Baadhi ya washiriki walioshiki katika kiakao cha mrejesho wa mradi wa kilimo endelevu
Na Adelphina Kutika
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilolo
na Iringa zimetakiwa kuendeleza mradi wa kilimo endelevu uliokuwa ukifadhiliwa
na shirika la Campein Female Education (CAMFED) chini ya dona yahoo katika
wilaya hizo ili kufikia malengo yaliyotarajiwa.
Wito huo umetolewa na kaimu
mkurugenzi wilaya ya Iringa Donard Mshani katika kikao cha tathimini ya mradi
wa kilimo endelevu baada ya mradi huo kufikia kikomo mwezi huu ambao ulikuwa na
lengo la kuhakikisha upatikanaji wa chakula mashuleni ili kuongeza ufaulu
katika shule.
“Iringa na killolo zimeteuliwa
katika mradi huu kilimo endelevu na mradi wenyewe utatekelezwa na wasichana
waliomaliza kidato cha nne (agricultural champion) ambao tunaamini kuwa
watautekeleza ipasavyo” alisema Mshani
Mshani alisema kuwa lengo la
mradi ni kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kwa kasi kubwa ili kuwa na chakula
cha ziada ambacho kitatumika kwenye shule ambazo zinauhitaji mkubwa wa chakula
na kulipongeza shirika kwa kuchagua fungu jema ambalo litakuwa na faida kwa
taifa.
“Naomba kutoa angalizo kwa
wasichana waliopata elimu hii wanapaswa kuitumia vizuri ili ianze kuwasaidia
wenyewe na jamii kwa ujumla hapo ndipo tutakapo ona faida ya elimu waliyoipata
kutoka katika shirka hili” alisema Mshani
Aidha Mshani amelipongeza shirika
la Camfed kwakutoa elimu ya kilimo kwa vikundi 206 vya
wazazi vilivyopo katika wilaya ya iringa na kilolo jambo ambalo limesaidia
kuongeza ajira kwa vijana waliokuwa wanawezesha katika vikundi
Kwa upande wake mratibu wa
shirika la Camfed wilaya ya Iringa Marcus Nyagawa alisema kuwa ukomo wa mradi
huo sio chanzo cha vikundi hivyo kufa kwani ipo mikakati ambayo wameiweka
kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu kwa kuzidi kutoa elimu na wasimamizi
kuongeza juhudi za kutembelea vikundi hivyo.
“Serikali imetuahidi kuwa mara baada
ya mradi huu kuisha watakuwa wanaufatilia vikundi kama vinafanya kazi ipasavyo
hivyo imani yangu kuwa vikundi hivi haviwezi kufa kwa kuwa serikali inamikakati
madhubuti ya kuviendeleza” alisema Nyagawa
Naye afisa maendeleo kata ya
kising’a Anna Baraka ameomba mashirika mengine kuiga mfano wa shirika la camfed
kwa kuwasaidia watoto wanaoishi mazingira magumu.
“Nashukuru hata serikali ya
wilaya imetambua kazi iliyofanywa na shirika hili hivyo kwangu naona kama ni
shirika namba moja ambalo linafanya vizuri zaidi katika wilaya hii” alisema Baraka
Baraka alisema kuwa kazi
iliyofanywa na shirika la CAMFED ilitakiwa kufanywa na serikali lakini waisaidia
serikali kutokanana ufinyu wa bajeti isinge weza kufanya hivyo naomba mashirika
mengine kuiga mfano kutoka shirika hili.
0 comments:
Post a Comment