Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amemkumbusha Spika wa Bunge.
Job Ndugai, kuhusu kusudio lake la kuanza kuwapima wabunge kubaini kama
wametumia kilevi kabla hawajaiingia kwenye ukumbi wa chombo hicho cha
kutunga sheria.
Siku
chache baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Charles Kitwanga,
kwenye baraza lake la mawaziri kutokana na kuingia bungeni akiwa
amelewa, Ndugai alisema kuwa kuna wabunge kadhaa huingia bungeni wakiwa
wametumia vilevi vikali zaidi vikiwemo bangi, viroba na unga’
Aidha
kutokana ba hatua hiyo, Spika huyo alisema wanafikiria kuweka vifaa
maalumu vya kupima ulevi kwa watunga sheria hao na kutafuta wataalamu wa
kutoa ushauri nasaha wa kisaikolojia, utaratibu huo haujaanza kutolewa
bungeni licha ya kwamba ni miezi tisa ipite,
Jana
katika hafla maalum ya kukabidhi orodha mpya ya watuhumiwa wa biashara
haramu ya madawa ya kulevya Kumkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Kupambana na Kuzui Dwa za Kulevya, Rogers Siang’a, Makonda alimkumbusha
Spika Ndugai kusudio lake la kuanzisha utaratibu wa kuwapima wabunge
ulevi.
“Na
utaratibu huu wa kuwapima wabunge wetu utakuwa mzuri sana, na
ninakumbuka kuna kipindi Spika aliwahi kutangaza kuanzisha lakini sijui
ukaishia wapi, nitoe tena rai kwake afikirie tena kuanzisha utaratibu
huu ili tuweze kuwabaini wabunge kama wanatumia kilevi ama la,”alisema Makonda.
0 comments:
Post a Comment