Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwahutubia wananchi wa Kijiji na Kata ya Nyawilimilwa Wilaya ya Geita wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipanda Mti kwenye moja kati ya maeneo ambapo kuna zahanati ya kijiji cha Nyawilimilwa. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akipanda mti kwenye zahanati ya Kijiji. |
Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoa wa Geita,Dkt Joseph Odero akimuelezea Mkuu wa Mkoa ,Mhandisi Robert Luhumbi namna zoezi la upimaji linavyoendelea Kijijini hapo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipewa maelezo na moja kati ya wahudumu wakati alipotembelea banda la huduma za afya kijijini hapo. |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita,Dkt Japhet Simeo akitoa taarifa ya Mkoa juu ya shughuli ya upimaji na watu ambao wameathirika na virusi vya Ukimwi. |
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akihutubia. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa,Mhandisi Robert Luhumbi. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akitoa msaada kwa watoto ambao ni yatima waliondokewa na wazazi kutokana na ugonjwa wa UKIMWI. |
Na ,Faudhia Sharifu,Geita
Jumla
ya watu 1,412 sawa na asilimia 3.5 wameathirika na virusi vya ukimwi Mkoani
Geita uku wanawake wakiwa ni 828 na wanaume wakiwa Ni 584.
Akizungumza
kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi
Duniani ambayo kimkoa yemefanyika kwenye kijiji na kata ya Nyawilimilwa, Mganga
Mkuu wa Mkoa wa huo Dkt Japhet Simeo amesema Takwimu za upimaji wa virusi vya
UKIMWI ngazi ya jamii Jumla ya watu waliopimwa maambukizi ya VVU katika kipindi
cha Aprili hadi Septemba 2017 ni 40,910 wanaume wakiwa ni 22,569 na wanawake
18,341 na ambao wamekutwa na maambukizi
ni 1,412.
Na
kwamba kutokana na hali hiyo Kiwango kimeendelea kupungua kutokana na mbinu na
mikakati mbalimbali za Mkoa dhidi ya maambukizi ya UKIMWI.
Aidha Dkt Simeo ameongeza kuwa Jumla ya wagonjwa 65,825 ambapo wanaume ni 24,812 na Wanawake 41013 Wamekwishaandikishwa kwenye vituo vya
Tiba na matunzo ,ambapo ni kuanzia 2012
– Septemba, 2017kati ya hao walioanzishwa dawa ni 52,550 wakiwemo wanaume 19296 na wanawake 33,254 na wanaoendelea na dawa (matibabu ni 32,709 wanaume
11188, na wanawake 19914) ambayo ni sawa na 62.2.
Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert
Luhumbi alisema kuwa kundi kubwa ambalo linaongoza kwa maambukizi ni
vijana ambao wanakuwa kwenye umri wa
miaka 15 hadi 25 huku wanawake na mabinti wakiongoza kwa kiasi kikubwa Mkoani
humo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi kwenye kijiji hicho,Devid Maduka,ameshukuru
zoezi la upimaji kuwepo kijijini hapo huku akiomba serikali kutoa walau siku
nyingi za upimaji.
Maadhimisho
ya siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa yamefanyika Jijini Dar es salaam huku
kauli mbiu ikisema i “Changia mfuko wa udhamini wa ukimwi okoa maisha
tanzaniabila ukimwi inawezekana”
0 comments:
Post a Comment