Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited, Bakari Machumu (wa kwanza kushoto) vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) na Nahodha wa timu ya Mwananchi Communication Limited ambaye ni bingwa mtetezi Majuto Omary (wa pili kulia).
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) akimkabidhi Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communication Limited, Bakari Machumu (wa kwanza kushoto) vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa kwanza kulia) pamoja na kwa Nahodha wa timu ya Mwananchi Communication Limited, Majuto Omar (wa pili kulia) wakati wa halfa fupi ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa kwanza kushoto) akimkabidhi Nahodha wa timu ya Mwananchi Communication Limited, Majuto Omar ( kulia) seti ya jezi kwenye hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (katikati).
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa pili kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya Coca cola, Samuel Mwakatumbula wa pili kutoka (wa pili kushoto) kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa kwanza kushoto), Simon Masanja mchezaji wa timu ya Coca cola (wa kwanza kulia) na Salehe Omar mchezaji wa timu ya Coca cola (katikati).
Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wachezaji wa timu ya Coca cola, Simon Masanja (kulia) vifaa hivyo vya michezo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi hii jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (wa pili kulia), Mwenyekiti wa timu ya Coca cola, Samuel Mwakatumbula wa pili kutoka (wa pili kushoto) na Salehe Omar mchezaji wa timu ya Coca cola (katikati).
Na Mwandishi wetu,
Benki kongwe nchini Standard Chartered imekabidhi vifaa kwa timu za Mwananchi Communication Limited na Coca cola kwa ajili ya mashindano ya ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anified) yaliyopangwa kufanyika Jumamosi, kwenye viwanja vya JMK Park Kidongo Chekundu.
Mbali ya kutafuta washindi wa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Afrika Mashariki, mashindano hayo pia ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo vya michezo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba amesema jumla ya timu 32 kutoka mashirika mbalimbali yanatashiriki katika mashindano hayo.
“Tunatarajia timu 32 kushiriki hapa nchini na mshindi ataweza kuingia kwenye fainali ya Kanda ya Afrika Mashariki itakayoshirikisha timu moja moja kutoka Keny na Uganda, ambapo mshindi, atakwenda Liverpool kuangalia moja ya mechi za ligi kuu ya Uingereza ya Liverpool na vile vile kushindana katika mashindano mengine yatakayoshirikisha timu kutoka mabara ,” alisema Mramba.
Mbali ya mashindano, mshindi pia atapata mafunzo ya siku tatu kujifunza mambo ya soka na kutoka kwa magwiji wa mashindano hayo.
Mramba amesema kwamba benki hiyo ya Standard Chartered ilianzishwa mwaka 1917 na mwaka huu inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na imetenga zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 100 kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kutimiza umri huo kwenye sekta ya kifedha.
Wakati huo huo mmoja wa wachezaji waliowika miaka ya themanini na tisini wa timu ya Liverpool, John Barnes atawasili nchini mwanzoni mwa mwezi Machi tayari kwa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 yatakayohusisha timu za makampuni katika eneo hili la Afrika Mashariki.
Uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, yenye kauli mbiu “barabara ya kuelekea Anfield” inatarajiwa kutimua vumbi kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo timu mbili za wachezaji watano watano zitacheza kwa dakika kumi na mshindi atapewa zawadi.
Mashindano hayo ya Standard Chartered yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi hii kwenye viwanja vya JK Youth Park.
Yakiwa katika mwaka wake wa sita, mashindano ya Kombe la Sndard Chartered yamekuwa yakiimarika mwaka hata mwaka na kutoa washindi kutoka pande zote za dunia. Mataifa ambayo yamenyakua kombe hilo ni pamoja na Kenya (2016), Korea Kusini (2015) Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore (2012).
0 comments:
Post a Comment