Tuesday, January 31, 2017

CCM MKOA WA IRINGA YASHEHEREKEA MIAKA 40 YA CHAMA HICHO












WILAYA YA IRINGA YAENDELEA NA KAMPENI YA UPANDAJI MITI











RAIS MAGUFULI ALIVYOKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Malawi Peter Mutharika kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Rais wa Malawi Peter Mutharika pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kidemokrasia ya Sahrawi(SADR) Brahim Ghali katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.

PICHA NA IKULU

Juma Pondamali "Mensa" akijieleza kuhusu soka tangu akiwa na miaka 13

Mcheza soka mkongwe hapa nchini maarufukama Juma Pondamali “Mensa” ambeye kwa sasa ni kocha wa “Young Africa” amefunguka mbelea ya Super News Tv Online na kumtaja kocha ambaye alimkuza kisoka toka akiwa mdogo yaani umri wa miaka 13-14.

Juma Pondamali alikuwa ni golikipa hodari aliye fanikiwa kuiwakilisha Tanzania miaka ya 1980 katika michuano ya “African Cup of Nation”.
Tumia dakika zako kadhaa kuitaza hii video ili ujue mengi kuhusu Nyota huyo.  Endelea kutufuatilia hapa soon tutakuletea Taarifa yake mpya ya kuachia wimbo wake wa singeli…..

MHANDISI MTIGUMWE AWAONDOA HOFU WATUMISHI KUHAMIA DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo


Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo amewaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuhusu zoezi la serikali kuhamia Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa Umma.

Mhandisi Mtigumwe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu cha kuhusiana na uamuzi wa serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi mkoani Dodoma kilichokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea mjini Dodoma.

Mtigumwe amebainisha kuwa Awamu ya Kwanza ya uhamisho utawahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, ambapo katika mchakato huo watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia tarehe 14 – 15/2/2017 na wengine 47 waliobaki watahamia muda wowote katika kipindi cha kuanzia mwezi Februari hadi kufikia mwezi Juni.

Mtigumwe amewaeleza watumishi hao kuwa maandalizi ya ofisi za Wizara ya kilimo zilizopo mjini Dodoma zinaendelea vizuri na tayari baadhi ya maeneo yamekamilika huku mengine yakiendelea kukamilishwa ili kukidhi matakwa kwa ajili ya watumishi wote watakapohamia mjini Dodoma.

Uamuzi wa Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuhamia mjini Dodoma ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Serikali yote kuhamia Dodoma ili kutekeleza uamuzi uliofikiwa tangia miaka ya 70 na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutambua na kutangaza kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.

Mhandisi Mtigumwe amebainisha hayo hii leo katika kikao cha pamoja na watumishi wa wizara ya kilimo katika Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI YAINGIA KATIKA TUHUMA NZITO YA ARIDHI WANANCHI WAWAJIA JUU

 MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja  ni chake sasa hivi kiwancha hicho  kinataka  kunyang’anywa na halmashauri  ya Wilaya ya Monduli

 wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo 

 wamama wa kijiji cha Lendikinya   wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara



 MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Lendikinya



 Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo

Habari picha na  Woinde  Shizza,Arusha
 Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi  na kuwanyima  baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao
Hayo wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha  Lendikinya   kilichopo ndaniya halmashauri  ya  Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu zao .
Mmoja wawananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata  alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.
“Tumekuja apa siku nyingi lakini tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama waCCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa amevamia  msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hay o hayo kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti

Akiogea katika mkutano huo  Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa  halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama  chao  hakitakaa kimya kwa hilo.
Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi hivyo anashangazwa na kusikitishwa na  kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.
Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi .
“mimi nilipata  shamba hilo kama mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa  shamba hilo kama kiongozi wa CCM hivyo nashangaa sana kwa  kitendo cha kuingiza chama katika mambo yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa  na kingine kinachonishangaza  sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au tunamiliki ardhi katika kijiji hichi  kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu “alisema Sanare

 Kwa upande mwananchi mungine aliyejitambulisha kwa jina la  Olais Taiyai  alisema kuwa  ubaguzi na uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao  wanateseka na hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa  katika viwanja vyao
Naye  Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni upepo mchafu unaovuma kupitia
Hivi karibuni Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Monduli, lilipitisha azimio la kuchukua ardhi ya kijiji hicho kwa madai kuwa waliochukua ardhi hiyo hawakufuata sheria, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo.

Monday, January 30, 2017

WATANZANIA WAOMBWA KUMUUNGA MKONO RAIS DK.JOHN MAGUFULI

 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuuaga mwaka wa 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 Dar es Salaam jana. Kulia ni Msajili Msaidizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ADA na Waziri wa Nchi asiye na Wizara Maalum, Zanzibar.
 Mkutano ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari Suleiman Msuya akiuliza swali katika mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale

WATANZANIA wameombwa kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli kwa jitohada zake anazozifanya za kupongoza nchi.

Mwito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kuuaga mwaka wa 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 Dar es Salaam jana.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikifanyakazi kubwa ya kudhibiti mirija ya unyonyaji wa pato la Taifa kupitia watumishi hewa, wanafunzi hewa, kaya masikini bandia na kupitia wahujumu uchumi wa matumizi mabaya ya dhamana za Taifa mambo ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na vyama vya upinzani.

"Binafsi nawaomba watanzania bila ya kujali itikadi za vyama vyao kumuunga mkono Rais wetu Dk.John Magufuli na wasaidizi wake Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wengine wote kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuongoza Taifa letu la Tanzania" alisema Shibuda.

Alisema anaupongeza utumishi wa Serikali ya awamu ya tano kwa uzinduzi wa urejeshaji wa uwajibikaji wa watumishi wote kwani hivi sasa watumishi wengi wanatabia za miiko ya utiifu kwa umma.

Akizungumzia Zanzibar alisema uchaguzi umekwisha pita na Rais wa nchi hiyo ni Dk. Ali Mohammed Shein ambaye anatakiwa kuongoza nchi hiyo na wenzake waliochaguliwa ili kuiletea maendeleo Zanzibar hivyo siasa za mihemuko ziachwe.

Shibuda alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wazanzibar hasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi walioupata Jimbo la Dimani na kuwaomba walioshindwa wasivunjike moyo kuvunjika jembe siyo mwisho wa uhunzi kwani hata timu kubwa hufungwa na timu ndogo.

Akizungumzia katazo la vyama vya siasa kutofanya mikutano hadi mwaka 2020 alisema majibu ya suala hilo yatatolewa baadae baada ya kulifanyia kazi jambo hilo. 

Katika hatua nyingine Shibuda alisema Baraza la Vyama vya Siasa litakuwa mshirika rafiki wa wadau wote wa siasa na kusimamia maslahi mapana ya jamii na Taifa yanayosimamiwa na Serikali na kuungwa mkono na Bunge mfano Azimio la EPA.

Shibuda alitoa ushauri kwa vyama vyote vya upinzani kuzingatia umakini wa mabadiliko ya Tabia nchi ya mfumo wa uwajibikaji wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli.

UONGOZI WA BODABODA MKOANI MWANZA WAPONGEZA ZOEZI LA UKAGUZI WA POLISI.

Binagi Media Group
Umoja wa waendesha bodaboda mkoani Mwanza umepongeza zoezi la ukaguzi wa vyombo hivyo linaloendeshwa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.

Jana Mwenyekiti cha umoja huo, Makoye Kayanda, amesema zoezi hilo linaangazia maeneo makuu manne ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa watumiaji wa bodaboda wakiwemo abiria.

"Cha kwanza ni uvaaji wa kofia ngumu, cha pili leseni ya udereva, cha tatu kuwa na BIMA na ni ubebaji wa mishikaki. Kuna baadhi ya abiria zaidi ya 14 wametozwa faini kwa kukataa kuvaa kofia ngumu, sasa lazima tufuate sheria bila shuruti". Alisema Kayanda huku akipongeza zoezi hilo.

Kayanda aliwasihi waendesha bodaboda wote kuzingatia utii wa sheria bila shuruti ili kuondokana na mazoea yanayoweza kuhatarisha maisha yao na abiria wao pia huku akiwaonya baadhi ya abiria kuepuka tabia ya kukataa kutumia kofia ngumu kwa kisingizio cha uchafu.

"Kupanga ni kuchagua, kama hutaki kuvaa kofia nguvu ya unayopewa na bodaboda, nunua ya kwako ama mfuko wa plastiki ili ukipewa kofia uvalie maana kuna watu wanapata ajali wanapasuka vichwa na inakuwa ni tatizo kwa familia zao na taifa kwa ujumla". Alihimiza Kayanda.
Mwenyekiti wa bodaboda mkoani Mwanza, Makoye Kayanda

CHUO CHA AFRICA GRADUATE UNIVERSITY CHAWATUNUKU PhD WANAOFANYA KAZI ZA JAMII NCHINI

Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University  cha jijini Dar es Salaam, Profesa Stiven Nzowa, akiongoza mahafali ya kuwatunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) wanaharakati na watumishi wa mungu nane pamoja na wengine kadhaa waliotunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili HDD Dar es Salaam jana.

MWANASOKA DAVID AFARIKI DUNIA

Golikipa wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi kuchezea klabu mbalimbali za ligi kuu amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amethibitisha kutokea kifi hicho na kutuma salamu zake za pole kwa familia pamoja na klabu ya Kagera Sugar na kwa wote ambao wameguswa na kifo cha mchezaji huyo.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji...

MLIMBWENDE WA SHINDANO LA MISS KIBOSHO 2017 JIJINI MWANZA APATIKANA.

Baada ya mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa shindano la MISS KIBOSHO 2017 kufanyika kwa mara ya kwanza usiku wa ijumaa Januari 27,2017 na jana jumamosi Januari 28,2017 katika Ukumbi wa Kibosho Luxury Bar Kiseke Ilemela Jijini Mwanza, hatimaye mshindi amejulikana.

Mshindi wa shindano hilo lililofana vyema alikuwa ni Kephlin Jacob (katikati), nafasi ya pili ni Aida Gazar (kulia) na nafasi ya tatu ni Caren Nestory (kushoto), ambapo wanyange hao walifanikiwa kupenya na kuibuka na ushini huo miongoni mwa wanyange 10 walioshiriki shinano hilo.

Miss Kibosho 2017 iliandaliwa na Raju Entertainment kwa ushirikiano wa karibu na Kibosho Luxury Bar and Guest House Kiseke, Wema Salon, Mama Ngenda Sakon, Top Model na Hangano Cultural Group lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji vya urembo kitaifa na kimataifa.
Na Binagi Media Group
Miss Kibosho 2017 Kephlin Jacob (katikati), Miss Kibosho 2017 nambari mbili, Aida Gazar (kulia) na Miss Kibosho nambari tatu ni Caren Nestory (kushoto).
Awali hatua ya tatu bora ilikwena kwa washiriki, Caren Nestory (kushoto), Kephlin Jacob (katikati) na Aida Gazar (kulia)
Awali washiriki waliotinga nafasi tabo bora ni Caren Nestory, Jackline Moses, Denzry Michael, Kelphine Jacob na Aida Gazar.
Washiriki wote 10 wa Miss Kibosho 2017 ambao ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth Michael, Elizabeth Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline Moses, Denzry Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.

Saturday, January 28, 2017

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO WA JESHI LA PILISI,NSATO MARIJANI AWAFARIJI ASKARI WALIOPOTEZA MALI ZAO KWA TUKIO LA MOTO MJINI MOSHI.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.
Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo..
Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao.
Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.
Kamishna Marijani akita pole kwa PC  Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo.
Kamishna Marijani akimfariji  CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea athari iliyotokana na moto huo.
Kamishna Marinaji akimpa pole SGT Hashim baada ya kupoteza vitu vyote vya ndani pamoja na mavazi kufuatia moto ulioteketeza seheumu ya juu ya jengo hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuongoza Kamishna Marijani kukagua maeneo mengine  ya jengo hilo ambalo linakumbwa na tukio la moto kwa mara ya pili sasa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi ,Nsato Marijani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kutoa pole kwa asakri waliounguliwa vitu katika jengo hilo.
Waliovalia kiraia ni askari Polisi waliofikwa na janga la kuunguliwa moto vitu vya ndani pamoja na mavazi wakionekana wenye huzuni.
Afisa Mnadhimu daraja la kwanza wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani alipotembelea kambi ya polisi mjini Moshi.
Kamnada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa juu ya tukio la moto katika jengo la makazi ya askari Polisi.
Baadhi ya wanandugu wa familia zilizounguliwa moto wakionekaa wenye huzuni.
Mkuu wa Shule ya Polisi,Kamandanti Matanga Mbushi akizungumza wakati wa kuzifariji familia za askari waliopoteza vitu vyao katika tukio la moto.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisni nchini ,IGP Ernest Mangu kwa askari waliopoteza vitu vyao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa katika makazi ya askari Polisi mjini Moshi.
Mmoja wa wageni waalikwa akizungumza wakati akitoa salamu za pole kwa jeshi la polisi. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi nchini limetangaza kuwahamisha askari tisa wa vikosi mbalimbali vya jeshi hilo waliopoteza mali zao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa vya jengo la ghorofa mbili ambalo ni makazi ya askari.

Mbali na hatua hiyo jeshi hilo pia limetoa kiasi cha Sh Milioni tisa kwa familia za askari hao kwa ajili ya kuanza kununua vitu vidogo yakiwemo mavazi baada ya kutoambulia chochote wakati wa tukio hilo zikiwemo sare za jeshi hilo.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani ametoa kauli hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisi ,Inspekta Jenerali,Ernest Mangu wakati akizifariji familia za askari hao pamoja na kutembelea jengo lililoteketea kujionea athari za moto huo uliotokea usiku wa kuamkia juzi.

Akiwasilisha salamu za Pole kwa niaba ya IGP Mangu,Kamishna Marijani alisema jeshi la Polisi litaendelea kutoa msaada kwa askari hao hadi pale maisha yao yatakaporejea huku akivishukuru vikosi vya jeshi la zima moto vya uwanja wa ndege wa KIA,kiwanda cha sukari cha TPC na Halmashauri kwa kazi waliyofanya.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa amemwelea kamishna Nsato kuwa thamani ya mali za askari zilizoteketea kwa moto imefikia sh Mil 93.9 huku akiomba wadau kujitokeza kusaidia familia hizo.

Tukio la moto katika jengo hilo lililopo jirani na ofisi za kikosi cha kutuliza ghasia lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 2:30 usiku ,ukianzia katika chumba kimojawapo cha ghorofa ya pili na kuenea katika vyumba vingine nane wakati huo umeme ukiwa umekatika.

Kufuatia moto huo familia tisa za askari hao zenye jumla ya watu 40, ambao 23 ni watu wazima na 17 ni watoto tayari zimepatiwa malazi ya muda katika chuo cha Polisi Moshi wakati taratibu nyingine za kuwasaidia zikiendelea.

Tayari jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limeunda timu ya wataalamu kutoka katika jeshi hilo wakisaidiana na wale wa kikosi cha zimamoto pamoja na shirika la umeme (TANESCO) kufanya uchunguzi wa matukio ya moto katika jengo hilo.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More