Saturday, October 31, 2015

ASKARI WA KIKOSI CHA UPELELEZI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI SHINGONI

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?view=att&th=150bdff8c446975b&attid=0.1&disp=inline&realattid=file0&safe=1&zw&saddbat=ANGjdJ_joySY0ohOhzwcnrrpp7U7iluESV3i8d4MV5-jIC5JtSYWT0605cQkDqR9T0FcZRtt4ycxzHRS27j4XtDq8XwxlO65rJpgWbSay6_iHnNEg8oy8WaZDsTe9Q-z3RZ7tYUCuWK2gJrqYVCZRzifcn15kGyOxWFe0jig8YkW9TJEvuqTHP7nfFyLC4GHRWWV499nP7pfS4mXZDWbcGbF1TjUixB3wXxOVY38Zag6iVurwHG8Mq__7ZwdpTXm-lAEnMzzcF9FEStXPYfLeaoj_RXht-_EroaBGCJZQhzDIfAPPQEf6OaLhzlmilhgZdWKZ68e4WFdmG3ZkXhM1AxIDkJmnEltc1cxnMY4YXvuCYEg1MPtj8ZyjJHkETDVmU7uQqVJQsB0NQ3VLGHLYuay2_t50R0QNlq5upoZ_DGvuOuz7wSpG5UAdttt5lQ_7dMtrcFN_quIiZFjwf3eJKGRTXsJrgwQimR5iID6Ko1OR4RRfaAg0hAPZkN8rrmbUDiIhSC9deguKOEqQ6TJNsp1gXdiKoCI0hIJAtRp79E62vv6DuO4qx014graBOpJVyP1Y_BUDV3VaOWm5zaWum6aEvV5omACCBWcunslLySQTqexpZUzTUYiZLZBcf4

 
Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na ujambazi mkoa wa Iringa Pascal Shila (30) pichani amejiua kwa kujipiga risasi kichwani kutokana na msongo wa mawazo.

Askari mwenye namba G.343D/C Pashal James Shila wa Ofisi ya RCO-Kikosi cha Anti Robbery amejiua kwa kujipiga risasi na mwili wake kukutwa kwenye jengo bovu la ghorofa la mjerumani lilipo nyuma ya kituo cha polisi.

Akizungumza na mwangaza wa habari blog wakati wa kuaga mwili wa marehemu kwenye kituo kikuu cha polisi Manispaa ya Iringa, Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea jana kati ya saa tisa na kumi jioni.

Kamanda Mungi alisema askari huyo kutoka ofisi ya upelelezi mkoa wa Iringa (RCO) alichukua silaha aina ya ya SMG saa sita mchana kutoka kwenye ghala ya kuhifadhia silaha kwa madai kuwa yeye na wenzake wanakwenda kufanya kazi ya dharura huko Ifunda.

Alisema baada ya hapo hakuonekana na saa saba mkewe alikwenda kwenye ofisi ya RCO kupeleka ujumbe alioandikiwa na mumewe kuwa amtunzie watoto kwa kuwa anawapenda sana.

Kamanda Mungi alisema kufuatia ujumbe huo askari wenzake walianza kumtafuta na baadaye kukuta mwili wake ukiwa kwenye jengo lililopo nyumba ya kituo kikuu cha polisi akiwa amejipiga risasi shingoni karibu na kidevuni na kabla hap alimtumia mkwewe meseji aliomba amtunzie watoto wake kwani ana wapenda sana.

Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuweza kubaini
chanzo cha tukio hilo na kuwa huenda limesababishwa na msongo wa mawazo aliokuwa nao marehemu.

Alisema tukio hilo limewaumiza askari sote kwa kuwa alikuwa anachukia uhalifu kwa dhati na kuwa mwili wake utasafirishwa kesho kwenda nyumbani kwao wilayani Kyela katika kijiji cha Ilolo kwa ajili ya mazishi.

Aidha alisema matukio kama hayo yanawakuta askari kwa kuwa nao ni sehemu ya jamii na kuwa jeshi la polisi hutoa mafunzo ya jinsi ya kupambana na msongo wa mawazo kwa askari wao.

Hata hivyo habari ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa jeshi la
polisi mkoa wa Iringa zinaeleza kuwa chanzo cha msongo wa mawazo.

Uchunguzi awali unaonyesha kuwa kulikuwepo na ugomvi baina yake na mkewe usiku jana.

Jesca: Siwezi kujiuzulu kwa shinikizo la majungu, fitina na vikundi vya uasi...


Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akizungumza na waandishi wa habari jana. 



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amesema hawezi kujiuzulu nafasi yake hiyo kwa shinikizo linalotokana na majungu, fitina na vikundi vya uasi vinavyoanzishwa ndani ya chama kwa lengo la kulinda maslai ya watu fulani.

“Hizi ni hoja zisizo na mashiko, hivi inawezekaneje mimi na hao wengine wanaowataja katika kipindi chote cha kampeni tufanye kazi ya kukihujumu chama, tuvumiliwe tuendelee na kazi hiyo, halafu tuhuma hizo zije zitolewe sasa baada ya kushindwa uchaguzi?” alisema.

Kwa kutumia vikao na taratibu zingine za katiba yake, CCM inapaswa kukaa chini na kufanya tathmini ya kina ili kujua sababu zilizopelekea wakapoteza jimbo na kata hizo.

Wanachama hao wanawatuhumu viongozi hao kuwahujumu katika Uchaguzi Mkuu wa mbunge, madiwani na rais hali iliyosababisha kipoteze jimbo hilo na halmashauri baada ya kupoteza kata 14 kati ya 18. 

Hivi karibuni, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini, Ahamed Sawa alimtangaza Mchungaji Peter Msigwa aliyewania ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa mshindi baada ya kuzoa kura 43,154 dhidi ya kura 32,406 alizopata mgombea wa CCM Frederick Mwakalebela. 

Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni Chiku Abwao wa ACT Wazalendo (411), Daudi Masasi wa ADC (123), Paulina Mgimwa wa Chausta (66) na Robert Kisinini wa DP (56). 

Wakiongea kwa kupokezana na bila kutaja majina yao wanachama hao waliokuwa wamebeba mabango yaliyowataka viongozi hao kuachia ngazi, walisema wanao ushahidi unaodhihirisha jinsi viongozi hao walivyofanya kazi iliyosababisha wapoteze jimbo, kata 14 na mgombea wao urais, Dk John Pombe Magufuli kupata kura 36,584 dhidi ya kura 38,860 alizopata mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa. 

Katibu wa CCM Iringa Mjini, Elisha Mwampashi aliwataka wanachama hao kutumia vikao vyao vya kikatiba kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya viongozi hao. 

“Tumieni vikao vya tawi na kata kuwasilisha ushahidi wenu na pale mtakahisi kuwepo kwa dalili za kuhujumiwa, leteni ushahidi wenu moja kwa moja kwangu ili tuuwasilishe kunakohusika haraka iwezekanavyo,” alisema.

UKAWA Watoa Tamko Zito Lenye Masharti Manne

Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamesema baada ya kufuatilia mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wana taarifa za uhakika kwamba Maalim Seif Sharif Hamad, Mgombea Urais wa Chama cha Wananchi (Cuf) anayeungwa mkono na Umoja huo, ameshinda urais wa Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na viongozi hao jana kwa vyombo vya habari imetoa masharti  manne kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Sharti la kwanza ni kuzitaka mamlaka zinazosimamia Uchaguzi Mkuu huo kuondoa mara moja tangazo la kuufuta Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
 
Sharti la pili ni kumtangaza Seif kuwa ni mshindi halali wa nafasi ya urais na hivyo aapishwe kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sharti la tatu, wametoa  wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati na kulaani kwa nguvu zote kinachofanyika Zanzibar ambako kwa mara nyingine tena demokrasia inataka kuminywa wazi wazi  ili tu kuinusuru CCM isiondoke madarakani kama ambavyo wapiga kura wamekuwa wakiamua. 
 
Aidha sharti la nne ni kwa wananchi wa Zanzibar, “tunapenda kuwahakikishia  kuwa tuko nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kupigania mabadiliko .

Kura  za  Urais
Aidha  wamedai ushindi wa urais umetengenezwa, kwenye taarifa rasmi ya NEC ambayo imetangaza hadharani na kunukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba; wapiga kura walikuwa 15,589,639.
 
Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa 15,193,862 na kati ya hizo zilizoharibika ni 402,248:”Kupitia hesabu hizo hapo juu unaweza kushuhudia upikwaji na utengenezwaji wa matokeo uliofanywa ili kuhujumu matokeo ya Lowassa kwa ajili ya kumbeba na kumpatia ushindi Dk. Magufuli ili kuinusuru CCM.”

Viongozi hao walisema Ili kuthibitisha kauli yao kwamba wameongoza uchaguzi katika nafasi hiyo kwa Lowassa ndiye Rais aliyechaguliwa na Watanzania walio wengi walioshiriki uchaguzi Mkuu Oktoba 25.
 
“Tunazitaka mamlaka zinazohusika, kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu za uchaguzi, zitengue matokeo batili waliyoyatangaza na zimtangaze mara moja Lowassa kuwa ni mshindi wa nafasi ya urais na Duni Juma Haji kuwa Makamu wa Rais,” walisema viongozi hao

Hali ni Tete Zanzibar....Bomu Lategwa Kituo cha Polisi, JWTZ Waliwahi na Kulilipua


Jeshi la Polisi Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ), limefanikiwa kuteguwa bomu lilitegwa eneo la Mkunazini karibu na kituo cha polisi mjini Zanzibar.
 
Bomu hilo lilitegwa na watu wasiofahamika na jeshi la polisi lilipata taarifa ya kutegwa kwa bomu hilo kutoka kwa wasamaria wema.

Akizungumza na mwandishi wetu, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame, alisema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa eneo hilo kuna kitu kimetegeshwa, jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa ni bomu na kufanikiwa kulitegua kwa kuliripua ili kuepusha maafa.
 
“Ni kweli kulikuwa na kishindo kikubwa baada ya jeshi la polisi kuliripua bomu hilo lakini hakuna madhara yoyote yaliotokea,” alisema.

Aidha alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini ni aina gani ya bomu lililotegwa na aliyefanya kitendo hicho.

Friday, October 30, 2015

Lembeli Aeleza Hatma Yake Baada Ya Kushindwa, Ajibu Tetesi Juu Yake

Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.

Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.

Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.

Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa.

Dr. Magufuli Akabidhiwa Rasmi CHETI Cha Ushindi wa Kiti cha Urais

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemkabidhi cheti cha ushindi wa kiti cha urais, Dk John Pombe Magufuli  na  mgombea  mwenza  wake  Samia  Suluhu  katika  Ukumbi wa Diamond Jubilee  asubuhi  hii.

Katika  tukio  hilo, Wagombea urais wa Chadema Edward Lowassa na Hashim Rungwe wa Chauma wamesusia sherehe hizi  za kukabidhiwa cheti cha ushindi Dk John Magufuli wa CCM.

KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET KUISAFIRISHA TIMU YA TAIFA STARS KWENDA ALGERIA

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu ya taifa Taifa Stars kwenda nchini, Algeria kwa mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu.


Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu timu hiyo kwenda nchini Algeria kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedhamini safari hiyo kwa kutoa ndege yake kwa kwenda na kurudi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati na Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie.
 Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kudhamini timu ya Taifa Stars kwenda na kurudi  nchini Algeria kwa ndege yake kushiriki  mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 17  mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Kamati ya Timu ya Taifa Stars, Teddy Mapunda na Mkuu wa Masoko wa Fastjet, Jan Petrie. 
 Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Ndege ya Fastjet imetoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha timu ya Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wake na timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi  Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati alisema hatua ya kuisaidia timu hiyo ni mwanzotu wa ushirikiano baina ya kampuni hiyo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

"Kampuni yetu imeanza ushirikiano na TFF katika kukuza michezo nchini na ndio maana tumeanza kuwasafirisha wachezaji hao kwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo huo" alisema Kibati

Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda alisema safari ya kwenda nchini humo itakuwa Novemba 16 na kuwa mchezo huo utafanyika Novemba 17.

Alisema gharama za kusafiri na timu hiyo kwa mtu atakayependa kusafiri ni dola 800 kati ya hizo dola 640 ni kwa ajili ya safari na 60 ni malipo ya kodi ya uwanja wa ndege hapa nchini na Algeria.

Alisema safari hiyo itaanza asubuhi na kuwa ndege hiyo watakayosafiri nayo inabeba abiria zaidi ya 150.

UN TANZANIA STATEMENT ON TANZANIA GENERAL ELECTIONS

IMG_5569
UN Resident Coordinator, Alvaro Rodriguez.
Dar es Salaam, 29 October 2015: The United Nations is following very closely the Tanzanian general elections of 25 October and congratulates the president elect. We congratulate Tanzanians for exercising their democratic rights in a peaceful manner. We take note of the international observers statement (Commonwealth, AU, SADC and EU) of today that indicates they are pleased that the voting and counting took place in an environment of peace.
However, the observer missions as well as the US Embassy and UK High Commission have also shared their great concern with the statement issued by the Chairman of the Zanzibar Electoral Commission in which he nullified the Zanzibar elections.
We call on political leaders to promote an environment of peaceful dialogue to resolve their differences and to ensure a continued peaceful and democratic elections process. It is through this peaceful and democratic process that the social and economic development of the United Republic of Tanzania can be ensured.
SIGNED BY: ALVARO RODRIGUEZ
UN RESIDENT COORDINATOR

Vyama 6 Yyamtaka Mwenyekiti ZEC Ajiuzulu......Maalim Seif atoa Wito kwa Rais Kikwete Na Dk Shein

Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amemuomba Rais Jakaya Kikwete na Rais Ali Mohamed Shein kubeba dhamana ya uongozi katika siku hizi chache zilizobaki za uongozi wao kwa kusimamia katiba na sheria za nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtendeni Maalim Seif amesema marais hao wawili kuheshimu maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba na kuwataka washirikiane nae katika kuinusuru Zanzibar.

“Nawaomba sana Rais Kikwete na Rais Shein kukwepa matumizi ya nguvu na badala yake tushirikiane kutunza amani na haki za wananchi. Mimi niko tayari kushirikiana nao kama ambavyo nimekuwa nikifanya mara zote. Tushirikiane kuiepushia Zanzibar na Tanzania fedheha ya kimataifa”. Alisema Maalim Seif.

Akizungumzia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi iwapo ni halali au sio halali Maalim Seif amesema lile lilikuwa ni tamko binafsi la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha ambapo Chama Cha Wananchi (CUF) kimetiwa nguvu na tamko la Makamishna wawili wa Tume waliothibitisha kwamba tamko lile ni lake binafsi.

“Ni kwamba hakukuwa na kikao cha Tume kilichokaa kuamua yaliyosemwa na Jecha, na kwamba hakuna misingi ya kikatiba na kisheria ya tamko lile” alisema Maalim Seif na kuongeza kwamba.

“Jana jopo la wanasheria wa CUF lilikutana kuangalia kwa kina kama kuna misingi ya kikatiba na kisheria ya tamko lile binafsi la Jecha Salim Jecha, na limetoa hoja za msingi zifuatazo kwa kuanzia muundo wa Tume ambapo Kifungu 119(1) kinaanzisha Tume ya Uchaguzi yenye wajumbe saba (7) akiwemo Mwenyekiti wao.

Alisema (1) Kifungu 119 (10) kinatamka kuwa: “Kiwango cha mikutano ya Tume ya Uchaguzi ni Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wane na kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na Wajumbe walio wengi”.

Aidha alisema (1) Kwa sababu Tume haikukaa kwa pamoja ikiwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na angalau wajumbe wengine wanne, na kwa sababu maamuzi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume yalikuwa ni yake peke yake, maamuzi hayo kikatiba ni batili na hayana nguvu zozote.

Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF alisema waangalizi wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na SADC, AU, Commonwealth Observer Team, European Union Election Observation Team, Waangalizi kutoka Uingereza na Marekani, na TEMCO, wote walisema mbali na dosari ndogo ndogo uchaguzi ulikuwa huru, wa haki na amani.

Aidha aliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwenyekiti wa ZEC mwenyewe naye pia alisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki ambapo Mwenyekiti huyo huyo alisimamia kazi ya uhakikiwa matokeo na kutia saini fomu za matokeo yaliyohakikiwa na kuthibitishwa za majimbo 31 ya Unguja na kuyatangaza matokeo hayo kabla.

“Kwa nini ghafla ilipofika siku ya tatu ambayo ni jana aligeuka na kukataa kuendelea na uhakiki na badala yake kudai eti kulikuwa na mambo kadhaa ya kufanya uchaguzi huo usiwe huru na wa haki? Tena dosari zenyewe za tamko lake eti ni pamoja na wajumbe wake kuvua mashati na kutaka kupigana” alisema Maalim.

Akizungumzia suala la baraza la Wawakilishi jipya Maalim Seif alisema Kifungu 92(1) cha Katiba ya Zanzibar kinaeleza kwamba maisha ya Baraza la Wawakilishi ni miaka mitano tokea lilipoitishwa mkutano wake wa mwanzo hivyo Kifungu 90(1) kinaeleza kwamba mkutano wa mwanzo wa Baraza la Wawakilishi utafanyika si zaidi ya siku 90 tokea Baraza lilipovunjwa kwa ajili ya kuitishwa uchaguzi.

Kuna masuali kadhaa ya kujiuliza alisema Maalim Seif ikiwemo ni “Rais yupi ataitisha Baraza?, Wawakilishi wapi wataitwa (wakati hawapo)?, Yote haya yanaleta mgogogro wa kikatiba ambao umesababishwa na mtu mmoja anayeitwa Jecha Salim Jecha kwa sababu tu ya kufuata maelekezo ya chama chake cha CCM”. Alihoji Maalim Seif huku akionekana kuongea kwa kujiamini.

Hata hivyo alisema kuna suali la muundo wa mpito ambapo kama uchaguzi utarejewa, kama anavyotaka Mwenyekiti wa Tume, jambo ambalo alisema halikubaliki kwa sababu ya kukosa misingi ya kikatiba na kisheria, ina maana kuwa serikali itakuwa haipo.

Akitoa sababu za kutokuwepo Maalim Seif alisema kwanza muda wa Urais ni miaka mitano kuanzia tarehe aliyochaguliwa kwa mujibu wa kifungu 28(2) cha Katiba, Ingekuwa tamko la Jecha Salim Jecha ni halali, basi maana yake hakuna Rais anayefuata kwa sababu ya kufutwa kwa uchaguzi, hivyo hakutakuwa na kiapo cha kumuapisha rais mpya. Kwa msingi huo, msharti ya kifungu cha 28(1)(a) hayana nafasi katika mtafaruku huu uliosababishwa na mtu mmoja.

“Hiyo maana yake, kipindi hicho sasa kitakuwa tete na haijulikani kikatiba ni nani ataongoza nchi? Tunasema hivyo kwa sababu vifungu vya Katiba 33(1) na (2) havitumiki hapa kwa suala la kuwa wazi kwa kiti cha Urais na kukaimiwa kwa nafasi hiyo”. Aliongeza.

Alisema hiyo ni kwa sababu nafasi ya Urais haipo kwa sababu itakuwa imemaliza muda wake ifikapo tarehe 2 Novemba, 2015, siku ambayo Urais wa Dk. Ali Mohamed Shein unakamilisha miaka mitano kamili.

Halikadhalika Maalim Seif alitaka kujua jee katika suala hilo suluhisho ni nini? “Kutokana na hoja tulizozieleza hapo juu, ni wazi kwamba tamko la Jecha Salim Jecha ni lake binafsi na kama tulivyotangulia kusema, halina misingi ya kikatiba na kisheria.  
 
Kwenye taarifa yake alisema kuwa “… kwa uwezo nilionao …”. Masuala ya kujiuliza ni uwezo upi? Chini ya kifungu kipi cha Katiba au Sheria ya Uchaguzi?” alihoji.

Katika kutilia nguvu hoja yake hiyo ya kisheria Maalim Seif alisema kwa kifupi, ni kwamba Mwenyekiti wa ZEC uwezo huo hana kikatiba na kisheria na kwa msingi huo, maamuzi yake hayo ni batili.

Kufuatilia masuali hayo ambayo majibu yake yapo kisheria Maalim Seif alisema CUF inasisitiza kile kinachodaiwa na waangalizi wote wa uchaguzi waliotoa taarifa zao kwamba uamuzi wa Mwenyekiti wa ZEC ni uamuzi wake binafsi pekee na haukuwa uamuzi wa Tume, kwani hakukuwa na kikao chochote cha Tume kilichokaa kufikia uamuzi huo.

Alisema uamuzi huo uwekwe upande na Jecha Salim Jecha amepoteza sifa ya uadilifu ambayo ni msingi mkuu wa kazi ya Tume ya Uchaguzi katika kusimamia maamuzi ya Wazanzibari ambao kikatiba (kwa mujibu wa kifungu cha 9(2) (a) ndiyo wenye mamlaka ya kuwaweka madarakani viongozi wa Serikali.

“Hivyo, anapaswa awajibike kwa hatua yake ya kuiingiza nchi katika mgogoro pasina sababu yoyote na ajiuzulu” alisema Maalim Seif huku akionekana na furaha katika mkutano huo wa waandishi wa habari.

Aidha alishauri Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar waendelee na kazi ya kukamilisha uhakiki na majumuisho ya matokeo ya uchaguzi kwa majimbo 14 yaliyobaki na kisha kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Zazibar.

Alisema baada ya ukamilishaji huo alisema mshindi wa nafasi ya Urais wa Zanzibar aapishwe, Viongozi wa CUF na CCM washirikiane kuunda Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa itakayoiongoza Zanzibar katika miaka mitano ijayo.

“Kwa maana hiyo, kitumike kifungu 42(6) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoeleza kwamba kama kuna matatizo yoyote katika vituo vya kupigia kura a na matokeo hayawezi kutolewa ndani ya siku tatu; basi Tume iendelee kuhesabu na kuhakiki kura na kutangaza matokeo ndani ya siku tatu nyengine na shughuli za kiserikali ziweze kuendelea” aliongeza.

Katika hatua nyengine Malaim Seif alirejea tena kauli yake ya kuhimiza Amani na kuwataka wafuasi wake na wananchama wa CUF na Wazanzibari wote kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu na kutunza amani ya nchi yetu huku wakitambua kwamba tutayasimamia maamuzi yao waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.
Baadhi ya wafuasi wa CUF wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi za CUF Mtendeni kusikiliza kauli za viongozi wao kuhusu maamuzi watakayochukua baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi

Rais Kikwete Alivyomkaribisha Kumpongeza Dk. Magufuli Baada ya Matokeo ya Urais Kutangazwa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakifurahia matokeo mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni  jana  jioni Oktoba 29, 2015


Mama Salma Kikwete akimpongeza mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tais kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jana jioni Oktoba 29, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jana jioni Oktoba 29, 2015


Mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea salamu za pongezi kutoka kwa mgombea Urais Mwanamke Pekee kwa tiketi ya ACT Wazlendo Mama Anna Mghira mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni. Dkt Magufuli amemshukur sana Mama Mghwira na kumwita mkomavu wa siasa na mwana-Demokrasia wa mfano jana jioni Oktoba 29, 2015

Mambo Yaliyombeba Dr. Magufuli Kushinda Urais Wa Tanzania

Tanzania  imeandika historia mpya, ambapo jana imempata Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli, ambaye alikuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu uliohitimishwa Jumapili ya Oktoba 25, mwaka huu.

Dk Magufuli ambaye katika kampeni ya kuwania urais alikuwa na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu, si mgeni katika safu za uongozi wa Tanzania kwa kuwa amekuwa serikalini kwa miaka 20, akishika majukumu mbalimbali ambayo yalitumiwa na Watanzania kumpima.

Moja ya sifa yake kubwa tangu alipotangaza nia ya kugombea urais kupitia chama hicho mwishoni mwa Mei mwaka huu, ni uadilifu katika utendaji kazi wake katika majukumu tofauti aliyokabidhiwa Rais huyo mteule wa Awamu ya Tano, anatajwa kuwa katika majukumu yote ya kitaifa aliyowahi kukabidhiwa, alionesha sifa ya juu ya uaminifu na uadilifu, ambao umeelezwa kwa namna mbili tofauti.

Ujenzi barabara 
Kwanza ni uongozi wake wa miradi mikubwa ya fedha nyingi, ambayo kwa muda wote wa uongozi wake hakuwahi kukumbwa na kashfa. Kwa mfano mwaka huu tu, alikuwa akiongoza Wizara ya Ujenzi, iliyokuwa na bajeti ya Sh trilioni 1.2 na Mfuko wa Barabara uliokabidhiwa zaidi ya Sh bilioni 866.

Katika miaka 15 aliyoongoza Wizara hiyo ya Ujenzi, katika ngazi hiyo alisimamia miradi ya zaidi ya Sh trilioni 9.5, lakini hakula hata senti tano, badala yake alijenga mtandao mrefu wa barabara za lami nchi nzima.
 
 Usimamizi 
Namna ya pili ya kuzungumzia uadilifu wake ni usimamizi wake wa watendaji na wadau wa sekta ya ujenzi, ambao amekuwa akiwapa kazi za mabilioni ya shilingi na kuisimamia kwa karibu katika kuwatumikia Watanzania.

Dk Magufuli amekuwa akisimamia makandarasi zaidi ya 8,500, wahandisi zaidi ya 15,000 na wakadiriaji majengo zaidi ya 1,300, ambao wamekuwa wakinufaika na kazi za Serikali za mabilioni ya shilingi.

Kama angetumia vibaya nafasi hiyo na angetaka kumuomba au kushinikiza kila mmoja wao ampe Sh milioni moja tu kwa mwaka, angeweza kujikusanyia pato binafsi lisilo halali la zaidi ya Sh bilioni 100 kila mwaka. Pamoja na kuwa karibu na kishawishi hicho, lakini Dk Magufuli hakushiriki kuhujumu hata senti moja na hana historia wala hakuwahi kutajwa popote kutumia vibaya nafasi yake hiyo katika sekta yenye maslahi makubwa ya kifedha.

Ukali kwa wazembe 
Badala ya kuomba michango ya kujinufaisha kutoka kwa wadau hao wa ujenzi, Dk Magufuli alijikuta akifukuza kazi makandarasi zaidi ya 3,000 wa ndani na nje ya nchi, bila kujali utajiri wao, pale makandarasi hao walipozembea kazi au kufanya kazi chini ya kiwango.

Namna ya tatu inayotumika kuelezea uadilifu wa Dk Magufuli, imeelezwa mara kadhaa na Jaji Joseph Warioba, ambapo alisema mwaka 1996 alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuongoza Tume ya Kero za Rushwa, alikuta sekta ya ujenzi ikinuka rushwa kubwa. Lakini, anafafanua kuwa baada ya Dk Magufuli kuanza kufanya kazi katika sekta hiyo, kelele ya rushwa katika sekta hiyo imetoweka. Uchapakazi Mbali na uadilifu, Dk Magufuli pia anatajwa kuwa mchapakazi.

Hata Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi mara kadhaa amempa jina la ‘simba wa kazi’, huku Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake, akimpa jina la ‘tingatinga’ ambalo huwa halishindwi kazi katika mazingira yoyote ya ujenzi, huku wananchi wengine wakimuita ‘jembe’. Matokeo ya uchapakazi wake, yanaonekana katika sekta ya ujenzi, alikofanya kazi kwa miaka 15 tu, ambapo amefanikiwa kusimamia ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa 17,700.

Kazi hiyo imeweka historia ambayo hata wakoloni, Wajerumani na Waingereza, waliotawala Tanganyika wakati huo tangu mwaka 1884/1885 mpaka wakati wa Uhuru mwaka 1961, zaidi ya miaka 75 walijenga mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 1,360 tu. 
 
Wasifu wake
Dk Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 Chato (sasa Mkoa wa Geita), hivyo jana alipotangazwa kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ambapo alitimiza miaka 56.

Dk Magufuli ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 1991 – 1994 alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza. Mwaka 1985 – 1988 alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1981 – 1982 alisoma Diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Kati ya mwaka 1979 – 1981 alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Juu ya Sekondari Mkwawa, Iringa. Mwaka 1977 – 1978 alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza. Mwaka 1975 – 1977 alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera. Mwaka 1967 – 1974 alisoma Shule ya Msingi, Chato. Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mpwapwa mkoani Dodoma.

Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha. Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma. 
 
Uzoefu wa kazi 
Kuanzia mwaka 2010 alikuwa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato. Mwaka 2008 – 2010 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato). Mwaka 2005 – 2008 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).

Mwaka 2000 – 2005 Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1995 – 2000 Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1989 – 1995 Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Co-operative Union (Ltd) Mwanza. Mwaka 1982 – 1983 Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati). Amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa. Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.
 
 Mchakato wa urais 
Dk Magufuli alitangaza rasmi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa Mei mwaka huu, baada ya CCM kutangaza rasmi ratiba ya mchakato wa urais kwa wanachama wake. Aliingia kwenye harakati za kuwania nafasi ya urais kimya kimya, tofauti na makada wengine wa CCM ambao walihutubia Taifa.

Lakini, kimya chake kiliufanya mchuano wa uchaguzi wa nafasi hiyo ndani ya CCM, uliokuwa na wagombea 42 kuwa mkali zaidi. Baada ya hapo, waliorejesha fomu walikuwa wagombea 38 na kati ya hao baada ya kujadiliwa na vikao vya juu vya Chama, ikiwemo Kamati Kuu, wagombea watano - Dk Magufuli, Bernard Membe, Dk Asha Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ally na January Makamba, ndio waliofanikiwa kupelekwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.

Baada ya Nec, ambako wagombea hao walijadiliwa na kupigiwa kura, Dk Magufuli, Balozi Amina na Dk Migiro ndio waliofanikiwa kuingia tatu bora, ambapo walifikishwa katika Mkutano Mkuu na kuomba kura na baada ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano huo, akapatikana Dk Magufuli kupeperusha bendera ya CCM.
 
 Ahadi zake Dk
 Magufuli katika mikutano yake ya kampeni, alikuwa akiahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi aliosema atapigania kila mmoja awe na kazi ya kumpa kipato, wajenge nyumba bora.

Katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, Serikali yake itatoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake na vijana. Mbali na kutoa mikopo hiyo izunguke katika ngazi ya kijiji na mtaa, Dk Magufuli pia alisema Serikali yake itazuia kila aina ya usumbufu, unaofanywa kwa wafanyabiashara hao, ikiwemo kukamatwa kwa bodaboda na mama ntilie.

Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao kwa kuwa atahakikisha mbali na wakulima kupata bei nzuri ya mazao yao, watakapoiuzia Serikali itakuwa bidhaa kwa fedha taslimu. 
 
Aidha, aliahidi kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara wadogo na wakulima, ili wafanye biashara kwa uhuru wajipatie kipato halali.

Dk Magufuli pia alisema baada ya kusambaza umeme, atahakikisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vinajengwa vijijini ili kusindika mazao ya kilimo shambani ili kutoka shambani bidhaa za mazao hayo ziuzwe katika masoko ya ndani na nje ya nchi. 
 
Kuhusu migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, Dk Magufuli aliahidi kukabiliana na migogoro hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa ardhi zaidi kwaajili ya wakulima na wafugaji, ili kuondoa uhaba wa ardhi uliosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia mifugo na kulima.

Lakini pia aliahidi kunyang’anya mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo. 
 
Katika elimu, alikuwa akiahidi kuhakikisha kuanzia mwakani, wanafunzi kutoka darasa la awali mpaka kidato cha nne, wanasoma bila kulipa ada, ili kuondolea wazazi usumbufu wa watoto wao kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada.

Kwa wanafunzi wa elimu ya juu, aliwahakikishia kuwa hakutakuwa na usumbufu wa kupata mikopo na kuwataka wanahusika na kazi hiyo, kuwa tayari kwa kuwa atataka kila mwenye sifa ya kusoma elimu ya juu, apate mkopo.
 
 Katika sekta ya afya, aliahidi kujenga zahanati kwa kila kijiji na mtaa, kituo cha afya kwa kila kata na hospitali ya rufaa katika kila mkoa, na ameahidi kukomesha kero ya kukosekana dawa katika hospitali za Serikali.

Katika kero ya maji, alikuwa akisema kama amefanikiwa kujenga zaidi ya kilometa 17,700 za barabara ya lami, hatashindwa kujenga mabwawa na mtandao wa mabomba kwenda kwa wananchi ili kukomesha kero hiyo.

Pia aliahidi kujenga barabara mbalimbali za lami za kuunganisha wilaya na za mijini, huku akiahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi, ifanane na ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), taasisi aliyoianzisha na kuitetea, ambayo leo watu wengi wanatamani kuitumikia kutokana na maslahi mazuri na mafanikio yake.

Thursday, October 29, 2015

Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania pamoja na Ireland Kaskazini Wapinga Uchaguzi Mkuu Kufutwa Zanzibar


Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania pamoja na Ireland Kaskazini umetoa taarifa ukipinga kufutiliwa mbali kwa matokeo ya Uchaguzi kisiwani Zanzibar.
 
Ubalozi huo umesema kuwa hauoni sababu za kufutiliwa mbali kwa matokeo hayo ilhali waangalizi walifurahishwa na vile uchaguzi huo ulivyofanyika kwa amani.
 
Wameitaka tume ya uchaguzi Kiswani Zanzibar kuorodhesha matokeo hayo bila kuchelewa.
----------------------------
PRESS STATEMENT
Thursday 29 October, 2015

United Kingdom statement on Zanzibar elections

The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland is deeply concerned by the announcement of the Chairman of the Zanzibar Electoral Commission to nullify the elections. We note that all the international observers were impressed by the quality of the electoral process they witnessed. We call on ZEC to resume the results tabulation process without delay.

We congratulate the people of United Republic of Tanzania on the peaceful and enthusiastic way in which they participated in their elections.We call on all political actors to seek a solution which respects the will of the Zanzibari people as expressed in the polls on 25 October.

The United Republic of Tanzania has a well deserved reputation for peace and stability and respecting democratic principles. We urge all Zanzibaris to maintain peace and we commend the restraint they have shown so far

Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais


Watanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Tumeainisha kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.

• Upunguzwaji wa kura zangu
• Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
•Tunaendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.

Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani

Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.
 
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.

Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.

Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015

Breaking News: Dr John Pombe Magufuli Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania kwa Asilimia 58.46


Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva   imemtangaza  Rasmi  mgombea  Urais  wa  CCM, Dr John Pombe  Magufuli  kuwa  mshindi  halali  wa  kiti  cha  Urais  katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.  

Kwa  Mujibu  wa  jaji  Lubuva, Dr  magufuli  amepata  ushindi  wa  kura Milioni 8 ( 8,882,935  ) sawa  na  asilimia  58.46%  huku  akimwacha  kwa  mbali  mpinzani  wake  wa  karibu , Edward  Lowassa (Chadema )  ambaye  amepata  jumla  ya  kura  Milioni 6 (  6,077,848  )  sawa  na  asilimia  39.97%
Dr  Magufuli  na  mgombea  mwenza, Samia Suluhu  watakabidhiwa  rasmi  vyetu  vya  ushindi  kesho  saa  nne  asubuhi  katika  ukumbi  wa  hoteli  ya  Diamond  Jubilee  

TULINDE AMANI TUNAPOENDELEA KUPOKEA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU


Ndugu watanzania wenzetu, tunapenda kuwapongeza kwa kumaliza mchakato wa kampeni za vyama vya siasa na wagombea  kwa amani na utulivu. 

Vile vile tunawapongeza kwa kupiga kura kwa kwa amani na utulivu, kwani pamoja na kujitokeza kwa wingi tulipiga kura kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ukiachilia mbali kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo. 

Ndugu watanzania wenzetu,  tangu juzi jumapili 25 Oktoba tulianza kupokea matokeo. 

Hiyo ni hatua muhimu sana kwa taifa letu, demokrasia yetu na amani ya nchi yetu. Wote tutakubaliana kwamba nchi nyingi za kiafrika zimeingia katika machafuko ya kisiasa na kuvuruga amani ya nchi hizo katika kipindi cha kupokea matokeo.
Nchi za Ivory Cost iliingia katika mgogoro wa kisiasa kwa wakati wa kupokea matokeo, ikaingia katika mapigano  ya wenyewe kwa wenyewe maelfu ya wananchi walipoteza maisha, wengine wakijeruhiwa vibaya na wengi wakiyakimbia makazi yao. 

Mwaka 2007, Nchi jirani ya kenya nayo ilingia katika mgogoro wa kupokea matokeo na hivyo kusababisha machafuko, watu zaidi ya elfu moja walipoteza maisha, wengi wakiachwa walemavu na maelfu wakiyakimbia makazi yao.
Sisi Global Peace Foundation Tanzania, tunaona mwenendo wa kupokea matokeo ukianza kuingia dosari, kwa baadhi ya wagombea na wafuasi wa wagombea kujitangazia matokeo.

 Ambao kwa Mujibu ka sheria ya uchaguzi ni kinyume, ni kuvunja kanuni kwani chombo chenye dhamana ya kutangaza matokeo ni Tume ya Taifa ya uchaguzi pekee.
Kwa sababu hiyo, tumeona tuwakumbushe wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa kuwa wakati huu wanapaswa kuwa watulivu na waangalifu pindi wanapotoa matamko. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamewasaidia wafuasi wao kuwa watulivu na hatimaye kutuvusha katika hatua hii tukiwa na amani na utulivu. 

Tunaisihi tume ya uchaguzi ya Taifa NEC, na ile ya Zanzibar ZEC, kuharakisha mchakato wa kutangaza matokeo pindi yanapopatikana na kujumlishwa ili kuepusha minong'ono na hisia hasi zinazoweza kupandikizwa kwa wapiga kura na wananchi na baadaye kusababisha machafuko. 

Tunakiri kuwa pamoja na kuwapo migogoro ya hapa na pale, kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani katika baadhi ya maeneo kama huko Unguja Zanzibar, baadhi ya maeneo ya Mbeya, Dar es Salaam na Lindi. 

Bado jeshi la polisi limeendelea kufanya kazi zake kwa weledi. Hata hivyo tunakisii chombo hicho kuwa waangalifu zaidi katika kipindi hiki adhimu kwani matumizi ya nguvu zilizopitiliza yanaweza kuchochea uvunjifu wa amani. 

Tunawakumbusha watanzania wenzetu mashabiki wa vyama vya siasa , wapiga kura na vyama vya siasa wajiandae kupokea matokeo ya aina yeyote. kwani misingi ya kidemokrasia inatutaka kuchagua na yule aliyepata kura nyingi ndiyo anakuwa mshindi. 

Na mwisho ni kwa wanahabari na vyombo vya habari nyie mnabeba dhamana kubwa kwa taifa hili katika wakati huu muhimu kwa taifa letu. 

Namna mtakavyotoa taarifa kwa watanzania ndiyo itakayo amua mustakabali wa amani na utulivu wa taifa hili. 

Mnalo jukumu na wajibu mahususi katika kuhakikisha kuwa nchi hii inabaki salama, inabaki na umoja na mshikamano, inabaki na utulivu. 

Toeni habari kwa kulingana na matakwa ya taaluma yenu muhimu.
Waswahili husema, sindano ya daktari huponya na kuua na kalamu ya mwandishi hujenga ama kubomoa. Kama ilivyo daktari mwema, mwenye maadili huchagua kuponya na mwandishi makini atachagua kujenga jamii yenye amani, utulivu na mshikamano kwa kutambua kuwa bila amani hakuna maendeleo. 


Tunasimamia msemo wa watanzania uliopata umaarufu katika wakati huu wa uchaguzi kuwa KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI . Asanteni, Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania

Tafadhali bonyeza hapa chini kusikiliza wimbo maalumu wa kuhamasisha Amani ulioimbwa na Barnaba Boy 

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More