Friday, September 8, 2017

DC ASIA APIGA MARUFUKU WILAYA YA KILOLO KUTOA WAFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI

Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa katika moja ya shule ya msingi ya wilayani humo akiangalia hali ya usalama wa wanafunzi wakati wa kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi
 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanafuzi waliohitimu elimu ya shule ya msingi katika shule ya msingi Boma la ng'ombe wilaya kilolo mkoani Iringa 

Na fredy Mgunda,Iringa.

Wananchi wa wilaya ya kilolo mkoani iringa watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza uchumi wa taifa.

Akizungumza wakati wa kuangalia amani ya wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wanafanya mitihani ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema sasa imefika mwisho wa wilaya hiyo kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa kilolo sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Abdallah

Abdallah aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwapeleka shule watoto waliofaulu kinyume cha hapo wazazi watachukulia hatua kali.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Abdallah

Aidha Abdallah aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo.

“Acheni kuwavulia sketi wanaume mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu kama mimi ambavyo leo hiii nimekuwa kiongozi wenu kwa kwasababu nilikataa kuvua sketi nikiwa na umri kama wenu ndio maana leo hii nipo hapa”alisema Abdallah

Aidha Abdallah aliwapongeza walimu wa shule za msingi za wilaya ya kilolo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri wilaya ya kilolo kupitia elimu.

“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu wa wilaya hii kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika wilaya yangu ya kilolo na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Abdallah

Kwa upande wake diwani wa kata ya boma la ng’ombe Anderson Mdeke alikiri kuwepo kwa tatizo la mimba shuleni limekuwa sugu hivyo wameanza kulitatua tatizo hiyo na limepungua kwa kiasi kikubwa.

“Kwa kweli tatizo la mimba kwenye shule za kata yangu ya lipo na tumeanza kutafutia ufumbuzi ili kulitokomeza kabisa na watoto wetu wasome bila kuwa na buguza” alisema Mdeke

Naye mwalimu wa shule ya msingi Mwanzala Grace Magawa alikiri kuwepo kuwepo kwa mimba za utotoni katika  baadhi ya shule za msingi za wilaya ya kilolo kutokana mazingira yanayowakabili baadhi ya wanafunzi ndio husababisha mimba za utoto.


“Mwanafunzi akirudi nyumbani anawakuta wazazi wake washakunywa pombe na hawana habari ya kuulizia maendeleo ya mtoto wake hivyo mtoto anaamua kufanya anachotaka kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha kutoka kwa wazazi wake au walezi wake” alisema Magawa

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More