Wafugaji
Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,wamemuomba Naibu waziri wa mifugo na
uvuvi,Abdallah Ulega kuingilia kati manyanyaso ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka
kwa watu wa maliasili ambao wamekuwa
wakichukua mifugo yao na mwisho wa siku kupigwa mnada bila ya kufikisha mahakamani hali ambayo
imekuwa ikiwasababishia umasikini.
Imeelezwa
kuwa baadhi ya Minada ya Ng’ombe wanaokamatwa katika Mapori ya Hifadhi imekua
ikifanyika kinyume na kwa udanganyifu hasa ambapo katika mnada uliofanyika hivi
karibuni Wilayani Bukombe imegundulika katika Ng’ombe waliopigwa mnada 1600
kati yao 500 haijulikani ilipo huku kukiwa na malalamiko mengi kutoka kwa
Wafugaji.
Akizungumza
kwa niaba ya wafugaji Bw,kwa niaba ya wafugaji Bw,Emmanuel Maricholi wanzake
amemweleza naibu waziri kuwa wamekuwa wakikutana na shida kubwa pindi mifugo
yao inapokamatwa na kwasasa wafugaji wengi wamefilisika kutokana na hali ya
mifugo yao kukamatwa na kupigwa mnada bila ya kuwepo kwa maelewano baina yao na
watu wa maliasili na kwamba ni vyema wakaitazama kwa makini sheria ambayo
inafanyiwa kazi kwa sasa kwani imewafanya kuwa masikini zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko alisema ana taarifa ya baadhi ya Watu wanafaidika na Mnada huo kwa
manufaa yao wenyewe lakini pia amewataka Wafugaji kuvuta subiri juu ya
mabadiliko ya sheria ambayo yanaendelea kwani ukiangali sheria ya Wanyamapori
ya Mwaka 2009 ilikua inatoa adhabu ya vitu vitakavyokamatwa katika Mapori ni
kutaifishwa na Marekebisho yameplekwa bungeni na ishasomwa mara moja yenyewe
inaondoa adhabu ya kutaifisha na badala yake kuna faini.
Aidha,Mh
Doto Biteko ameongeza kuwa anatambua serikali imeendelea kujishughulisha na watu
masikini na kwamba ni lazima wafugaji wakaelimishwa hili wajue sheria na wajue
kuyatunza mazingira kabla ya kuendelea kuwahukumu kuwa wanaharibu mazingira na
kwamba kuna watu ndani ya idara wamekuwa na tabia ya kukamata mifugo kwaajili ya
kujipatia fedha hata kabla ya mnada.
Hata hivyo
kwa upande wake Naibu waziri wa mifugo na uvuvi,Abdallah Ulega,amewataka
wafugaji kutokukataa tamaa na kusubili hadi pale watakapo kuwa wameweka sheria
mpya huku akivitaka Vyombo vya Dola kuchunguza tuhuma za
uendeshaji wa minada ya Ng'ombe na hatua za haraka zichukuliwe kwa wote ambao
wamefanya minada hii kujinufaisha na kuwanyanyasa .
0 comments:
Post a Comment