Mradi
wa majaribio wa miezi 15 wa watoto waliokosa shule, kujifunza wenyewe
kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumia tableti umezinduliwa mkoani
Tanga.
Mradi
huo uliozinduliwa katika kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani Muheza ni
sehemu ya mradi mkubwa wa miaka mitano wa majaribio duniani chini ya
Global Learning Xprize wenye lengo la kutatua matatizo ya kujifunza.
Mradi huo hapa nchini unaendeshwa kwa pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na XPrize ambao wametoa tableti husika.
Aidha
kuwezekana kuwapo kwa mradi huo kumetokana pia na makubaliano kati ya
serikali ya Tanzania kupitia Wizara yake ya elimu na TAMISEMI na
mashirika.
Katika
utoaji elimu huo watoto wanaohusika ni wa miaka kuanzia 9 hadi 11 na
watajifunza kwa kutumia program tano zilizowekwa katika tableti
zitakazomuwezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
- Ofisa
Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akivishwa skafu na kukaribishwa
katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia
teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza
jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa
kupitia UNESCO na WFP. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia
anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
Mradi
huo wa Tanga ambao utagusa watoto 2,400 kutoka katika vijiji 167 vya
wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga na Pangani unatoa
changamoto kwa timu ya wabunifu kuwezesha watoto walio na fursa ndogo ya
kuingia katika elimu darasani kujifunza stadi za msingi za kusoma,
kuandika na kuhesabu (KKK) kwa kutumia tableti wakijifunza wenyewe.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Zenith, Muheza Mkoani
Tanga, Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi huo Faith Shayo
alisema kwamba mradi huo unaendana na majukumu ya Unesco ya kuhamasisha
elimu jumuishi katika kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania
wakiwemo wa jamii za pembezoni zilizo nyonge zinapata fursa.
Alisema
UNESCO inatekeleza majukumu yake kwa kuisaidia serikali ya Tanzania
kuwezesha kutoa elimu bora kwa wananchi wake wote na hata wale ambao
hawana uwezo wa kupata elimu kutokana na mazingira yao au maeneo yao.
- Mwakilishi
wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith
Shayo akivishwa skafu na kukaribishwa katika hafla ya kukabidhi tableti
kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na
kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa
na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kulia ni Ofisa
Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu.
Alisema
Unesco kwa kuangalia mahitaji imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania
katika vitu mbalimbali vya kiufundi ili iweze kufanikisha lengo la kuwa
na taifa la watu walioelimika hivyo kuwa na nafasi ya kushiriki katika
kazi za kujenga uchumi.
“Mradi huu unawapa watoto ambao hawakuwahi kujiunga na shule ya msingi, fursa nyingine” alisema
Faith na kuongeza kwamba juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya
Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa utaimarisha viwango vya
weledi nchini.
Faith anasema kwamba kwa sasa japo upo kwenye majaribio utakapofanikiwa utaweza kufanyiwa kazi maeneo mengine ya Tanzania.
Aidha
Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji
wa programu hiyo, Xavery Njovu alisema kwamba watoto hao wataangaliwa
kwa namna ambavyo wanaelewa kila wiki, wanapoenda kuchaji tableti zao.
- Ofisa
Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu na Mwakilishi wa Unesco ambaye
pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo wakiwasili
katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia
teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza
jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa
kupitia UNESCO na WFP.
“wakati
wa kuchaji pia tunaangalia matumizi ya tableti na ufaulu wa mtoto
katika kumaliza porogramu utaonekana na kama ikionekana hasongi mbele
itaangaliwa kasoro” alisema Njovu.
Alisema
kuna vijana 10 wanaojua Tehama na wamefundishwa kusaidia wanafunzi hao
katika kuhakikisha kwamba tableti hazikwami au kuharibika. Watu hao
wanaoishi vijijini hukohuko pamoja na kulipwa mishahara wamepewa
pikipiki mpya aina ya Yamaha kwa lengo la kuhakikisha wanafika kila kata
yenye wahusika na kuzungumza nao.
Pamoja na tableti hizo pia kumefungwa sola za kuchajia na seva ya kuangalia mwenendo wa watumiaji wa tableti.
Kabla ya kuzinduliwa kwa mradi huo watu 282 walifunza namna ya kuhudumia vijana hao ambao wanashiriki katika program.
- Mwenyekiti
wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, mkoani Tanga, Juma Killo akitoa
salamu kwa XPrize, UNESCO, WFP na wageni waalikwa katika hafla hiyo. Wa
pili kulia ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global
Learning Xprize, Faith Shayo, Afisa Miradi wa UNESCO, Nadia Marques (wa
tatu kushoto), Ofisa Elimu wa wilaya ya Pangani, Mbwana Mohamed (wa
tatu kulia), Kaimu Ofisa Elimu Lushoto, Beatus Kipfumo (wa pili kulia)
na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, Xavery Njovu (kulia).
Katika
mafunzo hayo wasimamizi hao ambao wanajulikana kama mama au baba
vitongoji walifunza malengo ya mradi na namna ya kuangalia mwenendo wa
watoto na mradi wenyewe.
Mgeni
rasmi katika ukabidhiaji wa tableti, Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga,
Mayasa Hashimu aliwataka wazazi kuhakikisha kwamba tableti hizo
zinatumiwa na watoto kwa makusudi yaliyopangwa ili kuwa na taifa la
watoto wenye weledi mkubwa.
Alisema
tableti hizo maalumu ni msaada mkubwa kwa wananchi na serikali hivyo
hawana budi kuzitunza na kuzitumia kwa makusudio husika.
“teknolojia
hii inayowezesha watoto kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu pasipo
msaada wa mwalimu ni ubunifu wa kiwango cha juu kabisa” alisema
Mayasa na kuongeza kwamba hali hiyo itabadili kabisa fikra za utoaji
elimu na kuwakomboa watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.
- Mgeni
rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (kushoto) akitoa
hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa
kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa
Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning
Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji
cha Zeneth wilayani Muheza mkoani Tanga, Juma Killo, Mchumi katika
ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza, Nelson Mwanuna pamoja na
Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning
Xprize, Faith Shayo.
Aliwataka wazazi kuunga mkono jitihada za serikali kupitia kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa kusaidia kujenga taifa lenye uelewa mkubwa kupitia chanzo cha sasa cha maarifa pasipo msaada wa mwalimu darasani.
Alisema msaada huo ni pamoja na kutunza vifaa vyote vya mradi na kutumiwa na wahusika bila kukosa.
Aidha alishukuru Shirika la UNESCO, XPRIZE na WFP kwa kuonesha njia na kusema kwamba mkoa utafanya kila linalowezekana kuona mradi huo wa majaribio unafanikiwa.
Katika makadihiano hayo watoto zaidi ya 10 walipewa tableti kwa niaba ya wenzao ambao wanashiriki katika mradi.
Mmoja
wa wazazi wa watoto waliokabidhiwa tableti aliyejitambulisha kwa jina
la Musa Ramadhani alisema amefurahishwa sana na mpango huo na kuahidi
kuhakikisha kwamba anatunza kifaa hicho ili mtoto wake afaidike nacho.
- Mwakilishi
wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith
Shayo akitoa salamu za UNESCO katika hafla ya kukabidhi tableti kwa
ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na
kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa
na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
“Mtoto
wangu mimi anaitwa Amir Musa na ana miaka 9; hapa tulipo ni ndani sana
kupatiwa kifaa hicho kitatusaidia sisi maskini tuliosahaulika kuwa
katika utaratibu tena wa weledi” alisema.
Aidha
alisema kwamba dhamana ya utunzaji inamuangukia yeye kwa kuwa anaamini
ni kazi yake kuhakikisha kwamba mtoto wake anapata mafanikio kutokana na
mradi huo.
Naye
mama Kitongoji Hilda Hule alisema kwamba ana uhakika kwamba watoto hao
watapata maarifa na kujua kusoma kwa kasi zaidi kwa kuwa hatua za mwanzo
zilionesha hamu yao ya kutaka kujua.
Anasema
kwa upande wake yeye anawaangalia watu wa kitongoji cha Zeneth na
anaamini kwamba kwa mradi huo watoto wengi watafunguka.
Mmoja
wa mateknisheni wa mradi huo ambao watasaidia uwapo wa tableti na
program zake Francis Kibaja mwenye makazi yake Korogwe alisema kwamba
mfumo huo wa kitabu cha kielektroniki kinamfanya mwanafunzi ajifunze na
kujisahihisha na kama watamaliza programu mapema kutokana labda kwa
urahisi watawapangia programu ngumu zaidi ili kuwakomaza.
- Mwakilishi
wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu
hiyo, Xavery Njovu akitoa salamu za WFP katika hafla ya kukabidhi
tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika,
kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio
unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
Aidha
alisema kwamba tableti hizo zinagemu kwa ajili ya mtoto akichoka na pia
wakati wa mazoezi program itamwambie mtoto kama amekosea au amepatia.
Programu
zilizowekwa kwa sasa katika tableti hizo ambazo hazina uwezo wa simu ni
sawa na mtu kuanza darasa la awali na kuingia shule ya msingi.
Katika
mradi huo WFP wamepewa dhamana ya kusimamia uendeshaji wa kitengo cha
lojistiki na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama-ICT) cha
majaribio katika mazingira halisi.
- Mama
Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule ambaye
anajukumu la kuchaji na kutunza tableti hizo akitoa maelezo ya namna
zinavyotumika kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa watoto wa kijiji hicho.
Aidha
jukumu lake ni pamoja na kuingiza programu katika tableti, kuanzia
vituo vya kuwekea umeme unaotokana na jua kwenye tableti hizo vijijini,
kusimamia matengenezo, marekebisho na kutoa tableti mpya kipindi chote
cha majaribio.
Uzinduzi
huo ulipambwa na mambo mbalimbali ukiwemo muziki wa asili ambapo
kikundi cha JAHAZI ASILI zilitumbuiza kwa ngoma za asili za wakazi wa
Tanga na pia muziki wa singeli.
Ofisa
wa Xprize naye alitumbukia katika burudani za singeli na kuwa burudani
kubwa kwa watu ambao walienda naye sambamba na kama yeye alivyokuwa
akienda sambamba na wenyeji katika zungusha.
- Mwakilishi
wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu
hiyo, Xavery Njovu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
jinsi programu mbalimbali za kujifunzia zinavyofanya kazi kwenye tableti
hizo.
- Ofisa
Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akisisitiza umuhimu wa wazazi
(hawapo pichani) kushiriki katika utunzaji wa tableti hizo kabla ya
kuzigawa rasmi. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia
mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
- Ofisa
Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia) akisalimiana na
mtoto Saidi Hausi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi la kukabidhi
tableti hizo. Kulia ni Mama Kitongoji Hilda Hule mwenye jukumu la
kutunza na kuchaji tableti hizo kwa umeme wa sola na Wa kwanza kushoto
ni Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia
utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu na Mwakilishi wa Unesco
ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
- Mama
Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule (kulia)
akikabidhi tableti kwa mtoto Saidi Hausi huku Ofisa Elimu wa mkoa wa
Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia), Mwakilishi wa Unesco ambaye pia
anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo (wa pili
kushoto) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia
utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (kushoto) wakishuhudia tukio
hilo wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia
teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza
jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa
kupitia UNESCO na WFP.
- Ofisa
Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia) akisalimiana na
mtoto Juma Saidi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi la kukabidhi
tableti hizo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kulia ni Mama Kitongoji Hilda
Hule mwenye jukumu la kutunza na kuchaji tableti hizo kwa kutumia umeme
wa sola, Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia
utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (wa kwanza kushoto),
Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning
Xprize, Faith Shayo (wa pili kushoto).
- Tala
Loubieh wa WFP akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia programu ya
kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu kwa mtoto Gabu Lakiki mara baada
ya kukabidhiwa rasmi tableti hizo kwenye hafla hiyo.
- Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller
akiwapongeza baadhi ya watoto wa kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani
Muheza, mkoani Tanga waliokabidhiwa tableti hizo.
- Baadhi
ya wafanyakazi wa WFP wanaotoa msaada wa Tehama kwenye tableti hizo kwa
watoto wa kijiji cha Zeneth pamoja wanakijiji wakifurahi jambo katika
katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia
teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza
jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa
kupitia UNESCO na WFP.
- Baadhi
wazazi/walezi wa watoto wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza
wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa
ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na
kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa
na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
- Kikundi
cha ngoma cha Jahazi Asilia cha wilayani Muheza wakitoa burudani katika
hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia
kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi
huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia
UNESCO na WFP.
- Makomandoo
wa Skauti wakionyesha umahiri wao wakati wa kusherehesha hafla ya
kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza
kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa
majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na
WFP.
- Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller
akijumuika na watoto wa kijiji cha Zeneth kucheza SINGELI wakati wa
hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia
kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi
huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia
UNESCO na WFP.
- Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller
aliponogewa na SINGELI katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya
mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu
uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global
Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
- Mgeni
rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto
waliowakilisha wenzao kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya
mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu
uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global
Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
- Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE ambao ndio wafadhili
wakuu, Matt Keller akiwa kwenye picha ya pamoja na Wataalamu wa Tehama
walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo
yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na
vitongoji vyake.
- Wafanyakazi
wa WFP wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa Tehama
walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo
yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na
vitongoji vyake.
0 comments:
Post a Comment