Zoezi la upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani linalofanyika kwa siku tangu kuanzia jana, linaendelea katika viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela.
Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) amebainisha kwamba jana zaidi ya wananchi 150 walijitokeza kupima afya zao ambapo zaidi ya 70 walihudumiwa na kurejea nyumba.
Alisema zoezi hilo limejikita kwenye uchunguzi wa afya ya uzazi, kisukari, presha pamoja na uzito likiongozwa na wataalamu wa afya kutoka Canada wanaosaidizana na wataalamu wazawa.
#BMGHabari
Umati wa akina mama waliojitokeza kwenye zoezi la upimaji afya bure katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya
Zoezi la kuchukua taarifa likiendelea kwa umakini
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana na linasimamiwa na wataalamu wa afya kutoka Canada
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Kwa wale watakaobainika kuwa katika hali ya uchunguzi zaidi watasaidiwa kufikishwa kwenye hospitali za rufaa ili kuhudumiwa.
0 comments:
Post a Comment