Thursday, December 7, 2017

TFDA YAWANOA WASINDIKAJI WA CHAKULA MKOANI GEITA

Kaimu Mkurugenzi usalama  wa chakula makao makuu ya TFDA  Bw Lazaro Mwambole akiendelea kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa kusindika chakula Mkoani Geita.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo ambao wanashughulika na usindikaji wa vyakula wakifuatilia mafunzo kwa umakini.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo ambao wanashughulika na usindikaji wa vyakula wakifuatilia mafunzo kwa umakini.

Kaimu Mkurugenzi usalama  wa chakula makao makuu ya TFDA  Bw Lazaro Mwambole akielezea dhumuni na malengo ya mafunzo hayo wakati alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi.

Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa idara ya uchumi na uzalishaji,Bw Emily Kasaga  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wafanyabiashara wa kusindika vyakula kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya mji wa Geita.

Baadhi ya washiriki  mkoani Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasimi na watumishi wa SIDO na TFDA.
Na,Joel Maduka,Geita.


Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA imewakutanisha wajasiriamali wanaosindika chakula mkoani Geita na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kutengeneza vyakula vinavyokidhi viwango vya usalama na vitakavyoweza kukuza soko la ndani na nje.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa usalama wa chakula makao makuu ya TFDA Bw Lazaro Mwambole alisema tafiti walizofanya zimebaini kuwa wengi wenye viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazotengeneza na hawajui kanuni za usindikizaji.

“Mgeni Rasmi taifiti ambazo zilifanyika mwaka 2016 zilionekana kuwa wamiliki wengi wa viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazozitengeneza hali ambayo imesababisha kutokufanya kwa ubora zaidi usindikaji wao”Alisema Mwambole.

Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita Bw Emily Kasaga amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha wanarutubisha vyakula ili view  salama na vyenye ubora kwa kuwa afya ya watumiaji iko mikononi mwao.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Bi Fatma Hassan na Bw Edward Geni wamesema mafunzo hayo yamewafungulia mwanga zaidi kwa kuwa wengi walikuwa wakifanya kazi hizo bila kujua kamawanakosea.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More