Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepiga marufuku viongozi wa Serikali
kuwakamata na kuwaweka rumande watumishi wa umma bila kufuata sheria na
taratibu za utumishi.
Gambo
alisema juzi kuwa siku za hivi karibuni kumejitokeza matukio ya baadhi
ya viongozi kuwaweka rumande watendaji wa Serikali bila kufuata
taratibu.
“Kama
mtendaji alikosea kuna taratibu zake, kuna masuala ya kiutumishi, kuna
ya kijinai na ya uchunguzi, hivyo ni busara kufuata taratibu,” alisema.
Gambo
aliwataka viongozi kutumia vyombo vilivyowekwa na Serikali kutatua
matatizo ikiwamo, Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na
pia kufuata sheria za utumishi wa umma.
Pia,
aliwataka watumishi wa umma mkoani Arusha kufanya kazi kwa kushirikiana
na kuepuka majungu kwa kuwa wote wanawajibika kwa wananchi.
“Fanyeni
kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana ili kuepusha migogoro isiyo ya
lazima katika halmashauri zenu na wilaya kwa jumla,” alisema Gambo.
Awali,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Vijijini, Wilson Mahera alisema
wamejipanga kutatua kero za watumishi na wananchi ili kuhakikisha
wanapata maendeleo.
Mahera
alisema katika bajeti iliyopita Sh580 milioni zilitumika kuboresha
miundombinu katika sekta ya elimu kama kujenga nyumba za walimu,
madarasa na kukabiliana na upungufu mwingine.
Alisema katika bajeti ya mwaka 2017/18 pia, mikakati imewekwa kukabiliana na kero mbalimbali za watumishi na wananchi.
Mahera alisema mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa ni zaidi ya Sh3 bilioni huku Sh39 bilioni zikitoka Serikali Kuu.
0 comments:
Post a Comment