waziri wa ardhi na makazi WILIAMU LUKUVI ambaye ni mbunge wa jimbo la Ismani na Mkurugenzi Msaidizi wa USAID
Tanzania, David Thompson alisema USAID wakikabdhi hati za kimila kwa wananchi wa kijiji cha kinywang'anga mkoani iringa
na fredy mgunda,Iringa
Wizara ya ardhi nyumba na
maendeleo ya makazi imetoa jumla ya hati za kimila 810 kwa wananchi wa kijiji
cha kinywang’anga kilichopo tarafa ya ismani mkoani Iringa ili kupunguza
migogoro ya ardhi,hati hizo zinazotolewa kupitia Mradi wa Urasimishaji Ardhi
(LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la
Misaada la Marekani (USAID). .
Akizungumza na wananchi wa
kijiji cha kinywang’anga waziri wa ardhi na makazi WILIAMU LUKUVI ambaye ni mbunge wa jimbo la Ismani alisema
kuwa mpango huu wa kurasimisha ardhi kimila utakuwa na faida kubwa kwa wananchi
na kukuza dhamani ya ardhi zao.
Akikabidhi hati hizo, Waziri
Lukuvi aliupongeza mpango huo akisema utasaidia kupunguza eneo kubwa la ardhi
ya Tanzania ambayo haijapimwa.
“Ni asilimia 15 tu ya ardhi
yetu nchini imepimwa, kuna vipande vya ardhi zaidi ya milioni 12 vinatakiwa
kupimwa lakini hadi sasa vilivyopimwa ni kama 400,000 hivi,” alisema.
Akiwapigia magoti USAID,
Lukuvi aliwaomba wautanue mradi huo angalau ufike katika mikoa 10 huku
akizikumbusha halmashauri nchini kote kila mwaka kuvitengenezea vijiji vitano
hadi 10 mpango wa matumizi bora ya ardhi.
“Tunataka katika kipindi cha
miaka 10 kutoka sasa ardhi yote ya Tanzania iwe na mipango ya matumizi bora na
ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema.
Wakati mipango hiyo
ikiendelea, waziri huyo alisema sera ya ardhi ya mwaka 1995 imefanyiwa
marekebisho makubwa yatakayoleta sera mpya ya mwaka 2017.
Alisema kwa kupitia sera
hiyo, kutakuwa na usimamizi zaidi wa ulinzi wa ardhi ya watu masikini ili
kupunguza uporaji wa rasilimali hiyo unaofanywa na matajiri.
“Marekebisho ya sera hiyo ya
ardhi yatawezesha pia kufanyika kwa mrekebisho ya sheria mbalimbali za ardhi
ili ziendane na sera na mazingira ya sasa,” alisema.
Aliwataka wananchi
wanaondelea kupata hati miliki za kimila za ardhi kuzitumia kupata mikopo kutoka
katika taasisi mbalimbali za fedha ili kuchochea maendeleo yao badala ya
kusubiri pembejeo za ruzuku.
Mkurugenzi Msaidizi wa USAID
Tanzania, David Thompson alisema USAID inafadhili mpango huo ili kuisaidia
Tanzania kuwa na mfumo mzuri na wazi wa kulinda haki ya kumiliki ardhi kwa raia
wote, wanaume na wanawake.
“Usajili wa ardhi ni muhimu
kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza
thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema.
Thompson alisema
Kinywang’anga ni moja kati ya vijiji 41 vya mikoa ya Iringa na Mbeya
vitakavyonufaika na mradi huo wa miaka minne utakaopima na kutoa hati miliki za
kimila zaidi ya 70,000 kwa wananchi wa vijiji hivyo.
Awali Meneja Msaidizi wa
LTA, Malaki Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango
ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati miliki
za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani Mbeya.
“Bada ya kukamilisha zoezi
la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji chote cha Kinywang’anga, hivi
sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika vijiji vya Kiponzero, Magunga
na Usengelindete wilayani Iringa.”
MSIGWA aliongeza kuwa lengo
la mradi ni kuhakikisha wanapunguza migogoro ya ardhi kwa wananchi wa vijijini.
Nao wananchi wa kijiji cha
kinywang’anga waliwashukuru wafadhili pamoja na wizara ya ardhi na makzi kwa
kuwasaidia kupata hati ambazo zitakuwa na faida nyingi kwao.
0 comments:
Post a Comment