Tuesday, May 2, 2017

VIDEO: WAKAZI WA KATA YA BUZURUGA JIJINI MWANZA WAFANYA USAFI KITUO CHA AFYA CHA KATA HIYO

George Binagi-GB Pazzo

Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machemba, amewakutanisha pamoja wakazi wa Kata hiyo na kufanya usafi wa mazingira katika Kituo cha Afya Buzuruga ili kuondoa hatari ya vichaka kituoni hapo.


Akizungumza jana wakati wa zoezi hilo, Machemba alisema uamuzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani na kwamba hatua hiyo pia itasaidia kuondoa hatari za kimazingira ikiwemo magonjwa kituoni hapo.



Mwenyekiti wa Kamati ya Afya Kituo cha Afya Buzuruga, Daniel Buluya, alisema awali mazingira ya Kituo hicho hayakuwa salama hatua ambayo ilikuwa inahatarisha usalama wa wagonjwa na watumishi wa afya kituoni hapo.


Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei Mosi ili kutoa mwanya wkwa wafanyakazi pamoja na viongozi mbalimbali kutafakari changamaoto zinazowakabiri wafanyakazi na namna ya kuzitafutia ufumbuzi ambapo Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika Moshi mkoani Kilimanjaro huku kauli mbiu ikiwa ni "Katiba na Utawala, Vizingatie Haki na Maslahi ya Wafanyakazi".
Tazama Video hapo chini.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More