Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu mpya ya muziki wa injili ya kwaya ya Wakorintho wa Pili utakaofanyika Desemba 24.
Wakorinto wa Pili wanazindua albamu yao ya pili inayoitwa Nguvu ya Imani iliyowekwa kwenye mfumo wa video katika tamasha kubwa litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Cheles, Sawala wilayani Mufindi.
Akitoa taarifa ya uzinduzi huo, makamu mwenyekiti wa kwaya hiyo, Ingrid Mwipopo alisema kwaya mbalimbali zinatarajia kuwasindikiza ikiwamo Muhimidini ya Iringa mjini, Upendo ya Kinyanambo-Mafinga na Upendo ya Mgololo.
Kwaya nyingine ni Halleluya, Vijana-Kibao, Edeni na Kaanani zote za wilayani Mufindi.
Mpaka sasa maandalizi ya uzinduzi wetu yamekamilika. Uzinduzi huu ni wa kihistoria, tutaanza saa saba mchana hadi saa 12 jioni, alisema.
Aliwataka wakazi wa mkoa wa Iringa na maeneo mengine jirani kujitokeza kuona kazi yao hiyo mpya ambayo imefanywa na Kampuni ya MBC Production ya Dar es Salaam.
Nyimbo mpya katika albamu hiyo licha ya Nguvu ya imani ni Mwimbieni Bwana, Bwana wanijua, Vyote ni mali yake, Mungu nguzo yangu, Tutashinda na Yesu, Shetani hana rafiki, Yesu ninakupenda na Jina la Yesu
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment