Watu watano wamefariki dunia katika kijiji cha Ngiresi wilaya ya Arumeru mkoani Arusha baada ya mti mkubwa kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa kuamkia leo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa kuanguka kwa mti huo kumetokana na athari za
mvua zinazoendela kunyesha.
Amesema
kuwa waliofariki dunia ni watoto watatu ambao walikuwa wanafunzi na
vijana wa wiwili. Kamanda huyo amesema taarifa zaidi atatoa hapo baadae.
0 comments:
Post a Comment