Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amewataka wananchi kuwa watulivu wakati
Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto
ulioteketeza nyumba yake.
Nyumba
hiyo iliteketea jana Jumamosi alasiri na hakuna madhara kwa binadamu
yaliyotokea isipokuwa mali zote zilizokuwamo ndani zimeteketea.
“Tumepata
ajali kidogo. Nyumba yangu ninayoishi katika eneo la Kibingo, mji mdogo
wa Mwandiga, Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii. Alhamdulillah, kuwa
hakuna binaadam aliyeumia,” aliandika Zitto katika ukurasa wake wa
Facebook.
Alisema
analishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, majirani zake na wananchi
wenzake kwa ushirikiano walioutoa ili kuzima moto huo.
“Kwa
sasa Jeshi la Polisi wanafanyia kazi kujua chanzo cha ajali. Naomba
wananchi wawe watulivu wakati Polisi wanaendelea na uchunguzi husika,”
alisema Zitto.
Nyumba hiyo aliyoijenga wakati akigombea ubunge kwa mara ya kwanza iko kiwanja kimoja na nyumba yake ya sasa.
Msaidizi
wa mbunge huyo, Nyembo Mustafa alisema Zitto hakuwa anaishi kwenye
nyumba hiyo baada ya kujenga nyingine kubwa kwenye kiwanja hicho.
0 comments:
Post a Comment