NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema, tayari asilimia 95 ya uboreshaji miradi
ya umeme katika jiji la Dar es Salaam, imekamilika.
Meneja
Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi, Mahende Mgaya, (pichani juu), amewaambia
waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2017 na
kwamba ifikapo Desemba mwaka huu wa 2017, wananchi na wakazi wa Dar es Salaam
wataona ile hali ya kukatika kwa umeme, mara kwa mara imebadilika.
“Tulikuwa
na jumla ya miradi mipya 18 ya kuboresha vituo vya umeme jijini Dar es Salaam
ili viweze kutoa umeme wa kutosha na wa uhakika, hadi sasa, vituo vinane
vimekamilika kabisa na vinafanya kazi, vimebaki vituo 10 ambavyo navyo viko
katika hatua za mwisho za kukamilika, na ifikapo Desemba, 2017 vituo vyote 18 vitakuwa vinafanya akzi.”
Alitoa hakikisho Mhandisi Mgaya.
Alisema,
kufuatia kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi na idadi ya watu jijini Dar es
Salaam, mahitaji ya nishati ya umeme nayo yameongezeka na hivyo Serikali
kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliamua kuchukua hatua za haraka kuboresha
vituo vyake vya umeme ikiwa ni pamoja na kujenga vipya ili kukidhi mahitaji halisi ya
umeme.
“Wafadhili
kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB, World Bank, Finland, na Japan),
walijitokeza na kufadhili miradi hiyo.”Alifafanua.
Kazi
hiyo ya kuboresha vituo hivyo ambavyo ni pamoja na Mbagala, Kurasini, Kigamboni, Ilala
Mchikichini, Kisutu, Mikocheni, Gongolamboto, na maeneo mengine imekuwa
ikifanyika tangu miaka miwili iliyopita lakini kutokana na matatizo ya hapa na
pale, ikiwa ni pamoja na mapingamizi ya wananchi kuzuia utekelezaji wa miradi
hiyo, na wakandarasi, kumepelekea ucheleweshaji.
Maeneeo
ambayo yamekuwa yakiathirika zaidi na hali hiyo ya kukatika kwa umeme mara kwa
mara ni pamoja na Wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo na baadhi ya maeneo ya
wilaya ya Kinodnoni.
“Nichukue
fursa hii kuwaomba radhi wananchi, hususan wateja wetu, kutokana na hali hii ya
kukatika kwa umeme, lakini napenda pia waelewe kuwa hali hiyo inatokana na kazi
ambayo tumekuwa tukiifanya, na mara nyingi umeme tunakata siku za weekend, kwa
vile shunguli nyingi za kiofisi zinakuwa zimepungua na hivyo inakuwa fursa
nzuri kwetu kufanya kazi.” Alifafanua Mhandisi Mgaya.
Alisema,
wananchi wanataka umeme, tena ulio bora na wa uhakika, ndio maana TANSCO
imeamua kuchukua hatua madhubuti za kuboresha na kujenga vituo vipya vya kupoza
na kusambaza umeme ikiwa ni pamoja na kujenga lini mpya za kusafirisha umeme.
“Hatu
hizi zote lazima ziwe na changamoto za hapa na pale, lakini kwa kiasi kikubwa
TANESCO inaelekea kulitatua tatizo hilo la umeme jijini Dares Salaam na
Mkuranga.”. Alisisitiza.
Wakandarasi na mafundi wa TANESCO wakiwa kazini
Moja ya vituo ambavyo vimefungwa mitambo mipya ili kuboresha upatikanaji wa umeme jijini Dar es Salaam.
Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kisutu.
0 comments:
Post a Comment