Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amekerwa na uchafu ulioko katika vyumba vya upasuaji vya hospitali ya rufaa ya Musoma na zahanati ya Murangi na vyumba hivyo kubadilishwa stoo na eneo la taka.
Naibu Waziri ambaye Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku nne alifanya ziara ya kushtukiza katika hopsitali ya rufaa ya Musoma na kubaini uchafu uliopo katika chumba cha upasuaji kilichozinduliwa mwaka jana kwa mashuka na mipira yake kuwekwa chini na huku kukiwa na vifaa vya kuwekea mashuka hayo.
‘’Hivi ndivyo mnatunza vitu vya upasuaji kweli,matroni hivi,kuna sababu gani ya nyie kuondoka hapa,mali ya umma inaharibiwa hivi, hamna uchungu jamani, sisi sote ni watanzania, leo mimi naweza kuugua hapa, Mkuu wa Mkoa au mwanachi,kwa hali hii hapa kun ahuduma kweli..na hii eti ndo hopspitali ya rufaa ambayo mtu akizidiwa huku pembeni analetwa hapa? Alihoji Kigwangalla na kuonyesha masikitiko makubwa.
Aidha aliagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Adoh Mapunda kuajiri Mganga mfawidhi wa hospitali (Medical officer Incharge) mpya atakayesimamia hospitali hiyo.
Sanjali ya hayo alishangazwa pia kuona chumba hicho mabomba na masinki yakiwa mabovu na ukosefu wa taa katika chumba cha kutokosea vifaa, (stearlization Room) vifaa vya kubebea madawa ambavyo vinanesa nesa na vifaa vya kuchemshia vifaa vya upasuaji vikiwa chakavu na sehemu ya kuwekea vifaa hivyo ikiwa pia chakavu.
Akiwa katika chumba cha upasuaji cha Murangi alipokelewa na harufu za damu iliyooza na harufu ya popo,huku vifaa vya kutupia taka zikiwa ni ndoo za mafuta ya kupikia na kuagiza pia usafi ufanyike na kuondolewa kwa kinyesi cha popo na kuziba maeneo wanayopita kwani sehemu hiyo inatakiwa kuwa na usafi wa hali ya juu.
Aidha aliagiza kuwepo kwa mtaalamu wa mashine mpya iliyopo katika chumba hicho,na mashine ya usingizi,(Anaesthesia Machine), kwani hakuna mtaalamu na kuwekwa mfumo wa computer ili kukusanya mapato halisi.
Akiwa katika wodi ya wazazi aliwasalimu wazazi waliojifungua siku hiyo na kuwaombea afya njema.
Nao Wazazi, Nyachiro Phares wa kata ya chumwi aliyejifungua siku hiyo mtoto wa kike na Sikujua Goda wa Kata ya Musanja aliyejifungua mtoto wa kiume waliipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Mwanamke anajifungua salama kuliko hapo awali ambapo walikuwa wanajifungua nyumbani hali ambayo ilikuwa inahatarisha afya na usalama wao.
Akizungumza mara baada ya Naibu Waziri kutembelea wodi ya wazazi,chumba cha upasuaji na Maabara, Mjumbe Mkutano Mkuu UWT Taifa kutoka Wilaya ya Musoma, Eva-Sweet Musiba alimpongeza Naibu waziri huyo kwa ziara yake Mkoani Mara ambayo italeta chachu ya kufanya kazi kwa uadilifu na si kwa mazoea ambayo yalikuwa yamekidhiri.
Aidha amewataka akina Mama kuipenda Serikali ya awamu ya Tano kwani inajali akina mama, wazee na watoto.
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mfumo wa maji ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akihoji uchafu uliokuwa ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana
Baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani ya chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mkoa wa Mara, hali hiyo ni kinyume na utaratibu wa vyumba vya upasuaji
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo chumba hicho cha upasuaji huku akipata maelezo.
Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara
0 comments:
Post a Comment