Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani
Jafo amewatakaa Wakuu wa Wilaya kuitumia vizuri sheria ya kumuweka mtu
ndani kwa saa 48 pasipo uonevu wowote.
Jafo
ameitoa kauli hiyo Mjini Dodoma alipokuwa akifunga mafunzo ya Uongozi
ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri
kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Shinyanga
na Dar es Salaam, Yalioanza Septemba 11, mwaka huu.
"Fanyeni
kazi kwa kufuata mipaka yenu ya kazi, kwani ndilo jambo pekee litakalo
waepusha na migogoro katika maeneo yenu ya kazi," amesema Jafo.
Amesema
, viongozi hao wanapaswa kufanya kazi pasipo kumuonea au kumpendelea
mtu kwa namna yoyote ile, bali wakawe mifano kwa kujenga uhusiano mzuri
na watumishi wanao waongoza pamoja na wananchi.
Jafo
amewataka kwenda kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni
pamoja na vita dhidi ya rushwa na dawa za kulevya, usimamizi wa miradi
ya maendeleo,matumizi ya mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa
mapato ya Serikali pamoja na kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma.
Wakati
wakiendelea na mafunzo hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi
amewatembelea Wakuu hao wa Wilaya na kuwapa miongozo ya utendaji kazi
pamoja na mipaka ya kazi yao ili kuepuka migogoro katika maeneo yao ya
kazi.
0 comments:
Post a Comment