Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempongeza
Rais Magufuli kwa kuendelea kutekeleza ahadi za mgombea wake Urais Ndg.
Edward Lowassa kwa kuwapa msamaha wasanii Nguza Viking na mwanae
Johnson Nguza (Papii Kocha), waliofungwa kifungo cha maisha.
Msamaha huo wa Rais Magufuli kwa wafungwa hao na wengine zaidi ya 60
umetolewa leo kwenye sherehe za Uhuru zilizoadhimishwa Kitaifa Mkoani
Dodoma.
Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari inaeleza kuwa, Chadema
inampongeza Rais Magufuli kwa ujasiri wa kuendelea kutekeleza baadhi ya
ahadi zilizotolewa na Chama hicho kupitia Mgombea wa Urais wake Mhe.
Edward Lowassa, wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, imeeleza kuwa, pongeza hizo wamezitoa baada ya Rais Magufuli
kuhutubia sherehe za siku ya Uhuru wa Tanganyika ambapo ametoa msamaha
kwa wafungwa wa kifungo cha maisha Ndg. Nguza Vicking (Babu Seya) na
Johnson Nguza (Papii Kocha).
Ilieleza kuwa, kutokanana kitendo alichokifanya leo Rais Magufuli kwa
kutumia ibara ya 45 ya Katiba ya nchi kama ambavyo mgombea wa urais
aliahidi iwapo CHADEMA ingeshinda uchaguzi , kushika dola na kuongoza
Serikali, chama kingetoa wito kwa serikali kutumia mamlaka yake kwa
mujibu wa sheria za nchi, hususan kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya
(DPP) kwa utaratibu wa *Nolle Prosqui*, iondoe nia ya kuendelea
kuwashtaki, Masheikh wa Zanzibar wanaoshtakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Tanzania Bara pamoja na Mahabusu na watuhumiwa wa makosa ya
mitandao.
Pia watuhumiwa na mahabusu wa makosa ya kisiasa, ikiwemo kesi za
uchochezi zinazohusisha kumkosoa Rais Magufuli, kuikosoa serikali yake
na chama chake au tuhuma zinazotokana na kutekelezwa shughuli halali za
kisiasa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchini, ikiwemo maandamano,
mikutano ya hadhara na vikao vya ndani.
0 comments:
Post a Comment