hayo? ” amehoji.
Kuhusiana na asilimia 44.45 ya wasichana wenye umri wa
miaka 19 kupata ujauzito mapema Bw. Kikoti amesema kwamba wengi wao wanapata
mimba wakiwa majumba na asilimia kama 2% ivi wanapata wakiwa mashuleni.
Amesema wale wanaopata wakiwa mashuleni ni kwa sababu
wanakaa umbali mrefu na shule zao na njiani wanakutana na changamoto mbalimbali
zinazowapelekea kupata mimba wakiwa na umri mdogo, na kama atachaguliwa kuwa
mbunge wa jimbo hilo atahakikisha shule zilizo mbali na makazi ya wananchi
kujenga mabweni yakutosha pia shule zingine zijengwa na maeneo ya wakazi hao.
“Mie nimesoma shule ya Uduzungwa sekondari na hata
hili suala la wasichana kupata mimba wakati ule lilikuwepo wengine walikuwa
wakitoka umbali mrefu,sasa hujui njiani anakutana na watu wa aina gani hadi
afike shule,nikichaguliwa kuwa mbunge nitahakikisha kuwa mabweni yanajengwa
kwenye shule na pia hata ujenzi wa shule kwenye maeneo ya karibu na wakazi wa
maeneo husika” amesema Bw. Kikoti.
Pia amesema kwamba atahakikisha viwanda vilivyofungwa
vinafufuliwa upya na akatolea mfano wa kiwanda cha chai kilichokuwepo Dabaga wilaya
Kilolo ambacho kilifungwa na kwa mujibbu wa Bw. Kikoto kiwanda hicho kilianza
kuinua uchumi wa wakazi wa maeneo ya Kilolo, amesema iwapo kiwanda hicho
kitafufuliwa kitaongeza ajira kwa vijana wa maeneo husika na hivyo wananchi
watakuwa na kipato cha kutosha katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment