Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Iringa kama Naibu Meya Joseph Lyata na mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati wakisikiza hoja za wananchi wa Kata ya mlandege
Na Fredy Mgunda, Iringa
Watendaji wa kata ya mlandege wamepewe wiki mbili kuitisha mikutano ya kusoma mapato na matumizi ya kila mitaa ili kupunguza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka viongozi kufanya kazi kwa umakini na kuitisha mikutano ya hadhara kwa wakati ili kupunguza kero zinazowakabili.
"Wananchi wa Kata hii wanakero nyingi ambazo viongozi wa Kata mnaweza kuzitatua sio lazima zinifikie mimi huku,nawaombeni sana viongozi fanyeni kazi la sivyo nitawachukulia hatua mara moja"alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa kata ya mlandege haina changamoto nyingi ili changamoto hizo zinasababishwa na viongozi wa Kata kwa kutofanya mikutano ya hadhara kwa wakati.
Aidha Kasesela alisema kuwa ataendelea kutatua kero zote kwa wananchi kwa kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi na ameletwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kufanya kazi kwa wananchi.
Kero nyingine zilizokuwa hapa Kata ya mlandege zitatatuliwa wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa atazitatuwa kulingana na mipango iliyopo serikalini.
Kasesela alimuomba mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuzipeleka bungeni baadhi kero ambazo zipo juu ya uwezo wao kama kero ya maji,ardhi na swala Mipangomiji.
Kwa upande wake mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati alisema kuwa ameyapokea na anayapeleka bungeni kuyatatua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi wa kero za wananchi.
"Nimekuja hapa kwenye mkutano hadhara kuzichukua kero hizi ili nizipeleke sehemu husika na mimi nitafanya kazi kwa kujituma ili kuisaidia Manispaa ya Iringa kuwa na maendeleo ya haraka sana"alisema Kabati
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa dr mafwele alisema kuwa amezisikia kero zote na atazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili kuboresha maisha ya wananchi wa Manispaa ya Iringa.
1 comments:
Safi sana viongozi wanajisahau sana
Post a Comment