Serengeti. Mtuhumiwa anayedaiwa kuingia kininja ndani ya
gesti bubu na kumkata koromeo mwanaume aliyekuwa na mke wake kisha
kutoroka katika kijiji cha Tamukeri wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara
amenaswa.
Mtuhumiwa Simioni Mturi(50) alitenda unyama huo oktoba 3 mwaka huu
majira ya usiku baada ya kuingia gesti bubu kwa kupitia darini na
kumkata kichwani Paul Chacha (24)Mkazi wa kijiji cha Nyansurura wilaya
hapa na baada ya kuanguka akamchinga mithiri ya mbuzi, kisha akamkata
kifundo cha mguu mkewe Bhoke Simion(36)na kutoroka.
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Mang’era Magesa amesema mtuhumiwa
amekamatwa desemba 10 majira ya sita mchana mwaka huo muda mfupi baada
ya kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
“Baada ya kutenda tukio hilo alitoroka na amekuwa anaishi kwa kujifichaficha, tuliweka mtego baada ya kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha, amekabidhiwa Polisi kwa ajili ya hatua za kisheria,” amesema.
“Baada ya kutenda tukio hilo alitoroka na amekuwa anaishi kwa kujifichaficha, tuliweka mtego baada ya kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha, amekabidhiwa Polisi kwa ajili ya hatua za kisheria,” amesema.
Polisi wilayani hapa wamekiri kumshikilia mtuhumiwa na kuwa taratibu za kiuchunguzi zikikamilika atafikishwa mbele ya Sheria.
Kwa mjibu wa majeruhi Paul na Bhoke walikiri kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na siku ya tukio walikuwa ndani ya gest bubu hapo kijijni na
kushambuliwa.
“Tukiwa ndani mlango wa chumba tulichokuwa uligongwa na
hatukufungua,ghafla mtuhumiwa akaingia chumbani kupitia darini akiwa na
panga na kuanza kumkata mke wake kifundo cha mguu kisha
akanishambulia,nilizinduka baada ya siku mbili nikiwa hospitali Teule ya
Nyerere wilaya ya Serengeti,” alisema Paul.
Hata hivyo Bhoke ambaye ni mke wa mtuhumiwa alisema, siku ya tukio
Mme wake aliaga anaenda msibani kijiji tofauti na hakujua nani alitoa
siri hiyo na kuwavamia na baada ya kuwa kata akiamini Paul amekufa
alichukua sh 80,000 alizokuwa nazo huyo mwanamke na kutoroka.
Majeruhi baada ya kutoka hospitali hawajaonekana Polisi kutoa maelezo kwa kile kinachodaiwa hofu ya kuhojiwa kwa kukamatwa ugoni.
Majeruhi baada ya kutoka hospitali hawajaonekana Polisi kutoa maelezo kwa kile kinachodaiwa hofu ya kuhojiwa kwa kukamatwa ugoni.
0 comments:
Post a Comment