Wednesday, December 13, 2017

KESI ZA WANAUME KUTELEKEZA FAMILIA ZAO ZAIDI KUONGEZEKA DAR

Huduma zikitolewa kwenye Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

Na Joachim Mushi

Kesi za wanaume kutelekeza familia zao zimejitokeza kwa wingi Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.
Akizungumza katika kituo hicho kilichoratibiwa na Kituo cha Usuluhishi – CRC, kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mwanasheria wa Kituo cha CRC, Bi. Suzan Charles alisema idadi kubwa ya wateja waliowahudumia kwa siku mbili ni akinamama waliotelekezwa na waume zao au wanaume waliowazalisha.
Zoezi hilo la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ lililoendeshwa kuanzia Desemba 11 na 12 eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam tangu majira ya asubuhi hadi jioni lilishirikisha huduma za msaada wa kisheria, Ushauri nasihi pamoja na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi.
Akifafanua zaidi Mwanasheria wa CRC, Bi. Suzan Charles alisema licha ya uwepo tatizo la utelekezaji watoto, lakini walikuwepo pia akinamama wajawazito ambao nao walitelekezwa wakiwa na hali hiyo jambo ambalo lilikuwa na changamoto kubwa kwao, kwani hali zao ni dhaifu hawawezi hata kufanya kazi kujipatia kipato kwa sasa.
Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Kituo cha CRC, Bi. Violeth Chonya mbali na kutoa ushauri wa wateja waliojitokeza walishirikiana na vitengo husika vya serikali katika kuwaita wanaolalamikiwa kutelekeza familia na kuangalia namna ya kutatua kesi hizo.
Alisema wateja waliokuja kupata huduma katika kituo hicho pia wamekuwa wakitoa elimu ya uzazi kwa kushirikiana na idara ya afya ili wana jamii kujitambua na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali.
“..Unajua masuala mengine kwa wateja waliotutembelea kwa siku hizi mbili tumebaini akinamama wengi hawana elimu ya kutosha juu ya masuala ya uzazi, unakuta mama hapewi huduma zozote za msingi toka kwa mwenza wake lakini bado anaendelea kuzaa huku analalamika kutosaidiwa matunzo…hapa utabaini kabisa mama hataki kuongeza idadi ya watoto ila ameshindwa kuzuia mimba anaendelea kuzaa,” alisema Bi. Violeth Chonya.
“Naamini mtu kama huyu akipatiwa elimu ya masuala ya uzazi anaweza kuamua kupata mtoto pale tu anapoitaji na kuacha kulundika idadi ya watoto huku akiendelea kukumbana na changamoto ya huduma toka ama kwa mume au wenza wake..,” alisema Afisa Ustawi wa Jamii huyo wa Kituo cha KCRC.
Alisema kumekuwa na muamko mkubwa kwa jamii ya Kata ya Saranga, Temboni kuja kupata huduma zilizokuwa zikitolewa kituoni hapo jambo ambalo linaonesha upo uhitaji mkubwa ya kutengenezwa kwa vituo hivyo, ili vihudumie jamii kwa karibu.
Huduma zikitolewa kwenye Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

Huduma zikitolewa kwenye Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.
Huduma zikitolewa kwenye Kata ya Saranga eneo la Kimara Temboni jijini Dar es Salaam kwenye kituo maalumu cha muda kilichoendeshwa kutoa huduma za pamoja kwa waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More