Bi Mili Rughani, gwiji katika anga la teknolojia Afrika, akabidhiwa kijiti cha uongozi wa tovuti namba moja ya matangazo Tanzania, ZoomTanzania.com, katika kuendeleza safari ya mafanikio.
Miaka ya hivi karibuni imekuwa ya kusisimua sana kwa hii kampuni ya dot-com ya Kitanzania. Mnamo Septemba 2014, Ringier Afrika ilichukuwa asilimia kubwa ya umiliki wa kampuni ya Zoom Tanzania.
Hii iliwezesha upatikanaji wa rasilimali na utaalamu unaohitajika zaidi ili kukua zaidi. Kisha mwaka 2016, ZoomTanzania.com ilikuwa jiwe kuu la msingi katika muungano wa Ringier Africa na One Africa
Media, na kufanikisha kuundwa kwa kundi linaloongoza kwa matangazo ya mtandaoni barani Afrika - Ringier One Africa Media (ROAM).
"Imekuwa ni safari ya kusisimua sana," alisema Kirk Gillis, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa ZoomTanzania. "Miaka michache iliyopita Zoom ilikuwa na wafanyakazi wanne, katika ofisi ndogo ikiwa na ndoto kubwa huku ikiangaika kuweza kufanya malipo ya wafanyakazi."
Leo hii, ZoomTanzania ni tovuti namba moja ya matangazo nchini Tanzania na ina wafanyakazi 35 wengi wao wakiwa ni vijana wachapakazi mahodari, wenye vipaji na wataalamu wakuendesha hili gurudumu la matangazo ya mtandaoni kisasa zaidi.
ZoomTanzania imeshuhudia ukuaji na utendaji mkubwa na wenye kuvutia sana. Kwa mujibu wa wataalamu wa Google,
ZoomTanzania inapata zaidi ya watumiaji 1,000,000 na watumiaji wapya karibu 350,000 kila mwezi. Zoom pia inajivunia kuwa na watumiaji waliosajiliwa zaidi ya 225,000, na tovuti inazalisha maulizo zaidi ya 135,000 kati wanunuzi na wauzaji kila mwezi!
Uamuzi wa kujiuzulu kutoka Zoom Tanzania ulikuwa ni mgumu sana kwa Mr Gillis.
"Muungano wa ROAM ulitengeneza fursa muafaka kwangu kujitoa Zoom na kujikita katika biashara zangu nyingine, lakini nilihitaji kumpata Kiongozi mwenye nguvu, mjasiriamali, na mwenye uwezo mkubwa wakidigitali ili aiongoze Zoom iweze kufikia uwezo wake kamili."
Akiwa mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 ya kiutendaji katika sekta ya usimamizi wa masoko ya kitigitali na IT barani Afrika, Bi Rughani ana kila sifa ya kuchukuwa wasifu huu.
Anakuja ZoomTanzania.com akitokea Microsoft makao ya Kenya, ambapo alisimamia Ufumbuzi wa biashara ndogo na za kati ( Small and Medium Business (SMB) solutions) kwa ajili ya nchi 10 za Afrika ikiwemo Tanzania.
"Ninaiacha Zoom katika mikono salama na yenye uwezo mkubwa na ni imani yangu kampuni itanufaika sana na mtazamo mpya na safi wa Milli," alisema Gillis.
"Nafurahishwa zaidi kwa sababu yeye ni Mtanzania." ZoomTanzania.com ilitengenezwa na Watanzania, kwa ajili ya Watanzania, na sasa Mtanzania ataiongoza ZoomTanzania kuelekea mafanikio zaidi Bi Rughani alianza ZoomTanzania Januari 2017, na mipango ya makabidhiano ya uongozi inakwenda vizuri sana. "Hii ilikuwa nafasi ya kusisimua sana kwangu," alisema Bi Rughani.
"Nina imani kubwa katika ukuaji wa soko la mtandaoni Tanzania, na ZoomTanzania.com ina nafasi kubwa sana kuchangia kwenye ukuaji huu."
Wakati Bi Rughani akizidi kusimamia kazi za kila siku, Bw Gillis bado yupo hadi Machi mwaka 2017 akisimamia uzinduzi wa tovuti mpya na iliyoboreshwa zaidi.
Uzinduzi wa tovuti mpya ya ZoomTanzaniainatarajiwa kuongeza kasi ya tovuti na kuwarahishishia watumiaji, ikiwa ni pamoja na mfumo mpya wa matangazo ili kuongeza ufanisi katika kuwakutanisha wauzaji na wanunuzi.
"Jiandaeni kupokea mambo makubwa na mazuri "Mr Gillis na Bi Rughani," katika miezi ijayo utaona mfululizo wa vitu vipya vitakavyoongeza ufanisi kwa wauzaji kuonyesha bidhaa na huduma zao kwa Watanzania kwa ujumla."
0 comments:
Post a Comment