Mkuu
wa Wilaya ya Mbarali Mh. Reuben Mfune ameagiza bar zote, migahawa,
vilabu vya pombe na grocery kufungwa kwa siku zisizojulikana kutokana na
ugonjwa wa kipindupindu kuzidi kusambaa wilayani humo.
Mkuu
wa wilaya ametoa taarifa hiyo kupitia Afisa habari wa wilaya hiyo Daudi
Nyingo na kuwataka wananchi kuwa makini na matumizi ya maji ya mito na
mifereji kwani yameathiriwa na vijidudu vya kipindupindu.
"Wananchi
wote wa wilaya ya Mbarali mnatangaziwa kuwa hali ya ugonjwa wa
Kipindupindu bado ni mbaya sana wilaya hapa, hivyo basi biashara zote za
migahawa, vyakula vyote vinavyotembezwa, minada, vilabu vya pombe, bar,
grocery zote, pamoja na mikusanyiko yote inayohusiana na sherehe, vyote
vimefungwa hadi hapo mtakapotangaziwa tena"
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali amesema kuwa mtu yoyote ambaye atakiuka maagizo hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria
"Aidha
mashine zote zitakazobainika kusaga vimea au unga wa pombe za kienyeji
hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao Vilevile mnakumbushwa
kwamba, maji yote ya mito pamoja na mifereji yameathiriwa na vijidudu
vya Kipindupindu, hivyo basi wananchi wote mnaagizwa kuchemsha maji au
kutumia vidonge vya 'water guard' pamoja na kufanya matumizi sahihi ya
vyoo" alisema Mfune
Hadi
kufia Septemba 15, 2017 jumla ya wagonjwa 628 wamepatikana huku jumla
ya watu nane wamefariki kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu wilayani
Mbarali jijini Mbeya.
0 comments:
Post a Comment