Thursday, May 25, 2017

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA UBUNGO LAAGIZA IDARA YA MIPANGOMIJI KUFUATILIA NA KUTWAA MAENEO YA UMMA

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakiwa kwenye Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Waheshimiwa Madiwani wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakisoma muongozo wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam

Viongozi wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kikao cha Baraza la Madiwan Jumatano Mei 24, 2017
Waheshimiwa Madiwani wakijadili jambo wakati wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma Ally akifatilia kwa makini kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 kwenye ukumbi wa mikutano leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja kwenye ukumbi wa mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akipitia muongozo wa Kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo kwa kauli moja limeridhia na kuagiza Idara ya Mipangomiji na Mazingira kufuatilia na kutwaa maeneo kwa ajili ya matumizi ya Umma hususani maeneo ya Shule.

Aidha Baraza la madiwani limeagiza Idara hiyo ya Mipango Miji kutembelea na kupima eneo la shule ya Sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba ambalo eneo lake limesalia ekari 31 kati ya 22 huku eneo jingine likitumiwa na wananchi kinyume na utaratibu.

Pia imebainika kuwa hali ya ukusanyaji mapato inaendelea kukua kutokana na juhudi na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato tangu kuanza kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo baada ya mgawanyo wa Halmashauri hiyo kutoka Manispaa Mama ya kinondoni.

Akijibu swali lililoulizwa kuhusu ubovu wa mashine za kukusanyia mapato POS Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa hajawahi kupokea malalamiko juu ya mashine hizo na kubainisha kuwa Manispaa imepata mtaalamu anayeshughulikia mashine hizo ambapo atatoa taarifa juu ya kiasi kilichokusanywa tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo za POS.

Akiongelea kuhusu semina kwa madiwani MD Kayombo alikiri kuwa kuna umuhimu wa madiwani kupata semina hususani kwenye eneo la kanuni na sheria mbalimbali na pia katika sheria za manunuzi hivyo ameahidi kuandaa semina hiyo ili waweze kuelimika zaidi.

MD Kayombo akizungumzia suala la maendeleo ya jumla katika kuboresha miundo mbinu katika shule za Manispaa ya Ubungo alisema kuwa zitakuwa zikifanyika hatua kwa hatua katika kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa huku akibainisha kuwa katika kuinua elimu katika Shule za Manispaa ya Ubungo ujenzi wa Madarasa, Vyoo sambamba na Ukuta vitaanza kujengwa hivi karibuni katika shule ya Msingi Ubungo Plaza.

Kuhusu hoja ya malalamiko ya kodi ya Service Levy ambayo Manispaa ya Ubungo  imekuwa ikifuatilia wafanyabiashara walipo kuhakikisha wanalipa kodi aliwataka madiwani kutambua kwamba hakuna mfanyabiashara anayependa kuona analipa kodi hivyo sio rahisi kutokuwa na malalamiko pale wanapolazimishwa kulipa kodi.

Alisema kuwa Manispaa imefanya juhudi kubwa kuwaelimisha juu ya kodi hiyo huku akiahidi kuendelea kuwaelimisha kutokana na wao kutoielewa vizuri kodi hiyo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo alisisitiza umuhimu wa semina kwa madiwani huku akitilia mkazo ulipaji wa kodi.

Alisema Ubungo ina idadi kubwa ya watu hivyo inapelekea kuwepo kwa idadi kubwa pia ya wafanya biashara hivyo kwa asilimia kubwa pato la Manispaa linatoka kwa wafanyabishara zaidi.

Akizungumzia mchakato mmojawapo katika kuongeza mapato alisema tayari mkurugenzi ameeleza kuandaa sheria ndogo ndogo za Manispaa zitakazosaidia katika ukusanyaji wa mapata na kuongeza pato la Manispaa hivyo aliwataka waheshimiwa madiwani kuunga mkono juhudi hizo za ukusanyaji kodi ili kuleta maendeleo.

Baraza hili la madiwani la Robo ya tatu lilikuwa na agenda takribani nane ambapo ikiwemo kuthibitisha taarifa za utekelezaji wa kazi za kamati za kudumu za Halmashauri.

Pamoja na hayo baraza lilikuwa na agenda ya kupokea taarifa kama vile taarifa ya wenye vyeti feki kwa manispaa ya Ubungo, taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya tatu kipindi cha Januari hadi Machi 2017 na taarifa ya utendaji kazi na uwajibikaji wa Halmashauri.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More