Monday, May 1, 2017

RC MASENZA-IRINGA HAKUNA UPINZANI BALI UPINZANI UPO NDANI YA CCM

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akizungumza mbele ya viongozi wa Kata na matawi wa chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya Iringa
Mkuu wa mkoa wa iringa bi Amina Masenza akizungumza na viongozi na wananchama wa chama cha mapinduzi Manispaa ya Iringa

Na Fredy Mgunda, Iringa

Unafiki na Chuki binafsi zilichangia kukimaliza chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya iringa katika uchaguzi wa ubunge na udiwani mwaka 2015 kutokana na viongozi wengi wa chama hicho kutokuwa waadilifu katika kukitumikia chama hicho.

Maneno hayo yamesemwa na viongozi mbalimbali wa CCM ndani ya Manispaa na mkoa wa Iringa wakati wa kikao na viongozi wa matawi na Kata za Manispaa ya Iringa.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkuu wa mkoa wa iringa bi Amina Masenza aliwata mwanachama na viongozi wa chama hicho kuacha majungu,unafiki na usaliti kwa kuwa hiyo moja ya vitu vilivyo wamaliza katika uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini hivyo ifike wakati wasaliti wote wa chama kuacchia ngazi mwenyewe bila kufukuzwa na viongozi wapya walikuja sasa kukiongoza chama hicho hapa Manispaa ya Iringa.

"Haiwezekani mwanachama na viongozi wakakubali kununuliwa kwa shilingi elfu hamsini na kukisaliti chama hao sio wapenda chama na wafia chama bali ni wanafiki,waroho wa pesa hivyo nawaomba makatibu wote sasa ni wakati wa kukisafisha chama na kurudisha imani kwa wananchi wa Manispaa ya Iringa "alisema masenza

Masenza aliwataka viongozi wa Kata na matawi wa chama cha mapinduzi CCM kuanzia kufanya kazi kwa vitendo na kuacha unafiki na usaliti ili kufanikisha malengo katika uchaguzi wa mwaka 2020 uwe rahisi kwa chama hicho kukomboa jimbo la Iringa Mjini ambalo lipo chini ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati alisema kuwa sasa ni wakati wa kuzitafutia njia ya kuzitatua changamoto zinazowakabili wananchi na mwanachama katika maeneo wanayoishi ili kuwafanya wananchi kuanza kukipenda chama hicho.

"Lazima kufanya kazi kwa kujituma na kuacha majungu ni lazima tujitume ili wananchi wa Manispaa ya Iringa waone kuwa chama cha mapinduzi kinafanya kazi kubwa licha ya kuwa jimbo lipo upinzani" alisema Kabati

Kabati aliwataka viongozi wa Kata kuziweka bayana changamoto wanazokabiliana ili kuzitafutia ufumbuzi wa uhakika na kuwasaidia wananchi wa Manispaa ya Iringa kupata maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk John Pombe Magufuli.

Aidha Ritta Kabati alisema kuwa chama cha mapinduzi Manispaa ya Iringa kimechafuka sana taifa kutoka na usaliti ulifanywa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 hivyo ni lazima kurudisha imani kwa wananchi wa mkoa wa Iringa ili kuwasaidia viongozi wa chama wa kitaifa kuwa na imani na viongozi wa Manispaa ya Iringa.

"Wenzenu wabunge wa mkoa wa Iringa tumekuwa tunasemwa sana juu ya usaliti ulitokea hapa Manispaa hivyo kila kitu kibaya tunatolewa mifano mkoa wa Iringa chonde chonde tusirudie tena kilichotokea mwaka 2015" alisema Kabati

Naye Katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Christopher Magala aliwataka wanachama wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kuwa wamoja na kuendelea kujenga imani kwa wananchi wa mkoa wote na kuwataka viongozi wa chama Manispaa ya Iringa kujipanga na kuwa makini wakati wa kuendesha shughuli za kukiinua chama hicho.

"Kwa kweli chama hicho ndani ya Manispaa ya Iringa kimekuwa na wasaliti sana hivyo viongozi wangu wa wilaya ni lazima kuwa makini sana na wanachama pamoja viongozi wa chini hap huku juu ili kuondoa usaliti kwa maendeleo ya chama" alisema Magala

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More