Mkuu
wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Mhe Alexzender Mnyeti akisaini kitabu cha maombolezo kijijini
Misasi
Dc Mnyeti, MD Kayombo na familia nzima ya Mzee Kayombo walipotembelea kaburi la Mzee Kayombo
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Alexzender Mnyeti (Kushoto), na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakiwa katika mazungumzo
Dc Mnyeti akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mzee Kayombo
Wakati wa sala kwenye kaburi la Marehemu Mzee Kayombo
Maombi ni muhimu katika kila jambo
Mazungumzo na Ndegu, jamaa na rafiki
Na Mathias
Canal, Mwanza
Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Mhe Alexzender Pastory Mnyeti amezuru kijiji cha
Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kutoa pole kwa familia ya Marehemu
Mzee Kayombo aliyefariki Dunia siku ya saa mbili usiku katika Hospitali ya
Rufaa Bugando, Mkoani Mwanza.
Mhe Mnyeti
ametoa salamu za pole kwa wakazi wa Kijiji cha Misasi kwa kumpoteza mshauri katika
kijiji hicho ambaye amekuwa nguzo kwa maendeleo ya kijiji sawia na utaratibu
wake wa kuhamasisha wananchi kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi.
Mnyeti
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya
Misungwi kabla ya uteuzi wake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameeleza jinsi
alivyomfahamu Mzee Kayombo katika kuhakikisha jamii inasonga mbele katika
maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Mnyeti alisema kuwa Mkoa wa Mwanza umepoteza
mtu muhimu ambaye pia atakumbukwa kwa kazi njema alizozifanya wakati wa uhai
wake.
Dc Mnyeti ametoa pole kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo Ndugu John Lipesi Kayombo kwa kuondokewa na Mzee wake
ambaye ni Mlezi wake tangu akiwa mdogo sambamba na kuisihi familia ya Marehemu
Mzee Kayombo kuendeleza mshikamano na kupendana.
Marehemu
Mzee Kayombo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya wakati wa uhai wake
pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika shule zote
alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati huo, pia atakumbukwa kwa kuhamasisha
ujenzi wa Zahanati ya Misasi.
Marehemu
Mzee Antony Raphael Kayombo alifariki saa mbili usiku, siku ya Jumamosi ambapo
hadi mauti inamkuta alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao
ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospitali ya Misasi, Baadae
hospitaliti ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa
upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti
ilipomkuta.
INNALILAH WAINNAH ILAIHI RAJIUN
0 comments:
Post a Comment